Mzee Siro ile Vita yako na Ma-RPC waliokuwa wanataka U-IGP iliisha au inaendelea? Nadhani toka adharani uwakemee Tena wajue unawajua

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mzee Siro ni Moja ya IGP aliyewahi kuongoza jeshi kipindi Kuna mauaji mengi Sana akifutiwa Kwa karibu na Mzee Mahita. Siro amepokea jeshi kipindi Cha saga la Kibiti na Toka hapo mauaji yaliendelea Hadi Sasa.

Nakumbuka Kuna kipindi mauaji yalizidi na uhalifu kuongezeka enzi ya Magu akawaita ma RPC na Makamishna wake akawaeleza wazi kwamba anajua IPO Vita yakutaka aondelewe kwenye hiyo Nafasi. Baada yakuwa mkali Sana uhalifu ulipungua Kwa sababu alifanya pia mabadiliko ya uongozi. Kwa maana nyingine ni kweli wapo watu walitaka kumkwamisha wakidhani watakuwa IGP.

Leo Hii Tena naona uhalifu hasa mauaji yameongezeka kwa kasi ya ajabu. Viongozi wa polisi wapo relaxed hakuna seriousness unayoiona. Lakini pia mitandaoni Kuna hashtag yakutaka Siro aondoke ofisni Kwa kushindwa kazi. What I can advice Siro lazima awe mkali Kwa walio chini yake. Vita Hii ikiendelea wanaoumia zaidi ni wananchi na siyo viongozi wanaowaza kupat IGP. Atoke adharani na akemee.

Lakini pia Kwa Mhe. RAIS, Nadhani mbinu Hii ya watu kushindwa kusimimia usalama Kwa LENGO la kumgombanisha IGP na mamlaka ya uteuzi asiliruhusu kwenye utawala wake. Endapo Siro ataondoka Kwa presha ya waliochini yake basi hata huyo mpya atakayeingia atodumu Kwa sababu Naye atahujumiwa na pia atakosa confidence Kwa sababu ataamini akikaza sana watamwekea zengwe ataondolewa

Mhe. RAIS atoka adharani amkingie kifua mteule wake naamini ma RPC na Makamishna wa Polisi wataacha kuwaza kuwa IGP na badala yake watachapa kazi.

Jambo la Mwisho Kwa Mzee Siro; Pandisha wenzako vyeo. Usiwazibie Kwa sababu ya kuwakomoa. Waliingia Polisi wapande vyeo na wastaafu wakiwa na maslahi mazuri, mbembeleze RAIS awapandishe wenzako vyeo wamekaa miaka mingi sana kama Malisa alichoandika ni sahihi. Mamlaka ya kupandisha vyeo ni Mhe. RAIS ila Wewe unakutana naye daily mwambieni umuhimu wa kuziba matobo kwenye chombo chenu.

Hakuna jeshi lenye nidhamu litazaliwa eneo ambalo juniour ataamka asubuhi akawa senior. Pandisheni Ma. RPC vyeo uhalifu utapungua. Wamekata tamaa.

Ni mtizamo wangu
 
Kwamba askari wasipopandishwa vyeo matokeo yake wanaanza kuua raia wasio na makosa?

Hainiingii akilini.

Kama ni hivyo basi jeshi lifumuliwe lote.

Hii dhana ya kuajiri watu waliofeli ni kati ya mambo yanayonipa wasiwasi sana.
 
Muroto alikuwa moto balaa... Mambosasa alikuwa moto kinyama.. HAHAHA... Mambosasa Lazaro sasa hata hajulikani alipo.....
 
RPC wengi wana vyeo vya ACP na SACP sio rahisi kupiga mbizi ya moja kwa moja kuwa IGP hivyo sidhani kama RPC anaweza kuingia ligi ya IGP
 
Back
Top Bottom