Mzee uliahidi pesa zitatiririka kwa wanyonge baada ya kubana mafisadi. Imekuwaje?!

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,867
2,000
Wakati wa kampeni Raisi wetu uliwaahidi Watanzania kwamba ukiingia ikulu utawabana mafisadi na utayafunga kwa Magufuli huko juu ili yaachie pesa zitiririke kwa Masikini. Walikuamini sana. TenaTena kuna kibwagizo chako ulichokuwa unapenda kumalizia nacho cha Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Sina Shaka na dhamira yako, lakini kiuhalisia, eidha uliwahadaa au ulipiga mahesabu yako vibaya. Kwa hali halisi ilivyo mitaani kwa sasa, baada ya Mwaka mmoja kuingia hapo Magogoni kwa kweli hali ni mbaya sana. Hali hii hakuna Mtanzania aliyewahi kuishuhudia Tangu Rais Mwinyi aingie Madarakani hadi awamu zote zilizopita.

Ushauri wangu kwako. Ni Kama ifuatavyo.
1 Tafuta washauri wa uchumi wazuri na ambao hawakuogopi
2. Mshauri wako wa mambo ya siasa mfukuze kazi haraka sana kabla hujaharibikiwa. Uliahidi kuiboresha demokrasia lakini kinachofanyika kwa sasa kila mpenda amani wa nchi hii anakichukia. Kumbuka Tanzania haijawahi kuwa na siasa za chuki, kumbuka ni Tanzania hii ambayo baba anaweza kuwa kuwa chama cha Cuf au CHADEMA na baba akawa CCM na bado wakawa familia moja. Uliahidi Huna chama, lakini kinachofanyika kwa sasa ni Dhahiri kuwa, hukujiandaa kuwa Mwanasiasa au una washauri ambao hawana vision,

3 Jiji Kama la Dar, ni wendawazimu kuwapangia watu wazima Muda wa kutumia visenti vyo. Ati kuna Muda wa kazi na ambao siyo wa kazi. Kumbuka uchumi wa hii Nchi unaendeshwa na sekta binafsi, Ila bado kuna watu wako umewateua wanapenda kukutukuza badala ya kukueleza ukweli ni kana kwamba Nchi iko katika tangazo la hali ya hatari. Raia wa Nchi hii ni mlipa kodi. Anastahili kuwa huru na kulindwa kwa Masaa 24/ Siku 365. Ndiyo maana tuna majeshi yote haya na tunawalipa mishahara kutokana na kodi za Raia wa Nchi hii.

Angalia haya mambo kwa jicho la tatu, jinsi unavyoendelea kuchelewa na ndivyo Wananchi wana endelea kukuona Kama unafanya yasiyofaa, na ndiyo maana wengi wao wameanza kukuita dikteta.

Ukweli mitaani hali siyo nzuri. Kila nyumba kila kaya ni huzuni.je?, ni kweli kuwa watu wote walikuwa wapiga deal? Tafakari. Msimu huu wa mwisho wa mwaka Siku zote huwa ni shamra shamra lakini jaribu kutuma makachero wako wakakuchunguzie, Kama hawakuogopi, basi watakuambia ukweli. Mitaani ni Kama Tanzania imepata msiba mkubwa.

Usipokuwa makini, wapinzani wako kisiasa wanaweza kutumia hali mbaya ya maisha ya Raia na baada ya Muda ukajikuta uko peke yako.

Binafsi nimeshachoka kukuombea.
 

treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,634
2,000
Kwa wale wanaosubiri milioni 50 kila kijiji, mtasubiri sana. Hakuna fedha ya bure nyie wapiga dili.. Pindeni migongo mle kwa jasho lenu., Kisha tukutane 2020 kwa ahadi nyingine kem kem.
 

Super Don

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,490
2,000
Kwa wale wanaosubiri milioni 50 kila kijiji, mtasubiri sana. Hakuna fedha ya bure nyie wapiga dili.. Pindeni migongo mle kwa jasho lenu., Kisha tukutane 2020 kwa ahadi nyingine kem kem.
We unakula kwa kupindisha nn?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom