Mzee Shomari kumuita Membe kachero mbobezi ni kumvimbisha kichwa. Hana sifa kama za kachero mbobezi na mzalendo Agustine Lyatonga Mrema.

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Huyu mzee ni muuza kahawa maarufu jijini Dar es salam na anasema historia ya nchi nii ipo kiganjani kwake. Anasema watu wanaomuita Bernad Membe eti ni kachero mbobezi hawajui historia ya Tanzania kwa undani. Maana kama ni ukachero Membe hawezi fikia hata robo ya ya umahiri wa Mrema.

Mzee anasema Mrema yupo vizuri na anajua kila kitu kuhusu uzandiki na mbinu zote za kikachero. Mzee Shomari anasisitiza kuwa Mrema kumuunga mkono Magufuli wa CCM ni sababu anajua namna Magufuli anachukia ufisadi kama yeye Mrema alivyo.

Bernad Membe anayo historia gani ya kuchukia ufisadi? Maana akifunuliwa hapo alipo ananukia ufisadi. Lakini Mrema alikuwa Dso kahama miaka ya nyuma kila mtu alimuogopa. Pia alikuwa waziri wa mambo ya ndani alipambana na ufisadi kama anavyofanya JPM. Alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alikuwa halali kwake kuhakikisha mafisadi wanakamatwa.

Ni kashfa nzito ambazo zilihusu ufisadi zilisababishwa akafukuzwa CCM. Sasa safari hii ameona CCM ina kiongozi anayepinga ufisadi kama yeye ndio maana amemuunga mkono 100%.

Mzee Shomari ameninog'oneza kuwa Membe sio kachero mbobezi kama Lyatonga Mrema bali ni mjanjamjanja tu. Na wanaompaisha hawaijui hii Tanzania vizuri. Maana Mrema alikuwa akiongea majambazi wanasalimisha bunduki wenyewe. Ila ameshauri Chadema na Act wamtumie Membe kama mgombea wao ili kufuta aibu!
 
Sawa
 

Attachments

  • IMG-20200703-WA0023.jpg
    IMG-20200703-WA0023.jpg
    47.8 KB · Views: 1
Halafu mwaka 2025 utasikia pia limtu likisema "Kumuita G Sam kachero mbobezi ni kumvimbisha kichwa, hawezi kuwa kama kachero mbobezi Benard Membe"
Hii ndiyo Tanzania ya walamba viatu.
Huyo G Sam ana nini alichokifanyia Tanzania? Mbona mzee Shomari hamjui?
 
Bernad Membe anayo historia gani ya kuchukia ufisadi? Maana akifunuliwa hapo alipo ananukia ufisadi.
BM ni EL asiye na nywele nyeupe tu! Hiyo ndio sifa yake,

Hana sifa yoyote na hajawahi kuwa na sifa ya kuchukia wizi na Ufisadi, na hajawahi kujiepusha na vikao vyovyote viyenye kupanga namna ya kuiibia nchi na kwa Hilo Hana aibu, kumbuka pesa za Gadafi
 
Back
Top Bottom