Mzee Sabodo KUSAIDIA UPINZANI SIO TATIZO: Nape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Sabodo KUSAIDIA UPINZANI SIO TATIZO: Nape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Freemanson, Jul 6, 2012.

 1. F

  Freemanson Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MZEE SABODO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO.

  Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema.

  Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.

  Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote haya yamefanywa na serikali ya CCM.

  Sasa kama serikali ya CCM imefanya, cha ajabu hapa kwa mwanachama wake kufanya ni nini? Hivi kwanini tunataka kuwafikisha watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!

  Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!! Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni nini?!

  Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!


  HII NIMEIKUTA KWENYE FB YA NAPE. KUNA KIPINDI ANAWAZA KAMA ZAMANI KABLA HAJANYWESHWA MAJI YA BENDERA!
   
 2. H

  Honey K JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kauli hii ya Nape, Chadema hapa wameingia choo cha kike! Hili tonge lazima liwakabe kooni na hakuna wa kuwasaidia litakapo wakaba! Masikini Chandimu! Bye bye Chadema, kifo chako HAKIEPUKIKI!
   
 3. N

  Nipe tano Senior Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Do! Wamebugia ndowano! Soon wataanza kulia oooh nuhu awafungilie safina!!! Naye atawajibu funguo hana!!! Chadema byebye, hakika kifo chenu HAKIEPUKIKI


   
 4. A

  ACHEBE JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 348
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Honey, sweetheart kumbe ile gongo ilikulevya???
   
 5. A

  ACHEBE JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 348
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nipe tano ningekutana na wewe barabarani ningekunyonya macho!!! Walai, juzi nimemaliza ban sasa unanitafutia ban nyengine hapa
   
 6. F

  Freemanson Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye FB yake kuna kijana kaandika...KAWASAIDIA SANA MAGAMBA KWENYE HILI!
   
 7. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Mamilioni ya Sabodo yaitesa CCM

  • WANACHAMA WATAKA AONDOLEWE CHAMANI

  na Asha Bani na Abdallah Khamis
  MISAADA inayotolewa na kada wa CCM na mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Mustafa Sabodo, kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sasa inaonekana kuwagawa makada wa chama hicho tawala.

  Baadhi ya makada wamekuwa wakitaka Sabodo atimuliwe kwenye chama hicho kwa madai ni msaliti na mwenye lengo la kuiimarisha CHADEMA inayoonekana kutishia utawala wa CCM.

  Miongoni mwa makada wa CCM ambao kwa wakati tofauti walitaka Sabodo atimuliwe ndani ya chama hicho ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.

  Harakati za makada hao kutaka Sabodo atimuliwe jana ziligonga mwamba baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kuunga mkono hatua za Sabodo kukisaidia CHADEMA.

  Nape aliwataka Watanzania wengine waige mfano huo, kwakuwa itikadi za kisiasa haziwezi kuwakwamisha wananchi wasishirikiane.

  Katika taarifa yake iliyowekwa katika mtandao wa kijamii wa Daily Nkoromo, Nape alisema kuwa haoni tatizo kwa Sabodo kukisaidia CHADEMA hasa katika suala la upatikanaji wa visima kwa kile alichoeleza watakaonufaika na visima hivyo ni Watanzania wote pasipo kujali vyama vyao.

  Kauli hiyo ya Nape ambaye ndiye msemaji wa CCM, inapingana na kauli za makada wengine ndani ya chama hicho juu ya mtazamo wa kuendelea kumkumbatia Sabodo anayejipambanua na wafanyabiashara wengine katika kuhakikisha mageuzi ya kweli yanapatikana nchini.

  Nape alisema uamuzi wa kutoa ufafanuzi huo ni kutokana na maswali mbalimbali yanayoelekezwa kwake na watu tofauti juu ya hatima ya michango inayotolewa na Mustapha Sabodo kwa CHADEMA, pamoja na matamshi yake dhidi ya CCM.

  "Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa CHADEMA. Kimsingi sioni tatizo katika hili, la muhimu ni yeye kuendelea kuwa mwanachama muaminifu wa CCM," ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Nape.

  Alisema kama kuna mwanachama wa CCM atakayekuwa na shaka juu ya uungwana huo wa mzee Sabodo itampasa arejee maamuzi ya serikali ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na aangalie utaratibu wa kuvipatia vyama ruzuku, kwa kile alichoeleza kuwa ulikuwa na lengo la kudumisha umoja kwa kuviwezesha kufanya kazi ya kuikosoa serikali na kuhimiza maendeleo.

  Aliongeza kuwa wenye fikra ya kuona mzee Sabodo anakisaliti Chama Cha Mapinduzi watakuwa si wanasiasa wa kweli na Wana CCM
  waaminifu wanaoitakia mema Tanzania.

  "Hivi kwanini tunataka kuwafikisha Watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!....wapo wanaohoji kwanini mzee Sabodo ametoa visima kwa CHADEMA? Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi zao au kila mwananchi ana uhuru wa kutumia? Tatizo hapa ni nini? Narudia sioni tatizo kwa mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!" alisema Nape.

  Mzee Sabodo licha ya kuwa ni kada wa CCM mara nyingi amekuwa akijitokeza wazi wazi kuisaidia CHADEMA katika masuala mbalimbali
  ya kifedha.

  Miongoni mwa misaada yake ni pamoja na kuahidi kuchimba visima katika majimbo yote yanayoongozwa na CHADEMA, ikiwa ni pamoja na kuahidi kuwapatia jengo lenye ofisi za kisasa zitakazoendana na hadhi ya chama hicho.

  Mbali na ahadi hiyo, mzee Sabodo aliwahi kukaririwa akisema anatamani CCM ishindwe katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kwamba
  yupo tayari kumchangia mgombea urais kupitia CHADEMA.
   
 8. F

  Freemanson Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakaribisha, NARUDIA NAKARIBISHA WATUKANAJI
   
 9. M

  Makupa JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  honhera sana nape umeonyesha ukomavu wa kisiasa, big up
   
 10. F

  Freemanson Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watukanaji wamesepa?????????!!!!!
   
 11. L

  Liky Senior Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kwa hili nape umesema vyema.mi nahisi unaongoza watu wasiojielewa.hawajui maana ya multipartism.big up bro!
   
 12. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Upinzani si uadui kama wanavyodhani akina wasira na mwigulu. Kwa mara ya kwanza nakupa hongera Nape kwa kuonyesha ukomavu kwenye hili.
   
 13. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  unamaanisha nini? inamaana hii post imewekwa ili wachangiaji watukane? haueleweki kabisa
   
 14. F

  Freemanson Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWASABABU kila jema la dogo huyu hapa hutukanwa tu
   
 15. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  He?! Una hamu ya matusi? Haya chukua hilo basi!

  F..K You!!! Umefurahi sasa?

  Ukitaka mengine sema....
   
 16. F

  Freemanson Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ungekuwa na akili sana ungetoa mapya kabisa, hilo si umefundishwa na mamaako jana, tafuta lako ndo utaonekana mjanja
   
 17. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Haya basi...wewe ina akili zaidi.... Umefurai sasa?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu, nnamashaka napo. Hawa Magwanda wanaweza kukunyima maji ukiwa wewe CCM. Kuna picha humuhumu JF hata keki kwa kuwa ina rangi za CCM mbunge wao "Halima" Mdee, anaikataa. Hawa roho zao za kutu wala usiwawekee dhamana kusema katika hivyo visima wanaweza kuwapa maji watu wote.

  Kanisani Sumbawanga wameshawagawa waumini walioipigia kura CCM itakuwa maji? hata mungu wao walifikiri ni gwanda!
   
 19. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Masaburi@work, nani akutukane? kwa lipi hasa? umeishiwa mbinu za ki-freemason. Kacheze na watoto wenzako FB.:israel:
   
Loading...