Mzee Mwinyi: Magufuli Simba wa kazi

Umewahi kujenga??!!!
Unajua thamani ya ardhi ya maeneo zilipo??!!
Dili ya watu wachache ndio iliyumbisha serikali kiasi kile??!!

Kama kuna hoja nyingine iwekwe hii ni ngumu mno kueleweka kwa sasa. . . . . . . .

Kipi kilikua bora? Kuangalia thamani ya ardhi,!? Au kuangalia wizi na ufisadi unaofanywa na watendaji wa idara za serikali ktk ukarabati? Sawa ardhi unasema sehemu yenye thamani ndio iwe sbbu ya kuitia hasara serikali..? No way nyumba za serikali kwa viongozi ziwe nje ya Mji ili mji utanuke atakaye akakae asie taka hiyo ni issue nyingine.
 
Hata kama ni gamba magufuri yupo vizuri. Hakuna waziri yyote ki utendaji utamfananisha na magufuri,hata kama mnasema amejenga bara bara hazina kiwango sawa wengine wanashindwa hata kutengeneza madawati watoto wakalie vti miti tunayo,korosho zinaoza ktk maghara,mahindi vile vile kutafuta soko nje tatizo.
 
..mimi hata simuelewi Magufuli alikuwa na maana gani kumuita Mkapa ktk shughuli hiyo.

..mwana-ccm anayejitambua, na anayejiheshimu kimaadili, hawezi kujiweka karibu na Raisi Mkapa.

..Mkapa anahusika na kuiba mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira. Sasa mimi nilitegemea Magufulia atajiweka mbali kabisa na Mkapa, lakini yeye ndiyo ameona ni mtu wa mfano kumuita ktk hiyo shughuli ya wakandarasi wazalendo.

cc Mchambuzi, Ritz, ZeMarcopolo, Mkandara, Mahebe, Nguruvi3, VUTA-NKUVUTE

Mkuu JokaKuu,Magufuli ni teamMkapa tangu 1995

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Hujitambui wewe taahira, Nyumba za Serikali zenye thamani ya trillions zilikwapuliwa na mafisadi ndani ya Serikali akiwemo Mkapa na Magufuli kama hujui kaulize Lumumba kama watakuwa tayari kukwambia hili.

Huu uongo wako kamwambie mshumbushi ndiyo mmezoea kudanganyana.
 
Mzee Mkapa nilimwona akialikwa na World Bank kama mgeni rasmi "Tanzania Economic Update" naona duniani anakubalika kiasi kikubwa!

..asante sana.

..je mwaliko huo wa Mkapa huko World Bank, umekufanya wewe uamini kwamba hakuvunja sheria na kutumia madaraka yake vibaya ktk kujimilikisha mgodi wa Kiwira?

..World Bank wataendelea kumualika as long as serikali ya Tz, na sisi wenyewe wa-Tz tunamvumilia.

..tunapaswa kushughulika na mafisadi na usitegemee world bank kuja kutusaidia kuwakamata na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria.

cc Columnist
 
Last edited by a moderator:
Hata kama ni gamba magufuri yupo vizuri. Hakuna waziri yyote ki utendaji utamfananisha na magufuri,hata kama mnasema amejenga bara bara hazina kiwango sawa wengine wanashindwa hata kutengeneza madawati watoto wakalie vti miti tunayo,korosho zinaoza ktk maghara,mahindi vile vile kutafuta soko nje tatizo.

..inawezekana pia ni kati ya mawaziri waliotutia hasara kubwa kuliko wenzake.

..hivi umewahi kujiuliza nyumba na viwanja vile vingeuzwa kwa bei ya soko serikali ingepata kiasi gani?
 
Tungeweza kusema kwenye nchi ya vipofu, mwenye chongo ndiye mfalme ingawa bado sivyo. Sijaelewa kisa cha Magufuli kuonekana mtendaji wa maana kiasi hicho katika serikali ya CCM. Au ni kwa vile amejikita katika kukariri na kuongea kwa hamasa kuhusu kilomita na jiografia za barabara? Hakuna hata anayehangaika kuwauliza wataalamu halisi kuhusu vigezo muhimu vya barabara ili kujiridhisha kuwa tunapata "value for money"? Kwa vile barabara zinatengewa fedha nyingi hasa za wafadhili na Waziri ni bingwa wa kukariri na kusema sana basi ameshakuwa "mtendaji makini"?

Tumeanzisha utamaduni wa ajabu sana wa kumtambua waziri "mchapa kazi" kama yule anayebeba makabrasha ya ofisini na kuyaleta hadharani kuelezea "mipango inayotekelezwa" mbele ya TV. Akisimamisha kazi makandarasi anakuja kututangazia kwenye TV na nakala za mikataba. Kila kitu mbele ya TV. Kwa watu wenye shule wanaojua undani wa kazi za kitaalamu wanafahamu kuwa masuala hayo hayako kirahisirahisi kama anavyofanya huyo "mchapa kazi". The devil is in the detail!

Kwa utamaduni huo ndio maana wanasiasa wanaosimamia miundombinu hawana utashi wa kuhimiza kazi muhimu kama kuimarisha mifumo ya kudhibiti maji ya dhoruba (storm drainage systems) kwa sababu mifumo hiyo iko chini ya ardhi; huwezi kuwaonyesha wananchi wenye kushabikia ving'aavyo usoni hata kama ni kwa muda tu kabla havijabomoka. Miundombinu yetu yote haiwekewi mifumo thabiti ya kinga kwa vile mifumo hiyo inahitaji pesa na kazi kubwa na haionekani "usoni" na "wapiga kura". Kwenye miundombinu ya umeme shida hiyo hiyo, kwenye barabara, reli, n.k. Halafu anayewatangazia "kilometa kadhaa" ndiye mchapa kazi. Kazi ya ujenzi si ya majukwaa ya kisiasa. Tafuteni undani wa kinachoendelea; sio kuweka ushabiki usio na maana.
 
Kipi kilikua bora? Kuangalia thamani ya ardhi,!? Au kuangalia wizi na ufisadi unaofanywa na watendaji wa idara za serikali ktk ukarabati? Sawa ardhi unasema sehemu yenye thamani ndio iwe sbbu ya kuitia hasara serikali..? No way nyumba za serikali kwa viongozi ziwe nje ya Mji ili mji utanuke atakaye akakae asie taka hiyo ni issue nyingine.

We umeuza zako ngapi sababu ukarabati ni ghali kuliko kujenga mpya??!!!
 
akili kama mavi vile. hivi unaweza linganisha oyster bay na huko sijui boko bunju na upuuzi mwengine?
hizo nyumba sio ishu, tatizo ni maeneo kwa ajili ya viongozi na watumishi wengine wa umma. chukulia mfano rahisi tu. aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi alipewa nyumba ya mkuu wakituo mita 10 kutoka kituoni. mwenye nyumba amestaafu au kuhamishwa kikazi, na nyumba imepangishwa kwa raia wa kawaida na mkuu wa kituo analazimika kwenda kupanga mtaani.
hivi huko shule mlienda kufanya nini?

Kwa hili la nyumba sidhani kama kuna hoja hapo mwenyewe alikwisha litolea maelezo kuwa gharama za kuzikarabati zile nyumba lillikuwa ni dili la wapiga hela.. kila akiingia kiongozi mpya. Na hizo gharama zinakuwa mara nne ya ujenzi wa nyumba mpya.! Aliona zijengwe nyingine nje ya mji. Boko muulizeni zimejengwa ama bado? Huenda tatizo hao viongozi hawataki kaa huko wanataka masaki na oysterby tu. Big up Jembe John Pombe
Magufuri.
 
Nilishasema..kama CCM wana mpango wa kuendelea kukaa madarakani...basi wamsimamishe Dr Magufuli.
Huyo ndo mwana CCM pekee ambaye hata akisimama kwenye jimbo la CHADEMA, anakubalika sana..
CCM wakitaka kuumiza kichwa upinzani wamsimamishe huyo mkuu, vingunevyo...UKAWA watachukua nchi

naunga mkono sana
 
Huyu Jamaa hafai kuwa hata Diwani baada ya uchaguzi wa 2015 mbinafsi, muonevu, mla rushwa mkubwa, muongo, mshirikina, Hana uzalendo. Hapendi kuona watanzania wanaendelea alikuwa anagawa Kazi kwa wachina na kutengeneza barabara mbovu akidhani bado watanzania ni wajinga wa miaka ya 80 ya kuchagua Mwinyi na Giza!! Ana mental disorder na hana busara ya kuweza kumudu Kazi za Urais. Hizi damu za wakina Nkurunzinza hatutazipa nafasi over our dead bodies no way Rais akawa kichaa. CCM Ina watu wengi wenye busara na uweledi Kazi ya Uraisi sio ya kumjaribu kila mtu, hizo ela alizo iba kwa ajili ya kampeni zitaliwa bure lakini Urais atausikia tu hata Ubunge safari hii hapati.
 
editorial-cartoon-may19-2015.jpg

Na bara bara zake zinazotitia wakati wa manyunyu...
 
Huyu Jamaa hafai kuwa hata Diwani baada ya uchaguzi wa 2015 mbinafsi, muonevu, mla rushwa mkubwa, muongo, mshirikina, Hana uzalendo. Hapendi kuona watanzania wanaendelea alikuwa anagawa Kazi kwa wachina na kutengeneza barabara mbovu akidhani bado watanzania ni wajinga wa miaka ya 80 ya kuchagua Mwinyi na Giza!! Ana mental disorder na hana busara ya kuweza kumudu Kazi za Urais. Hizi damu za wakina Nkurunzinza hatutazipa nafasi over our dead bodies no way Rais akawa kichaa. CCM Ina watu wengi wenye busara na uweledi Kazi ya Uraisi sio ya kumjaribu kila mtu, hizo ela alizo iba kwa ajili ya kampeni zitaliwa bure lakini Urais atausikia tu hata Ubunge safari hii hapati.

Mkuu hasira zote za nini? Aliwahi kukukwaza wewe binafsi?
 
Huyu naye ni fisadi aliyekwapua nyumba za Serikali. Akianikwa huyu madudu aliyoyafanya katika awamu ya tatu na hii Ikulu ataisikia kwenye bomba. Hana sifa hata chembe.

Nyumba za Serikali yalikuwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri
 
Huyu Jamaa hafai kuwa hata Diwani baada ya uchaguzi wa 2015 mbinafsi, muonevu, mla rushwa mkubwa, muongo, mshirikina, Hana uzalendo. Hapendi kuona watanzania wanaendelea alikuwa anagawa Kazi kwa wachina na kutengeneza barabara mbovu akidhani bado watanzania ni wajinga wa miaka ya 80 ya kuchagua Mwinyi na Giza!! Ana mental disorder na hana busara ya kuweza kumudu Kazi za Urais. Hizi damu za wakina Nkurunzinza hatutazipa nafasi over our dead bodies no way Rais akawa kichaa. CCM Ina watu wengi wenye busara na uweledi Kazi ya Uraisi sio ya kumjaribu kila mtu, hizo ela alizo iba kwa ajili ya kampeni zitaliwa bure lakini Urais atausikia tu hata Ubunge safari hii hapati.

Chuki binafsi hizo wewe. Mtu mwenye track record ya miaka 20 ya utendaji wenye weledi ndani ya serikali mbili za Mkapa na Kikwete bila kashfa yoyote unamwita Mwinyi? Na YES, this country needs a kichaa kama Magufuli ili tuendelee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom