Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,788
30,084
MZEE RUKHSA SAFARI YA MAISHA YANGU

Leo nimeingia Maktaba nikawa naangalia makala ambazo nimeandika kuhusu mambo tofauti ya serikali wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Kilichonifanya nifanye hili ni kule kusoma sehemu za kitabu cha Mzee Mwinyi na katika kusoma huko kukanikumbusha baadhi ya matukio muhimu ambayo yalinisukuma kuandika makala wakati mwingine katika magazeti ya nje kama inavyoonekana katika picha - Africa Events na New African yote majarida yakichapwa London na wakati mwingine tukiandika katika magazeti yetu ya ndani.

Hapa nitacheka kidogo kwani ujana hakika una raha zake, wakati mwingine tukiandika kutoka ''msituni.''

Kwa hakika kipindi cha utawala wa Mwinyi hakupungukiwa na watu waliokuwa wanaona raha kumshambulia.

Ilisikitisha kuwa kulikuwa na magazeti yalimpa nafasi Reverend Mtikila kumshambulia Rais.

Kuna baadhi ya vijana wa wakati ule waliona wana wajibu na dhima kubwa ya kumtetea Rais pale ilipodhihiri kuwa hakuwa na mtetezi.

Nilikuwa mmojawapo wa vijana walioamua kumtetea Rais Mwinyi.

Namsoma Rais Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Historia ya Maisha Yangu,'' na natingisha kichwa kwa mengi ninayokutananayo.

Natingisha kichwa kwa kuwa baadhi ya matukio na mambo yaliyomo kitabuni mimi na wenzangu tuliyafahamu kwa undani na tuliyaandika kwa yale yaliyostahili kuandikwa na mengine tuliyanyamazia.

Ninapotembea katika Maktaba hakika inanikumbusha mengi na kuwaleta wenzangu wengi tuliokuwa pamoja baadhi wameshatangulia mbele ya haki.

Maktaba inanikumbusha watu muhimu sana wa nyakati zile kama Augustine Mrema Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Waziri Mkuu, Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro na Mchungaji Christopher Mtikila Muasisi na Kiongozi wa Full Salvation Church.

Hakika zile zilikuwa nyakati za aina yake.

1626668879875.png

1626669018293.png

Africa Events March 1993

1626669127220.png

New African November 1989

1626669154751.png

Mchungaji Christopher Mtikila Muasisi na Kiongozi wa Full Salvation Church

1626671468725.png
Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro
 
View attachment 1859211
View attachment 1859212
Africa Events March 1993

View attachment 1859213
New African November 1989

View attachment 1859214
Mchungaji Christopher Mtikila Muasisi na Kiongozi wa Full Salvation Church

View attachment 1859236
Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro
Muft ndio umemalizaaa!!!!!!!! Aiseee
 
Muft ndio umemalizaaa!!!!!!!! Aiseee
Muuza Viatu,
Naamini unanifanyia maskhara kwa kuniita ''Mufti.''

Maskhara baina ya watu ni dalili nzuri ya mapenzi na kuelewana ila kwa wewe kutumia neno hilo kwangu halifai.

Nakusihi tafuta neno lingine la kunitania.

Hiyo makala nimeweka kama nilivyoeleza baada ya kuingia Maktaba.

Ukweli ni kuwa kuna mengi sana ningeweza kuandika kuhusu kitabu cha Mzee Mwinyi khasa kwa yale ambayo niliyajua kutoka vyanzo vingine.
 
Asante sana Mzee Mohamed Said, kwa kutujuza kuhusu Makala za Mzee Rukhsa!
 
Muuza Viatu,
Naamini unanifanyia maskhara kwa kuniita ''Mufti.''

Maskhara baina ya watu ni dalili nzuri ya mapenzi na kuelewana ila kwa wewe kutumia neno hilo kwangu halifai.

Nakusihi tafuta neno lingine la kunitania.

Hiyo makala nimeweka kama nilivyoeleza baada ya kuingia Maktaba.

Ukweli ni kuwa kuna mengi sana ningeweza kuandika kuhusu kitabu cha Mzee Mwinyi khasa kwa yale ambayo niliyajua kutoka vyanzo vingine.
Ustaadhi Mohamed akiwaza: ''Rais Mwinyi alishambuliwa kwa sababu ya dini yake na hakuna aliyemtetea. Ona na sasa mama Samia ameanza kushambuliwa kwa sababu ya dini yake ndiyo maana nimekumbuka ya nyuma.... kipindi cha Mwinyi''
Unakosea sana ndugu yangu. Mwinyi alishambuliwa kwa sababu ya uongozi wake mbovu. Magufuli alishambuliwa kwa sababu ya uongozi wake mbovu.
 
Macho...
Naanza na hili.

Watu wengi wanapata shida ya kunifahamu.

Siku mbili zilizopita kuna mtu kaniita, "Mufti."

Leo wewe umeniita, "Ustaadh."

Natamani kuwa vyote hivyo laki Allah hakunijaalia.

Nimebakia na kutamani kuwa hivyo.

Huwa nataadharisha mapema kila nionapo makosa haya ili yule atakae mjadala na mimi angalau kwa uchache anifahamu.
 
Najua wewe hushindwi kwa kugeuza geuza maneno kama unavyogeuza geuza ID. Kule kwenye jukwaa la siasa nimeona umefungua tena thread jioni hii ukimkejeli Mbowe na Chadema! Kipindi cha Magufuli ulikuwa umepotea kabisa lakini sasa dini yako imeingia na wewe full umerudi kuendeleza udini wako. Sitasahau ile siku ya Jumapili nilivyokukamata kama panya buku uliposahau ukajibu kwa kutumia ile ID yako nyingine ya jukwaa la siasa. Ni roho za udini zinahungaisha tu lakini Tanzania atawale mkristo au mwislam maisha ni yale yale na hakuna kinachobadilika. Lakini watu wenye roho zinazoongozwa na udini kama wewe unajisikia ahueni anapotawala muislam kumbe ni illusion tu na hakuna uhalisia.
 
Tuko katika jina ulinonipa la ''Ustaadh,'' nikakuambia kuwa mimi si Ustaadh.

Umekuja na hili la ID na unasema nimemkejeli kiongozi mmoja wa siasa.

Umesema nilipotea hapa barzani katika kipindi fulani nk. nk.
Umekuja na lugha ambayo kwa kweli haipendezi kwa kunimithilisha mimi kama ''Panya Buku.''

Nakuomba kitu kimoja unifanyie kama ihsani kwangu.
Hebu weka hapa hizo ''link'' (kwa kurahisisha) ili nione hizo ID unazodai kuwa ni zangu.

Ningependa kukufahamisha kitu kimoja.

Mimi toka siku ya kwanza asubuhi nimeingia JF kwa jina langu halisi na sijapatapo hata siku moja kutumia ID ila hii ninayotumia.

Mimi sina sababu ya kujificha kwani siku zote nimesimama na kauli yangu nikieleza yale niyajuayo bila hofu.

Hili wewe huwezi kulijua ila uwe unanijua na umepata kunisoma.

Nina staili ya uandishi pekee sana na hata kama sitaweka jina langu wasomaji wataona sahihi yangu katika ''post'' yangu yoyote ile na watajua huyu si mwengine ila ni Mohamed Said.

Hilo la dini In Shaa Allah nitalizungumza baada ya kupata majibu yako.
 
Kuna ile siku ya jumapili watu walikuwa wanalumbana na wewe na ukakosoea ukajibu kwa ID ya hiyo nyingine. Tulipouliza kulikoni ukafuta ile post haraka. Ile ID ya Ritz! Kama siyo wewe basi ni mtu wako wa karibu sana na hiyo siku mlikuwa mnatumia device moja kuchangia! Kwa hiyo huyo Ritz kama siyo wewe basi ni mtu unayemjua fika. Na ana milengo kama yako kabisa, milengo ya udini na kulalamikia mfumo kristo. Hili nasema nikiwa na uhakika nalo. Kama siyo wewe basi ni hao vijana wako wa karibu kabisa.
 
Kuna ile siku ya jumapili watu walikuwa wanalumbana na wewe na ukakosoea ukajibu kwa ID ya hiyo nyingine. Tulipouliza kulikoni ukafuta ile post haraka. Ile ID ya Ritz! Kama siyo wewe basi ni mtu wako wa karibu sana na hiyo siku mlikuwa mnatumia device moja kuchangia! Kwa hiyo huyo Ritz kama siyo wewe basi ni mtu unayemjua fika. Na ana milengo kama yako kabisa, milengo ya udini na kulalamikia mfumo kristo. Hili nasema nikiwa na uhakika nalo. Kama siyo wewe basi ni h nao vijana wako wa karibu kabisa.
Macho,
Nitashukuru sana kama utanipatia ''link,'' ambazo nimekuomba ili nami nijue tunachojadili katika hizo ID unazosema ni zangu.

Lakini sasa unasema kuwa hizo ID kama si zangu ni za mtu ninayemfahamu fika.

Umebadili yale uliyosema kuwa ni zangu na kuwa huenda si zangu ila za mtu ninayemjua.

Unasema nina vijana wangu na ni wa karibu sana na mimi.

Mimi siwezi kuwa na vijana wangu.

Kwa nguvu gani nilizonazo mimi hadi niweze kuwa na watu?
Haya ni ya watu wa siasa si mtu kama mimi ninayeishi kwa kusukuma ''mouse.''

Ninachokifahamu kwa uhakika ni kuwa nina wasomaji wengi wanaopenda kusoma michango yangu.

Hili nina hakika nalo na naamini hata wewe unalijua.

Kama nilivyokwisha kusema ni kuwa hilo la dini nitalizungumza baada ya kupata majibu ya ''link,'' na ID kutoka kwako.
 
Sijabadili ila nimefafanua. Nimesema hivi: Jumapili moja wewe Mohamed Said ulianzisha thread (sikumbuki hasa ilikuwa ya nini). Kama ilivyo kawaida wachangiaji wakaanza kutiririka na wewe ukawa unajibizana nao. Baada ya muda yale majibizano yako yakawa yanaandikwa na member anayejiita Ritz. Yaani majibu ni yako lakini ID inayojibu ni ya Ritz. Baadhi ya members tuliposhangaa na kuuliza mbona ghafla tunajibizana na Ritz na siyo Mohamed tena, yale majibizano yakafutwa. Hii ina maana kuwa device ulikuwa unaitumia wewe kulikuwa na ID mbili ziko active. Moja yako na nyingine ya huyo anayejiita Ritz. Sasa kwa sababu ID yako ndiyo ilikosea, moja kwa moja wewe ndiye unawajibika kutoa maelezo kwani mkamatwa na ngozi ndiye mwizi. Kwa kutumia kanuni hiyo, nita-assume kuwa ID ya Ritz ni yako. Vinginevyo wewe utuambie ilikuwaje muingiliano huu ukatokea? Je kulikuwa na mtu gani yuko karibu anayetumia hiyo ID? Katu huwezi kukwepa kuwajibika. Ni kama bunduki yako ikitumiwa kuuwa mtu, wewe mwenye silaha ndiye utawajibika kujibu otherwise useme ni ilikuwa kwenye umiliki wa nani wakati wa tukio. Na kitu kingine ni kuwa huyo Ritz haiba yake kwenye mambo ya udini udini ni kama yako kabisa. Muda wote yeye anazungumzia hayo wewe unayopenda kuandika. Kulikoni?
Kuhusu link ya hiyo thread ni hii hapa, japo najua unauliza kimkakati tu.
CHADEMA Dodoma: Mbowe asipoachiwa, tutaitisha maandamano bila kikomo
 
Ahsante kwa kunipatia hiyo link.

Hapana mimi sijapata kuandika kuhusu CHADEMA.

Hayo si katika ujuzi wangu.

Mimi zaidi naandika katika historia ya Tanzania.

Unaweza kunifatilia kwa kipindi chote cha uandishi wangu takriban miaka 20 nyuma.

Ingia hapa:

Mjadala huu haujapata kutokea JF na umeweka rekodi ambayo hadi sasa haijavunjwa.

Angalia muda wake uliodumu na idadi ya wachangiaji.

Kitabu nilichokuwa nimeandika na kuchapwa mwaka wa 1998 kikauzwa kwa kiasi mimi nilishangaa.

Usifanye haraka soma taratibu utanifahamu na utajua kuwa mimi si mtu wa hivyo unavyonidhania.

Mimi si "Mufti" wala "Ustadh."

Tukimaliza hili In Shaa Allah nitazungumza hicho unachoita, "udini udini."
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom