Mzee Sumaye: Kuelekea uchaguzi mkuu wapinzani wanapaswa kuwa wavumilivu amani ikitoweka wote tutavurugikiwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,549
Waziri mkuu mstaafu mzee Sumaye ameviasa vyama vya siasa na hasa vya upinzani kuwa na uvumilivu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ili kuilinda amani yetu.

Sumaye amewaasa viongozi wa vyama vya siasa kukumbuka kuwa nchi iliyovurugwa na amani kupotea huwa haitawaliki.
Kwahiyo pasipo na amani sote tutavurugikiwa pasipo kujali itikadi na hata hao wapinzani wakishinda wakati amani imetoweka watatawalaje?....ameuliza Sumaye

Mzee Sumaye alikuwa akihojiwa katika kipindi kilichorushwa na Star tv.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Hahaha, Yani wapinzani wao ni wa kuvumilia miaka na miaka, acha damu imwagike kwani hata damu ikimwagika haichagui huyu ni mpinzani hivyo hata ya CCM nayo itamwagika tena sana tu

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Mkuu punguza uchawi!
 
Ni baada ya wale wazee wawili (Kinana na Makamba) kuambiwa kwamba kama wamejiweka pembeni na CCM basi wakae hivyohivyo bila kuvuka upande wa pili.

Ilitegemewa wale ndo pengine wangekuwa chachu ya upande wa upinzani.

Sumaye amesoma alama za nyakati.
 
Hahaha, Yani wapinzani wao ni wa kuvumilia miaka na miaka, acha damu imwagike kwani hata damu ikimwagika haichagui huyu ni mpinzani hivyo hata ya CCM nayo itamwagika tena sana tu

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Ya wewe?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom