Mzee Sumaye kura za hapana kwa Wengine ni sawa, Ukipigiwa wewe kura za hapana unakataa?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi,

Ule usemi mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu umetimia kwa huyu Mzee Fredrick Sumaye

Mzee Frederick Sumaye anahubiri demokrasia kwa wengine lakini ikitumika kwake na kuleta matokeo asiyoyatarajia anayaiita sio demokrasia
Mzee Sumaye uliingia kwenye kamati kuu ya Chadema bila kupigiwa kura wala hakuna mtu aliyehoji hata wewe mwenyewe ulikaa kimya, Je wewe kuingia kwenye kamati kuu ilikuwa demokrasia kwako wakati yu mgeni kwenye chama cha Chadema?

Sumaye alisimamia mchakato wa kuchagua mwenyekiti wa Bavicha mkuranga mwaka 2017 huku mgombea wa kiti hicho alikuwa mmoja tu Bwana Jerry kilenge , Kura za ndio au hapana zilipigwa na mgombea husika alishindwa mara ya kwanza kwa kura za hapana kuzidi kura za ndio

Mzee Sumaye kama Msimamizi wa uchaguzi huo alirudia uchaguzi huo mara tatu bali kura za hapana mara zote tatu zilizidi kura za ndio hivyo nafasi ikabaki wazi

Je? Mzee Sumaye mbona hakumtetea Bwana Jerry kilenge mgombea pekee wa uenyekiti wa Bavicha Mkuranga aliyeshindwa vibaya mkuranga chini ya usimamizi wake

Je? Mzee Sumaye amesahau haya yote au Yeye pekee alihitaji apigiwe kura za ndio

Peter Msigwa mwaka 2017 alikuwa mgombea wa uenyekiti pekee kanda ya Nyasa na alipigiwa kura za ndio au Hapana, Alipita kwa ushindi mwembamba sana wa asilimia 52% huku point zinazotakiwa ni kuanzia asilimia 50%, Je Sumaye hukuyaona haya

Mzee Sumaye alipoenguliwa mgombea mwezake wa uenyekiti kanda ya Pwani Bwana John Haule alipiga makofi akijiona sasa amebaki peke yake, Mzee Sumaye ulikaa kimya ukifurahia kuwa John Haule mshindani wako hana sifa za kushindana na wewe, Mbona hili tukio hujalizungumza

Kuna mambo yanafikirisha na kuchekesha sana hasa mtu anapoongelea mambo kwa kusahau kutunza kumbukumbu kichwani.

Mzee Sumaye bado anafikiria yeye ni Waziri mkuu hivyo kupigiwa kura za ndio ni lazima na ni heshima kwake

Mzee Sumaye bado anafikiria uchaguzi na mifumo ya CCM kuwa ukibaki peke yako lazima utangazwe mshindi na umepita bila kupingwa, Chadema kupita bila kupingwa hakuna na yeye ni moja wa Mtu aliyesimamia mifumo ya ndio au hapana Chadema

Je, zile ajenda na Propaganda za siri ulizokuwa unatuhumiwa kuwa unatafuta kuwa mwenyekiti ili chama cha Chadema kidhoofike ni kweli?

Kwanini nafasi ya uenyekiti wa chama inakuumiza sana wewe pamoja na wanaccm wenzako uliowahama mwaka 2015

Mzee Sumaye maumivu ya uenyekiti wa Chadema unayopata ndio hayo hayo viongozi wako wa zamani ccm wanayapata, Kwanini mnaumia kwa pamoja wewe na wana ccm wenzako?
 
Kwanini nafasi ya uenyekiti wa chama inakuumiza sana wewe pamoja na wanaCCM wenzako uliowahama mwaka 2015

Mzee Sumaye maumivu ya uenyekiti wa Chadema unayopata ndio hayo hayo viongozi wako wa zamani CCM wanayapata, Kwanini mnaumia kwa pamoja wewe na wana CCM wenzako?
 
Mnapozungumzia mambo ya Sumaye msiitaje CCM maana huko aliondoka kwa mbwembwe.
 
Alisimamia alichokiamini sio mbwembwe hata anavyoondoka sasa anasimamia anachokiamini

Sumaye anaamini Katika kupewa heshima, Hivyo anatumia uwaziri mkuu apewe heshima ya kugombea kila kitu

CCM walipomkataa aliona sio heshima
Chadema Wanaposema kura hapana kwake sio heshima

Fredrick Sumaye anaamini Katika kuheshimiwa tu, Hivyo anapenda ahurumiwe
Mnapozungumzia mambo ya Sumaye msiitaje CCM maana huko aliondoka kwa mbwembwe.
 
Baada ya rafiki yake wa karibu mzee Lowasa kurudi nyumbani, CHADEMA imekuwa na mtazamo hasi na wahamiaji wote. Sio rahisi kuwaamini tena. Mvuto wao na kuaminiwa kwao nako kumetoweka. Inavyoonekana hawa wahamiaji walikuwa na lengo moja linalofanana ambalo ni kupata uongozi wa juu na kisha kutumia nyadhifa zao kubomoa chama. Jambo la kujiuliza ni kwamba huyu Sumaye asingeweza kuheshimika bila kuwa na cheo ndani ya CHADEMA? Je, alihama CCM kwenda CHADEMA kufuata vyeo baada ya kuvikosa CCM? Kwa mtazamo wangu angesema hivi; nimekosa cheo, namfuata swahiba, nalinda mali na maslahi yangu ya kifamilia pamoja na kulinda heshima ya uwaziri mkuu. Onyo kwa CHADEMA. Alipokosea mwenyekiti ni kuwaamini hawa mamluki waliotumwa kwa mkakati maalum. Ni muhinu mzee aelewe kuwa heshima hujengwa kwa hekima na busara ulizo nazo na sio kwa cheo ulicho nacho. Angemuamini Dr. Slaa sasahivi chama na nchi wangezungumza mengine. Naamini mmejifunza mlipokosea. "USIMUAMINI MGENI NA KUMDHARAU MWENYEJI ULIYEISHI NAYE MIAKA MINGI"
 
Kama binadamu namuelewa Sumaye kwa angle hii:-

Kutogombea mtu mwingine yeyote ilimaanaisha kuwa katika kanda hakuna aliyejiona ana ubavu wa kushindana na yeye aliyekuwepo hivyo wakaona bora wajiengue. Hivyo kumpigia kura za hapana ikiwa hakuna aliyechaguliwa ni sawa na kumvua nguo. Otherwise iwe mchakato uliwazuia wengine kushindana nae.

Nachokiona hapa ni mkakati uliopangwa kumdhalilisha mzee Sumaye ili aone hasira na achukue maamuzi aliyochukua. Bora angeshindwa na mtu mwingine kwenye kura.

Huu ni msimamo wangu.
 
Huko chadema kunawaka moto,ukienda tofauti na wenye chama imekula kwako,kuna ubaguzi mkubwa sana,Mbowe ana watu wake kwenye chama chake.kina kunyoosheana vidole ukionekana wa tofauti tu fitina na chuki vitakukimbiza.
 
Kwanini nafasi ya uenyekiti wa chama inakuumiza sana wewe pamoja na wanaCCM wenzako uliowahama mwaka 2015

Mzee Sumaye maumivu ya uenyekiti wa Chadema unayopata ndio hayo hayo viongozi wako wa zamani ccm wanayapata, Kwanini mnaumia kwa pamoja wewe na wana CCM wenzako?
Yaaani MTU una miaka miwili unataka kuwa mwkt.....hata mtoto mdogo anajua una lako jambo......halafu wakionyeshwa democrasia wanalalamika kwaninukibaki peke yako ndo kigezo
 
Mmemuona hana pesa ndio maana hamjampitisha angekuwa na pesa kama Lowasa angepita bila ya kupingwa

Sasa na yeye anajua hana pesa anajibebisha nini kwenye chama? Mbona humo ccm walimkata, au huko nako hakuna demokrasia? Huyo Lowassa aliyepitishwa kwa hela zake alikuwa anagombea nafasi gani kwenye chama? Kwa hiyo Sumaye alivyoona mwenzake kapita bila kupingwa, akaona na yeye ailalie bahati ya mwenzake mlango wazi?
 
Vipi na sababu za Katibu wa hiyo Kanda Bwana Mabina kuachia ngazi?

Huyu si ndiye msimamizi wa huo uchaguzi!!
 
swali langu la msingi ni je?
Kama sasa mnawaita mamluki kila anayewapinga kimawazo na kimaoni.

vipi kuhusu nyalandu abaye kihistoria woote wametokea CCM?

Au kwa sababu bado ana pesa basi huyo sio pandikizi bado?

Naomba mnijibu hili kwanza mengine nitayaleta kadri mtakavyonijibu nyinyi.
 
Back
Top Bottom