Mzee Tom Nyanduga nakuunga mkono asilimia zote mia moja.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Kiongozi mkuu wa taasisi ya haki za binadamu Tom Nyanduga ameongelea suala la baadhi ya wana usalama kuwapiga picha raia wenye kufanya makosa barabarani na kuzirusha mitandaoni.

Unaamka asubuhi unakutana na picha za watu ambao baadhi unawafahamu, zikiwa zimerushwa mtandaoni wakiwa wameshikilia mabango yenye kueleza taarifa zao binafsi na makosa waliyoyatena barabarani wakiendesha magari yao.

Makosa ya kutanua njiani na kuendesha gari mtu akiwa kalewa nyakati hizi za krismasi na mwaka mpya. Ndani ya saa moja picha ya mtu aliyekamatwa na polisi na kuamriwa ashike karatasi yenye maelezo ya makosa yake, inakuwa imeshatazamwa na ulimwengu mzima.

Aliyeisambaza ni lazima atakuwa yule mtu aliyehusika katika kumkamata mhalifu wa barabarani. Huu sio uungwana hata kidogo.

Yaani mhalifu ambaye ni jambazi mwenye kuvunja nyumba za watu anakamatwa bila ya sura yake kurushwa hewani kupitia mtandao wa whatsapp halafu mtu ambaye kanywa bia mbili za krismasi nyumbani kwa rafiki yake anadhalilishwa!!.

Yaani yule ambaye anakata viungo vya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi sura yake hatuioni mitandaoni halafu tunakuja kumuona mtu aliyetanua barabarani!.

Siungi mkono tabia ya kuendesha gari mtu akiwa kaonja gambe, pia siungi mkono tabia ya kutanua njiani huku mtu akijifanya ana haraka kuliko aliwakuta barabarani, yote mawili ni makosa.

Lakini upo utu wa mfanya makosa, wapo ndugu na jamaa zake, sio ustaarabu kumuabisha binadamu mwenye makosa ambaye hayana ukubwa kulinganisha na mengi tu yatendwayo na watu ambao sura zao hazirushwi mitandaoni.

Namuunga mkono mzee Tom Nyanduga kiongozi mkuu wa taasisi ya haki za binadamu, katika suala hili la kupiga vita tabia ya kumdhalilisha mtu kwa kosa la barabarani wakati yapo makosa mengi mabaya sana ambayo wanaoyafanya wala hawadhalilishwi mbele ya macho ya wanajamii.

Happy New Year Jamii Forum.
 
Back
Top Bottom