Mzee Sumaye: Kuelekea uchaguzi mkuu wapinzani wanapaswa kuwa wavumilivu amani ikitoweka wote tutavurugikiwa

Waziri mkuu mstaafu mzee Sumaye ameviasa vyama vya siasa na hasa vya upinzani kuwa na uvumilivu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ili kuilinda amani yetu.

Sumaye amewaasa viongozi wa vyama vya siasa kukumbuka kuwa nchi iliyovurugwa na amani kupotea huwa haitawaliki.
Kwahiyo pasipo na amani sote tutavurugikiwa pasipo kujali itikadi na hata hao wapinzani wakishinda wakati amani imetoweka watatawalaje?....ameuliza Sumaye

Mzee Sumaye alikuwa akihojiwa katika kipindi kilichorushwa na Star tv.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Habari kama hzi muwe mnaweka clip kuliko kuchagua maneno unayopenda watu wayasome...context ni muhimu!
 
Hahaha, Yani wapinzani wao ni wa kuvumilia miaka na miaka, acha damu imwagike kwani hata damu ikimwagika haichagui huyu ni mpinzani hivyo hata ya CCM nayo itamwagika tena sana tu

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Hapana.Nakupinga damu isimwajike wavumilie tu hamna namna!
 
Huyu Mzee atakuwa ametumwa,kwanini asiwaambie CCM ambao ndiyo watailetea machafuko hii nchi kwa kulazi.isha kutawala wakati wamezeeka?Nchi yetu sote hii.
 
Waziri mkuu mstaafu mzee Sumaye ameviasa vyama vya siasa na hasa vya upinzani kuwa na uvumilivu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ili kuilinda amani yetu.

Sumaye amewaasa viongozi wa vyama vya siasa kukumbuka kuwa nchi iliyovurugwa na amani kupotea huwa haitawaliki.
Kwahiyo pasipo na amani sote tutavurugikiwa pasipo kujali itikadi na hata hao wapinzani wakishinda wakati amani imetoweka watatawalaje?....ameuliza Sumaye

Mzee Sumaye alikuwa akihojiwa katika kipindi kilichorushwa na Star tv.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!

Kuna ugonjwa fulani wana ccm wanaugua ambao bado haujajulikana
 
Wavumilie muda wao wa kutawala bado maana hawana jipya zaidi ya ku copy na ku paste kutoka chama tawala.

Niambie lini wapinzani walisimamisha mgombea awe rais au ubunge hana chembe chembe za chama tawala?
Kwani wewe ulishushwa toka mbinguni huna chembechembe za wazazi? Unadhani kabla ya mfumo wa vyama vingi watu walikua hawafanyi siasa? Na kama walikua wanafanya watitumia chama gani?. Chembe si hija, hoja ni maono na dhamira mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri mkuu mstaafu mzee Sumaye ameviasa vyama vya siasa na hasa vya upinzani kuwa na uvumilivu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ili kuilinda amani yetu.

Sumaye amewaasa viongozi wa vyama vya siasa kukumbuka kuwa nchi iliyovurugwa na amani kupotea huwa haitawaliki.
Kwahiyo pasipo na amani sote tutavurugikiwa pasipo kujali itikadi na hata hao wapinzani wakishinda wakati amani imetoweka watatawalaje?....ameuliza Sumaye

Mzee Sumaye alikuwa akihojiwa katika kipindi kilichorushwa na Star tv.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Angalizo Jema ila Lina chembe za UNAFIKI na U-CHAMADOLA, ukipigania AMANI lazima USIMAMIE HAKI , sasa unaposema vyama vya upinzani una maanisha nini?, kwa nini usiseme vyama vya siasa kiujumla ?, Mpaka uanze kuweka mafungu na wengine kuwasisitiza kwa kumpendelea MBUZIJIKE?, kwani kati ya wapinzani waliozuiwa kufanya Siasa huru kwa kuzingatia mipaka ya kisheria na Huyu mpambana na MABEBERU Aliejipa uhuru yeye na genge lake ni nani MCHAFUZI WA HAKI?, ama hajui kama kuchafuliwa haki ndio chanzo cha kuchafuka AMANI?. HITIMISHO:
Unapo toa angalizo kwa Maslahi ya Taifa kuwa MZALENDO na msingi wako uwe ukweli. Kama kuna ki-MbuziJike unakiogopa bora Ukae kimya kuliko kutoa ushauri ambao bado una ubaguzi ndani yake.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom