Mzee Upako: Kwa akili hizi za siasa za chuki, kujilimbikizia mali na kutukana mabeberu hamtafika mbali

Shida wengi hamuelewi ubeberu ni nini labda hadi muelezwe maana ya ubeberu kwa kingereza. Ubeberu maana yake kwa kingereza ni 'imperialism'. Mataifa makubwa ya ulaya ya magharibi hasa uingereza ufaransa na ubeljiji ni imperialists. Walitawala nchi zingine na wanaendelea kuzitawala kiuchumi. Ubeberu sio tusi. Haohao wanaotupa misaada ndio pia mabeberu. Mabeberu ni pamoja na marekani. Inatawala dunia kiuchumi na wanafanya kila hila kudhibiti uchumi wa dunia.
Nyie mnaowapenda wazungu hadi kupata kichefuchefu tukiwaita mabeberu mnashangaza. Hata wao hawaoni ni ajabu kuwaita mabeberu na hapohapo tukipokea misaada kutoka kwao.
Muache kudanganya wananchi kwamba mabeberu ndio wanawatia njaa.
 
Enzi za hayati watu waliishi kwa akili. Maana ukijifanya msemaji anakuondoa. Bora ubaki utayasema baadae kuliki uyaseme ukaindoka kabla ya kuyamaliza.

Safe mode
Kiukweli mie nashangaa kumbe kila mtu alikuwa anajuwa jamaa hayuko fit hata kiakili, ila walitulia tu hofu ya kudhuriwa na kichaa!
 
,namnukuu"Kwani wamewalazimisha?si mmewaita wenyewe?Si mnasaini mikataba ya kijinga,mnasaini mikataba ya kijinga kama mafala hivi, kwa sababu ya Ubwege wenu na wataalamu wenu mabwege,lazima mjue namna ya kuishi na wakubwa,wazungu ni wakubwa tu.
Na kwa akili hizi mlizonazo kuwafikia wazungu sio leo wala kesho wala keshokutwa,labda kizazi kijacho baada ya hiki chetu
Hao ni wadau wa maendeleo ya nchi yetu sio Mabeberu."
Kwani wewe ni mzungu?...au ndio wale waafrika ukitukanwa kwa uafrika wako utajibu 'hewala bwana'😂
 
Back
Top Bottom