Mzee Samwel Sitta mbona hata huchangii utumbuaji majipu?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Imenilazimu nimtafute aliko Mzee wetu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mh.Samwel Sitta .Mzee huyu amekuwa kimya sana wakati nchi chini ya Mh.Magufuli inapambana kutumbua majipu.

Nilitegemea Mzee huyo angeshiriki vita hivi vigumu japo kwa kumwonyesha kwa kidole jipu lolote analolijua ili Mh.Magufuli alitumbue,lakini mzee huyu amekuwa kimya sana.

Mzee Sitta uko wapi?
 
Aliwahi kumuomba JK aongeze ka ukali kidogo ili mambo yaende, nahisi anafurahia sana utendaji kazi wa JPM.
 
Imenilazimu nimtafute aliko Mzee wetu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mh.Samwel Sitta .Mzee huyu amekuwa kimya sana wakati nchi chini ya Mh.Magufuli inapambana kutumbua majipu.

Nilitegemea Mzee huyo angeshiriki vita hivi vigumu japo kwa kumwonyesha kwa kidole jipu lolote analolijua ili Mh.Magufuli alitumbue,lakini mzee huyu amekuwa kimya sana.

Mzee Sitta uko wapi?
Wewe ukiwa kwenye foleni ya kusubiri kukamuliwa, huwa unapiga kelele au kunyoshea vidole wakati hujui lako (katiba iliyompendeza) litakamuliwa vipi. Subirini zamu ifike kama mnataka kusikia sauti ya mkamuliwaji kama atapiga mayowe au kimya kimyaaa
 
Amestaafu siasa, na sasa amejikita katika utunzi wa vitabu. Tusubiri vitabu vya kusisimua kwani ana hazina iliyostirika ya siasa za Tz.
 
Yale ya bandari yalikuwa yanamfikia akaona atoe kauli ya kupuuzi ili kufifisha utumbuaji, sasa unategemea aongee nini wakti nae ni jipu?! lazima apotezee tu.
 
Amestaafu siasa hivyo ameamua kufuata miiko ya kustaafu siasa ikiwa ni pamoja na kutoropoka hovyo
 
Yeye mwenyewe anamajipu mpaka nyuma then wategemea aongee nini kwa Magufuli? Ila naomba kujuzwa nyumba aliyopangiwa na serikali imerudishwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom