Mzee Sabodo amshauri Raisi kupunguza mawaziri

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Hii ni habari iliyoripotiwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Jamboleo la siku ya leo tarehe 26/12/2016.

Chanzo:Habari za magazetini.
 
Wewe acha tabia za kikaburu za kubagua watanzania wenzetu kwa sababu wanatofautiana mawazo na sisi, huyo mzee ametoa ushauri mzuri
Ndivyo unavyojidanganya kuwa huyo ni mtanzania mwenzako, mwenzako!. Mawazo ya ukada hayo bila own reasoning!
 
Huyo mzee kaona mbali,
Kwa mwendo huu wa JPM (one man show) hata bunge litafikia ukomo.
Tusubirie
 
It is a pity, nchi zetu hizi jamani. Mwafrika unaweza kusema lolote jinsi India itakavyoendeshwa. Ponjolo, amekuja kuchuma achume atuachie nchi yetu. This for Africans not Indians. Alipo hapo ana passport za India, Uingereza, Tanzania, Canada! They are always like that with multiple nationalities
Huu ubaguzi usiutumie kuwaziba midomo watu wenye Asili ya Asia na kwingine Kumbuka Tanzania ni Nchi iliyopinga Ubaguzi wa Rangi kwa miaka yote,huyo mzee ni Mtanzania anayo haki ya kushauri au kutoa maoni yake kama Mtanzania yeyote kwani yy pia anajua hali ya Uchumi ni mbaya gharama za kuwalisha kuwahudumia kuwalipa mishahara mawaziri ni kubwa sana huku huduma zingine zimedumaa.
 
Ningemuunga mkono kama angeshauri mikoa ipunguzwe!
Vyeo vinginevyo kama katibu tawala vifutwe hata wakuu wa mikoa navyo havitumiki Nchi nyingi mfano kenya wao hawana wakuu wa mikoa wana wakuu wa majimbo ambao hupatikana kwa kuchaguliwa na wananchi ni kama marekani napo hawana vyeo vya wakuu wa mikoa kwani walishituka kitambo wakavifuta hata Africa kusini hawana vyeo vya wakuu wa mikoa,katiba mpya ikija inafaa ifute wakuu wa mikoa ije na mfumo bora wa kiutawala usiokuwa mzigo kwa walipa kodi.
 
Wakuu wa mikoa na wilaya waondolewe wote ni mizigo
Nchi zote zilizoendelea Duniani ikiwemo China,Japan,German,UK ,America hata barani Africa kama South Africa na Zinginezo hawana cheo kinaitwa mkuu wa mkoa, walifuta hicho cheo siku nyingi kwani ni mfumo Analogia wa kutawala,hata zile Nchi zilizokumbatia Ukuu wa mikoa zimedumaa kimaendeleo kama Tanzania.
 
Hii ni habari iliyoripotiwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Jamboleo la siku ya leo tarehe 26/12/2016.

Chanzo:Habari za magazetini.
HUYU BABU ATUSHAURI KUHUSU BIASHARA MAANA HUKO KAFANIKIWA,ASIJICHANGANYE NA MAMBO YASIYOMUHUSU
 
Tangu lini utanzania uwe kwa kigezo cha uzao wa rangi? Wewe mchangiaji una ushahidi gani kama wewe ni Mtanzania kwa vinasaba vya babu zako? Pengine asili yako ni Malawi, Afrika kusini, Ethiopia nk. Huwez kuingiza ubaguzi huo. Kama kuwa na uraia zaidi ya sehemu moja na wewe kaombe wa Canada, US, India nk, hukatazwi.
Hujui unachoongea!
 
Wangepunguzwa wa bunge maana wamejaa kibao sioni jipya kila siku matatizo yaleyale ningefurahi katiba ingeruhusu.
 
Ningemuunga mkono kama angeshauri mikoa ipunguzwe!
Mkuu umegonga point kubwa,wingi wa mikoa unaongeza viongozi wengi na kuongeza gharama kwa mwananchi.Kwa kisingizio cha wingi wa watu.Swali Tanganyika au Tanzania tulikuwa takiribani milioni 8 tukiwa na raisi mmoja sasa tuko milioni zaidi ya 40 ina maana kama kigezo ni wingi wa watu tungekuwa na maraisi watano wa nchi tano badala ya mmoja.
 
Huko india Uzembe wa wanafunzi kufanyiwa unyama upo kwa balozi wa Tanzania kwani endapo angesimama kidete kuwatetea na kulaani huo unyama serikali ya india ingechukua hatua,hata kule china watanzania wengi hunyanyaswa na wachina kutokana na Ubalozi kuwa wa hovyo hawana msaada kwenye balozi nyingi huko nje wamelala sana hawatekelezi wajibu wao ipasavyo.
Kwa nini wawafanyie waafrika? na sio wazungu? Wa asia wenzao? Come to your senses kijana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom