Mzee Mwinyi katika hili la kuongeza muda wa Asante kwa Rais Magufuli hapana, tunakukatalia kwa nguvu zetu zote

Hapa hatuzungumzii juu ya raisi ni nani!!---- Suala lililopo mezani ni; je wakati unaruhusu kubadili katiba ili kukudhi haja ya wakati??-- ni hapo Mzee Mwinyi ndipo alipokuwa anazungumzia kumuhusu Magufuli kuwa amefanya mambo makubwa kiasi kwamba inastahili katiba ibadilishwe ili aendelee kufanya makubwa zaidi. Hayo yalikuwa ni maoni na ushauri wake kama Raisi mstaafu na kama raia, sasa dhambi yake ipo wapi hapo??--- mbona hata wewe unapinga katiba kubadilishwa je na yeye akulaumu kwa kuifanya katiba kuwa ni sheria ya Mungu???, ni sheria ya Mungu tu ndiyo isiyoweza kubadilishwa na mwanadamu.
Sheria ya mwanadamu inabadilishwa na mwanadamu kukidhi haja ya wakati.

Itakuwa.ni ujinga kushikilia sheria zilizopitwa na wakati ilhali zinaweza kurekebishwa kukidhi haja ya wakati huo.

Mimi siungi mkono Magufuli kuongeza muda lakini sikubali Mwinyi alaumiwe kisa kutoa maoni yake.
Kafanya makubwa kwake na familia yake kwa kuipa maisha na sio kwetu tunaosemeshwa namba.
Hayo makubwa achilia propaganda yamesaidia nini kuboresha maisha ya walipa Kodi zaidi ya njaa na umasikini nchini baada ya kuuwa uchumi.
 
Akili kbwa hii, itakuwa kama Baba yake kwanza Zenj kisha anaingia Bara

Mzee amesha piga hesabu, magu akijiongeza hata mitano mingine, inatasha mwanae kumaliza awamu zake Zanzibar aje achukue na bara. Ni malengo tu
 
Katiba ni mali ya wananchi, pamoja na ukomo wanaweza kubadili kipengele kwa manufaa ya umma. Alichoanzisha JPM kitunzwe kwa nguvu zote.
 
Hapa hatuzungumzii juu ya raisi ni nani!!---- Suala lililopo mezani ni; je wakati unaruhusu kubadili katiba ili kukudhi haja ya wakati??-- ni hapo Mzee Mwinyi ndipo alipokuwa anazungumzia kumuhusu Magufuli kuwa amefanya mambo makubwa kiasi kwamba inastahili katiba ibadilishwe ili aendelee kufanya makubwa zaidi. Hayo yalikuwa ni maoni na ushauri wake kama Raisi mstaafu na kama raia, sasa dhambi yake ipo wapi hapo??--- mbona hata wewe unapinga katiba kubadilishwa je na yeye akulaumu kwa kuifanya katiba kuwa ni sheria ya Mungu???, ni sheria ya Mungu tu ndiyo isiyoweza kubadilishwa na mwanadamu.
Sheria ya mwanadamu inabadilishwa na mwanadamu kukidhi haja ya wakati.

Itakuwa.ni ujinga kushikilia sheria zilizopitwa na wakati ilhali zinaweza kurekebishwa kukidhi haja ya wakati huo.

Mimi siungi mkono Magufuli kuongeza muda lakini sikubali Mwinyi alaumiwe kisa kutoa maoni yake.

Mzee anataka mitano mingine ya "asante", Tangu lini urais ukatolewa kwa shukrani.
 
Katiba sio msaafu ,acha mambo ya ajabu we dogo,tutaibadilisha kulingana na mahitaji
 
Hii nchi kwa sasa, vijana shida....wazee shida. Kiukweli unafiki umeshika hatamu.
 
Naunga mkono JPM kuongezewa angalau miaka mitano.Akitawala miaka kumi na tano atatufikisha.
 
Mimi pia awali nilifikiria sana umuhimu wa kubadilisha katiba angalau kwa mazingira maalum ya Rais Magufuri kwa kazi ya kipekee na nzito aliyoifanya kwa muda mfupi na matokeo makubwa kuonekana. Maeneo yaliyonishawishi zaidi kuwa Rais anastahili kuongezwa angalau miaka 5 au 10 baada ya muda wake ni kupiga vita rushwa, ubadhirifu, na ufisadi ambao nchi nyingi za Afrika zimeshindwa. Pili uwezo wake wa uongozi na maono, tatu utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa kasi kubwa na kwa maslahi ya taifa na mipango kadhaa ya kiuchumi ambayo ni ya kihistoria mf Stiglers umeme, Kuhamia Dodoma , Ujenzi wa fly overs, REA. Na hatimaye kuingiza uchumi wa kati.Pamoja na changamoto alizopata za utekelezaji amesukumwa mno na utashi binafsi wa kisiasa. Siyo kitu rahisi kupata Rais mwingine wa aina hii tutakapokosea huko mbele baada ya muda wake kuisha itakuja kuwa majuto ni mjukuu. Pengine hata Mwalimu Nyerere angekuwa hai angeshauri aongezwe muda Rais wa sasa -who knows -kwa vile yule mzee alikuwa Pragmatist na mwenye maono ya mbali.Hivyo kama nchi kadhaa zilivyofanya mf China, Urusi kwa maslahi ya nchi zao zimebadilisha katiba zao na kuongeza muda wa maraisi sisi ni nani. Ni kweli Katiba siyo msahafu au biblia kwa hili la eneo la muda wa kuongoza linaweza kufanyika kwa KURA YA MAONI ya wananchi ambao ndiyo wenye nchi kuamua na kwa sababu maalum ya kimaslahi ya taifa. Iwapo hoja hii itashindikana basi maandalizi makubwa ya kuweka succession plan yafanywe kwa kumtambua mtu makini atayeingia viatu vya magufuri au katiba isukwe upya kulinda mafanikio yaliyopatikana na mifumo thabiti iwekwe kipindi hiki kutupeleka mbele.Nchi kama Marekani imeweza kuendelea na mfumo wa vipindi vya miaka miwili kutokana na mifumo yake imara na sera za kitaifa ambazo hazibadilishwi kwa upepo wa Rais. Hii inaweza kuwa option 2. Tunashauri Usalama wa Taifa waanze kazi ya kufanya utafiti na upekuzi maalum na wa kina hali itakavyokuwa baada ya Magufuri na nani mzalendo atatuvusha huko mbelena bila kusahau optios mbalimbali.Tukishindwa kuwa na Open program basi nakubaliana na wanaosema aongezwe muda huyu aliyepo baada ya miaka yake 10 Uongozi wa nchi haujaribiwi.
 
Umeandika gazeti dah, alie mponda kiatu yule mzee alikuwa na akili sana.

Kila mtu ashinde mechi zake kama ss wana simba, wengi wanawazia tu nafasi zao atakae kuja atawacha wawe walipo saivi,.

Njaa mbaya sana, Jiwe kafanya mazuri, ila yupo mmwingine atafanya mazuri zaidi,
 
Hofu yenu ni nini?, Mzee Mwinyi kuongea ni jambo moja lakini Bw John kimoyomoyo naye anasema "za kuambiwa ongeza na za kwako" muwe na imani.
 
Bahati nzuri hata Mh Rais kashasisitiza mara nyingi kuwa ataheshimu katiba
Labda hofu ya Watu ni vile ahadi ya kutokula inatolewa kabla ya kufika kwenye sherehe, tukikaribia na kusikia ile harufu ya pilau bado Mwenzetu atasema hali au atasema "nitaonja"?.
 
Mzee wetu mzee Mwinyi, Shikamoo

Mimi ni mtanzania, kwa umri niseme labda ni mjukuu wako, ni Mtanzania, naipenda nchi yangu na ningependa iwe na mustakbali mwema.

Mzee wetu nimekusikia mara kadhaa ukieleza hamu yako ya kumuona rais aliyeko madarakani akiongezewa muda wa kutawala kinyume cha katiba ya sasa inavyotaka.

Mzee wetu, mimi kama mtu mzalendo, mwenye uchungu na nchi hii, nimeitafakari kauli yako, hapo mwanzo nilitaka niiache kama ilivyo lakini nikaona nitakuwa sijaitendea haki nchi yangu kama nitaiacha hilo suala lipite hivihivi bila kulizungumzia, hususan baada ya kuona kuwa hilo suala linaweza kuwa sumu ya amani ya nchi yetu na mustakbali wake, Mheshimiwa rais mstaafu baba yetu mzee Mwinyi hebu tusemezane katika haya yafuatayo kuhusu suala hilo:

1. Je ni nini lengo la kuweka ukomo wa utawala katika katiba?

Mzee Mwinyi bila shaka ulikuwepo wakati Baba yetu wa Taifa alivyoongoza Taifa letu katika mchakato wa mabadiriko ya katiba yaliyohakikisha kuwa tunaweka ukomo wa madaraka katika katiba mwaka 1984, Kwa hakika Baada ya vuguvugu la wananchi katika Afrika kutaka kubadiri serikali zao kwa njia amani na iliposhindikana kujaribu kutumia nguvu za kijeshi, busara ilimuingia raisi wetu wa wakati huo baba wa Taifa letu mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa ipo haja na ulazima wa kuweka Transition ya amani ya madaraka kutoka generation moja kwenda nyingine. Na hii ilifuatia majaribio kadhaa ya mapinduzi dhidi yake.

Mzee wetu mzee Mwinyi unataka kuturudisha kwenye utaratibu wa utawala wa maisha?. Je mzee wetu unadhani tukimruhusu rais wa sasa aendelee kutawala tutaweza kweli kuwazuia na marais wajao kuendelea kutawala kwa kisingizio kuwa wanafanya kazi vizuri?, Je mzee wetu unataka kuwaandalia mazingira Watanzania utaratibu wa kufanya machafuko ili kumtoa rais ambaye watadhani hawafai, raisi ambaye atakuwa anatawala kwa katiba inayomruhusu kutawala bila ukomo?

Mzee wetu usidhani ukibadili katiba kwa ajili ya Magufuli, hiyo katiba itaishia kwa Magufuli tu, hata Magufuli baada ya kutawala tani yake akaamua kubadili katiba tena na kurudisha utaratibu wa zamani, atakayemfuata naye anaweza kuibadili tena naye akatawala tani yake!. Mzee wetu hayo ndiyo unayoyataka?

2. Mzee wetu, kumbuka Msisitizo wa Baba wa Taida kukutaka usibadili ukomo wa kutawala

Mzee wetu, mwaka 1999 pale uwanja wa Taifa kwenye msiba wa mwalimu, ulikuwa miongoni mwa watu waliopewa nafasi ya kumzungumzia Mwalimu, ulieleza mambo mengi, ulieleza jinsi alivyokuwa Mlima wa fikra na uongozi n. k na uliahidi kulinda yale mazuri yote aliyotuachia. Sasa mzee wetu mzee Mwinyi, hata hili la ukomo wa madaraka nalo unaliwekea question mark?. bado una chembe ya shaka juu ya umuhimu wake?

Mzee wetu mzee Mwinyi labda nikukumbushe tu namna mwalimu alivyotueleza wazi Watanzania kuwa wakati wa utawala wako, walikuwepo watu na harakati za kukutaka wewe ubadili katiba ili uendelee kutawala baada ya miaka kumi, Mwalimu alielezea jinsi alivyokuwa concerned na suala hilo na akatueleza kuwa jinsi wewe binafsi ulivyomhakikishia kuwa huna nia hiyo.

Sasa mzee wetu mzee Mwinyi, unadhani Mwalimu hakupenda usiendelee kutawala kwa sababu alidhani wewe hufai au alidhani kuwa wazo hilo siyo jema kwa mustakbali mpana wa nchi yetu?. Je Mzee wetu mzee Mwinyi, mbona basi na wewe unakuwa kama wale watu waliokuwa wanasukumasukuma mambo ili wewe uendelee kutawala kinyume cha ukomo wa vipindi kipindi cha utawala wako?.

Au mzee wetu mzee Mwinyi wakati ule ulikubaliana kishingo upande na mwalimu lakini wewe binafsi siyo muumini wa ukomo wa vipindi vya utawala?

3. Mzee wetu Mzee Mwinyi, Je una maslahi binafsi na utawala wa Magufuli?

Jana kwenye mkutano mkuu, Raisi Magufuli alituibia siri kuwa mwaka 2015 alikuwa yeye binafsi amempendekeza mwanao Hussein Mwinyi ili awe mgombea mwenza, Pia Mwanao Hussein Mwinyi amepata nafasi ya kuwa Mgombea wa CCM kwa tiketi ya Uraisi Zanzibar katika kipindi hiki ambapo Magufuli ni rais.

Sasa sisi tunajiuliza, hivi je mzee wetu unataka kulipa Shukrani kwa Magufuli kwa kumfanyia makubwa mwanao?, Je una maslahi binafsi yanayokusukuma kutaka Magufuli aendelee kuwa raisi, Je unamuandalia njia njema zaidi Mwanao kwa kutaka tuendelee na kile ambacho waswahili walisema kwenye methali "Zimwi likujualo"?

4. Mzee wetu, Mzee Mwinyi kumbuka hotuba ya baba wa Taifa kuhusu Nyufa zilizoikumba nchi yetu

Kabla ya uchaguzi wa mwaka 1995, baba yetu wa Taifa alizungumza nyufa mbalimbali ambazo zilianza kuikumba nchi yetu, na miongoni mwa mambo aliyoyasema ni suala la kutoheshimu katiba.

Mzee wetu mzee Mwinyi, mimi binafsi nilisikitishwa sana kusikia ukisema, Katiba tuiweke pembeni ili tumpe tena Rais wa Sasa miaka mitano kama Ahsante. Mzee wetu hata kama Rais Magufuli angeleta maendeleo ya namna gani, Je unataka tutoe ahsante kwa mtu aliyetimiza wajibu wake tuliomtuma afanye kupitia kuvunja katiba?. Mzee wetu mzee Mwinyi, wewe si uliapa kulinda katiba, Mwenzio naye si aliapa kulinda katiba, Sasa unamshawishi avunje katiba?

5. Mzee Mwinyi, Ushauri wako haujengi, ni mbaya na unatuma meseji mbaya kwa vizazi vijavyo

Mzee wetu mzee Mwinyi, wewe ni mtu mkubwa sana, wewe ni role model wa wengi, fahamu kwamba kauli zako zinawekwa kwenye rekodi na huenda zikawa rejea vizazi na vizazi hata miaka maelfu ijayo. Kauli za "huba" unazozitoa juu ya mtawala wa sasa hata kutaka katiba ipindishwe kwa ajili yake, wapo watu watakaokuja huko mbeleni watazitumia kama rejea ili kufanya hayahaya ambayo unatamani Taifa lifanye kwa ajili ya Magufuli, Watasema mbona miaka 50 iliyopita Rais wa awamu ya pili alitaka rais wa awamu ya tano naye aendelee kutawala?, basi kwa nini na sisi tusifanye?. Kwa kweli mzee wetu katika hili hauko sahihi kabisa, haujalitendea haki Taifa kabisa

Hitimisho
Ni dhahiri ushauri wa mzee wetu mzee Mwinyi ni ushauri mbaya kabisa kwa Taifa letu, ni ushauri usiozingatia hekima bora kabisa ya baba wa Taifa letu mwalimu Nyerere aliyeamua kuingiza ukomo wa utawala kwenye katiba, kitu ambacho leo hii tunajivunia Taifa letu kubadirishana uongozi kwa amani.

Mzee wetu Mzee Mwinyi akumbuke tu, Wakati mwalimu Nyerere anamuachia kijiti hapo mwaka 1985,Mwalimu alikuwa ni "kijana" kabisa wa miaka 63, pamoja na hali ngumu ya uchumi tuliyokuwa nayo wakati huo, Mwalimu alikuwa na uwezo wa kwenda kwenye uchaguzi na bado akashinda kwa kishindo, lakini aliona busara pana ni kung'atuka na kumuachia mtu mwingine kijiti.

Sasa swali la kujiuliza ni hili, kama Mwalimu asingeng'atuka mwaka 1985 yeye angekuwa rais?, Mkapa asingeheshimu mihula ya utawala Kikwete angekuwa rais?, Kikwete asingeheshimu katiba juu ya mihula ya Utawala Je Magufuli angekuwa rais?. Tunamuomba Mzee wetu alifikirie sana suala hili

Ama kuhusu Ahsante anayotaka tumpe Magufuli, Kama kuna ahsante yoyote ya kutoa kwa mtawala basi Watanzania wangetoa ahsante kwa mwalimu Nyerere kwa kuwaletea uhuru. Hakuna kitu kikubwa kilichofanywa katika nchi hii kuliko uhuru wetu. Lakini wananchi hawakuona eti wamfanye Mwalimu mfalme kisa katuletea uhuru.

Kama ni ahsante kwa sababu mtawala kaitendea jema familia, hata Mwalimu alikuwa na watoto pia akina madaraka Nyerere, Makongoro Nyerere, Rose Nyerere, lakini baba yetu wa Taifa hajawahi kuwa nice kwa mtawala teyote aliyekuja baadae ili watoto wake watendewe mema.

Mwisho kabisa nimpongeze katibu mkuu wa CCM ndugu, Bashiru Ally kwa kuzungumza wazi kupitia mahojiano na Tido Mhando kuwa suala la kubadili katiba ili kuongeza mihula ya utawala halimo katika ajenda ya CCM na si sera ya chama hicho na kwamba likiibuka CCM watalikataa. Mimi nasema hiyo ni busara kubwa sana

Pia nimshukuru rais Magufuli Mwenyewe ambaye yeye Mwenyewe kwenye mkutano mkuu alionyesha kutokubaliana na wazo hilo la mzee Mwinyi waziwazi, na ambaye mara kadhaa ameongea na kusema kuwa hana mpango huo

Mwisho kabisa ningependa Watanzania wote tulikatae wazo hilo la mzee Mwinyi, ni wazo baya, si jema kwa nchi yetu na halina mustakbali mwema kwetu na vizazi vyetu
Mwinyi amejiaibisha sana kwa kauli yake hii, amejionesha utupu wake.

Mkapa alishakataza kuongeza muda, Magufuli akishakataa, Mwinyi anaonekana anajipendekeza kwa mtu badala ya kuangalia katiba.

Kwani Tanzania imekosa viongozi mpaka imtegemee mtu mmoja?

Yani Mwinyi kasahau maneno ya Nyerere kwamba kwa kufuata katiba hakuna mtu atakayekaa urais zaidi ya miaka 10?

Mwinyi kaona kitu gani kitakachotufanya tuvunje katiba kwa kumtegemea mtu mmoja?

Na tukivunja hivyo, kipi kitatuzuia tusivunje tena na kuifanya nchi iwe ya kifalme?

Mkapa alionya kwenye kitabu chake kuhusu hizi yabari, Mwinyi kasoma hata dondoo tu?

Mkapa on presidential term-limits
 
Bahati nzuri hata Mh Rais kashasisitiza mara nyingi kuwa ataheshimu katiba
Labda hofu ya Watu ni vile ahadi ya kutokula inatolewa kabla ya kufika kwenye sherehe, tukikaribia na kusikia ile harufu ya pilau bado Mwenzetu atasema hali au atasema "nitaonja"?.
 
Mimi pia awali nilifikiria sana umuhimu wa kubadilisha katiba angalau kwa mazingira maalum ya Rais Magufuri kwa kazi ya kipekee na nzito aliyoifanya kwa muda mfupi na matokeo makubwa kuonekana. Maeneo yaliyonishawishi zaidi kuwa Rais anastahili kuongezwa angalau miaka 5 au 10 baada ya muda wake ni kupiga vita rushwa, ubadhirifu, na ufisadi ambao nchi nyingi za Afrika zimeshindwa. Pili uwezo wake wa uongozi na maono, tatu utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa kasi kubwa na kwa maslahi ya taifa na mipango kadhaa ya kiuchumi ambayo ni ya kihistoria mf Stiglers umeme, Kuhamia Dodoma , Ujenzi wa fly overs, REA. Na hatimaye kuingiza uchumi wa kati.Pamoja na changamoto alizopata za utekelezaji amesukumwa mno na utashi binafsi wa kisiasa. Siyo kitu rahisi kupata Rais mwingine wa aina hii tutakapokosea huko mbele baada ya muda wake kuisha itakuja kuwa majuto ni mjukuu. Pengine hata Mwalimu Nyerere angekuwa hai angeshauri aongezwe muda Rais wa sasa -who knows -kwa vile yule mzee alikuwa Pragmatist na mwenye maono ya mbali.Hivyo kama nchi kadhaa zilivyofanya mf China, Urusi kwa maslahi ya nchi zao zimebadilisha katiba zao na kuongeza muda wa maraisi sisi ni nani. Ni kweli Katiba siyo msahafu au biblia kwa hili la eneo la muda wa kuongoza linaweza kufanyika kwa KURA YA MAONI ya wananchi ambao ndiyo wenye nchi kuamua na kwa sababu maalum ya kimaslahi ya taifa. Iwapo hoja hii itashindikana basi maandalizi makubwa ya kuweka succession plan yafanywe kwa kumtambua mtu makini atayeingia viatu vya magufuri au katiba isukwe upya kulinda mafanikio yaliyopatikana na mifumo thabiti iwekwe kipindi hiki kutupeleka mbele.Nchi kama Marekani imeweza kuendelea na mfumo wa vipindi vya miaka miwili kutokana na mifumo yake imara na sera za kitaifa ambazo hazibadilishwi kwa upepo wa Rais. Hii inaweza kuwa option 2. Tunashauri Usalama wa Taifa waanze kazi ya kufanya utafiti na upekuzi maalum na wa kina hali itakavyokuwa baada ya Magufuri na nani mzalendo atatuvusha huko mbelena bila kusahau optios mbalimbali.Tukishindwa kuwa na Open program basi nakubaliana na wanaosema aongezwe muda huyu aliyepo baada ya miaka yake 10 Uongozi wa nchi haujaribiwi.
Kama kafanya mazuri, huenda akaja atakayefanya mazuri zaidi.

Kama akina Kikwete wasingeheshimu katiba yeye angepatikana?

Na yeye aheshimu katiba ili tupate waliobora zaidi yake mapema!

Mwalimu alikuwa pragmatist, lakini hakuwa pragmatist kuruhusu mambo ya kipumbavu

Katiba huwa haitungwi kwa ajili ya mtu mmoja huwa inatungwa kwa ajili ya all weather ili siku akija rais mbovu isaidie kulinusuru Taifa dhidi ya ubovu wake na akija mzuri basi imsaidie kufanya uzuri wake to a maximum

Ukibadili katiba halafu akafa akaja mwingine mbovu, muuaji, mwizi, mshenzi, muuza nchi unataka naye atawale kwa katiba inayomruhusu kutawala mamihula yote hayo bila kikomo?

Ni ufinyu wa mawazo kudhani kama katiba ikibadirishwa basi huyo atakayekuja baada ya Magufuli hatoitumia katiba hiyohiyo au naye hatataka aibadili ili naye atawale mimiaka mingi tu
 
Back
Top Bottom