Mzee: Sory kijana kama nimekutisha, unafanana sana na Mwanangu aliyefariki

mbwana semsimbazi

Senior Member
Sep 5, 2013
196
202
Copied somewhere...

Leo nimeingia Supermarket pale Kibo Complex Tegeta,..Basi nikachukua Mkate Mkubwa na Maji,
Ajabu tangu nachagua bidhaa kwenye Shelf kuna Mzee mmoja alikuwa ananifuata nyuma mpaka nikaogopa,
nikaenda kaunta kwa Cashier bado ananifuata nyuma!,
Nikarudi kwenye Shelf kuchukua Soda bado Mzee yupo! Duh!
MZEE : Sory kijana kama nimekutisha, unafanana sana na Mwanangu aliyefariki juzi na kuzikwa Makaburi ya Kinondoni,
MIMI: kwa hiyo mzee unataka kusema nini?
MZEE : bahati mbaya Mwanangu amefariki bila hata kusema bai, naomba unisaidie kitu kimoja, wakati naondoka nikikupa Mgongo walau useme BAI BABA! Ili nijisikie kama niliagwa na Marehemu Mwanangu jamani!, nisaidie (akatokwa machozi)
MIMI: hilo tu? Usijali Mzee!.
Kisha Mzee yule akachukua bidhaa zake mafurushi kibao mpaka pale kaunta akahesabiwa vitu vyake akabeba na kunipa Mgongo ili nitimize alichoomba.
MIMI : Bai baba!
MZEE: Bai Mwanangu Mpenzi, asante!!
Mzee yule alipoondoka nikaenda Kwa Cashier na kupigiwa hesabu
CASHIER : Kaka Unadaiwa Tsh 238,500/=
MIMI : kivipi? Yaani Mkate, Maji na Soda pesa yote hiyo? Acha Wizi wewe dada!!
CASHIER: wewe unadaiwa sh 8500 na Baba yako amesema unamlipia bili yake sh 230,000/=
Ngachoka kabisa!...By the way bado nipo hapa napiga Misamba na madekio!...leo nipo night shift, Korido ya juu kule TRA nitadeki kwa Ulimi!....Bai BABA!
 
teh teh teh...
silly.jpg
 
Naona huyo aliyeianzisha thread alikuwa na muda wa kutosha kuandika story.Hata hivyo sikulaumu wewe ume copy na ku paste!
 
daaaaah,kidingile hiko noma sana aisee,kacheza kama pele vile,by the way,mpe pole sana huyo mkuu aliyetokewa na tukio hili kama ni kweli
 
Back
Top Bottom