Mzee Upako: Kwa akili hizi za siasa za chuki, kujilimbikizia mali na kutukana mabeberu hamtafika mbali

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Haya yamesesmwa na Mzeee wa Upako Mchungaji Antony Lusekelo ktk moja ya video clip inayoenea mitandap ya kijamii kwa kasi.

Amesema siasa za chuki, uhasama, kujilimbikizia madaraka na mali ni za kijinga na zimepitwa na wakati.

Sikiliza mwenyewe hapa.

Jiwe limetupwa Gizani
 
Kasema Ukweli ila miongoni mwa waliopaswa kuyasikia hayo maneno yake ameshaondoka na alivyokuwa hai alikuwa rafiki yake lakini naona aliogopa kumwambia labda aliona angeharibu uhusiano wao hivyo angekosa mema ya nchi, kwahiyo na yeye ajifunze kutoa ushauri wakati muafaka.
Enzi za hayati watu waliishi kwa akili. Maana ukijifanya msemaji anakuondoa. Bora ubaki utayasema baadae kuliki uyaseme ukaindoka kabla ya kuyamaliza.

Safe mode
 
,namnukuu"Kwani wamewalazimisha?si mmewaita wenyewe?Si mnasaini mikataba ya kijinga,mnasaini mikataba ya kijinga kama mafala hivi, kwa sababu ya Ubwege wenu na wataalamu wenu mabwege,lazima mjue namna ya kuishi na wakubwa,wazungu ni wakubwa tu.
Na kwa akili hizi mlizonazo kuwafikia wazungu sio leo wala kesho wala keshokutwa,labda kizazi kijacho baada ya hiki chetu
Hao ni wadau wa maendeleo ya nchi yetu sio Mabeberu."
 
Jamaa ameewamindi sana. Ikumbukwe hii ni kauli ya Kinabii.
 
Haya yamesesmwa na Mzeee wa Upako Mchungaji Antony Lusekelo ktk moja ya video clip inayoenea mitandap ya kijamii kwa kasi.

Amesema siasa za chuki, uhasama, kujilimbikizia madaraka na mali ni za kijinga na zimepitwa na wakati.

Sikiliza mwenyewe hapa.

Jiwe limetupwa Gizani
View attachment 1933526
Shida wengi hamuelewi ubeberu ni nini labda hadi muelezwe maana ya ubeberu kwa kingereza. Ubeberu maana yake kwa kingereza ni 'imperialism'. Mataifa makubwa ya ulaya ya magharibi hasa uingereza ufaransa na ubeljiji ni imperialists. Walitawala nchi zingine na wanaendelea kuzitawala kiuchumi. Ubeberu sio tusi. Haohao wanaotupa misaada ndio pia mabeberu. Mabeberu ni pamoja na marekani. Inatawala dunia kiuchumi na wanafanya kila hila kudhibiti uchumi wa dunia.
Nyie mnaowapenda wazungu hadi kupata kichefuchefu tukiwaita mabeberu mnashangaza. Hata wao hawaoni ni ajabu kuwaita mabeberu na hapohapo tukipokea misaada kutoka kwao.
 
Back
Top Bottom