Mzee Shomari: Wakazi wa Dar bila kujali itikadi zetu twendeni tukasherekee mafanikio ya CCM kesho

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mimi nipo Kisarawe kwa muda kesho alfajiri nitaanza safari na baiskeli yangu aina ya Swala ambayo niliinunua mwaka 1987. Nakuja mpaka uwanja wa BWM. Kwa nia moja tu kusherehekea mafanikio ya CCM ndani ya miaka mitano.

Mfano makusanyo ya kodi ilikuwa bil 800,sasa zinakusanywa wastani wa tril 1.6, haya ni mafanikio ambayo lazima tusherehekee hata kama ni mwanaChadema.

Fedha hizi zimetumika kuimarisha sekta ya afya, elimu miundo mbinu na sekta ya nishati,maana hata vijijini kuna umeme.

Mfano tu stand ya Mbezi ambayo imejengwa kwa muda mfupi,ni mfano mzuri wa namna pesa zimesimamiwa vizuri maana imeghalimu bil 70. Na hii stand ya kisasa itamnufaisha kila mtanzania,awe Cuf,Chauma au CHDEMA.

Kwa hiyo nawahamasisha twendeni tukasherehekee mafanikio ya Serikali ya CCM bila kujali itikadi zetu maana imetufanyia makubwa. Najua Chadema mna maumivu makubwa lakini twendeni tu maana maendeleo hayana vyama.
 
Ila usisahau makusanyo yote ya halmashauri kwa kipindi hiki yameelekezwa hazina na wakatu ule 800B yalikuwa yanabakizwa kwenye Halmashauri za miji na majiji
 
Mods mpeni Mzee Shomari User Id, ili awe anarepoti habari na hekaya zake bila kupitia kwa mtu mwingine
 
Back
Top Bottom