Mzee Mwinyi awachomekea kizenji!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ametoa maneno mazito na ya hekima, ambayo kwa tamaduni nyingi za Kiafrika, hutolewa na wazee waliokula chumvi nyingi.

Mwinyi, ni mmoja wa viongozi adhimu wanaoweza kuwekwa katika daraja la juu miongoni mwa wanasiasa ambao hujipambanua kwa kutopenda makuu au hata kujikweza, tangu zama akiwa madarakani.

Watanzania walio wengi wanamkumbuka mzee huyo kwa maneno ya busara aliyoyatoa wakati alipokuwa akijilinganisha na mtangulizi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Huku akijua kwamba, yeye ndiye aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mwinyi aliwaeleza Watanzania kwamba, yeye alikuwa ni mtu ambaye asingeweza kulinganishwa na Nyerere na akasema kama kungekuwa na kipimo, basi yeye (Mwinyi) angekuwa ni kichuguu na Mwalimu ni Mlima Kilimanjaro.

Kwa hakika taifa linaweza likapata shida sana kupata aina ya kiongozi mkuu wa nchi, ambaye alipokuwa madarakani, alikuwa mtu mnyenyekevu, msikivu, mkarimu, mvumilivu na mcha Mungu wa aina ya mzee wetu Mwinyi.

Miaka takriban 12 tangu aondoke madarakani, Watanzania sasa wanaweza wakajithibitishia kwa kuyaangalia maisha yake na pengine hata kumuomba radhi kiongozi huyo aliyetudhihirishia kuwa alikuwa miongoni mwa viongozi wachache waadilifu wa kweli kweli waliopata kulitumikia taifa hili.

Tumelazimika kumtaja na kuelezea kwa sehemu tu wasifu wa kiongozi wetu huyo mstaafu, kutokana na ujumbe mzito wa maneno aliyotupa Watanzania siku mbili zilizopita.

Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa gazeti la Changamoto, aliwataka waandishi wa habari kutimiza wajibu wao kwa kuendelea kuwakosoa viongozi wao.

Kiongozi huyo alisema kuwa, waandishi wa habari wana dhima ya kuikosoa serikali na viongozi wake kwa sababu imejengeka tabia ya hatari miongoni mwa viongozi hao, ya kujisahau katika kutimiza wajibu wao.

Mwinyi maarufu kwa jina la Mzee Ruksa, alisema kuwa magazeti, ni moja ya njia madhubuti zinazoweza kutumika kukuza demokrasia nchini na sehemu nyingine duniani.

Alisema kuwa, watu wengi hupata habari za mambo yanayotokea kupitia magazeti, hivyo magazeti hayo na waandishi wake wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa, wanawapatia habari wananchi wenye kiu ya ufahamu.

Uzito wa maneno hayo ya rais wetu mstaafu, unaonekana hivi sasa, kutokana na ukweli kwamba, baadhi ya viongozi serikalini wamekuwa wepesi sana kuponda baadhi ya mambo yanayoandikwa magazetini dhidi yao.

Hulka hiyo mbaya ya baadhi ya viongozi, imefikia hatua ya kuwafanya baadhi ya waandishi wa habari wanaoonekana kuwa mstari wa mbele kukosoa waonekane kuwa ni wasaliti, wachimvi, wazushi na watu wasiolitakia mema taifa hili.

Hivi sasa ni dhahiri kwamba, wakati viongozi wa aina hiyo wakitamka kwa maneno tu kuwa tayari kukosolewa, baadhi ya maamuzi yao yamekuwa yakithibitisha kuwa, kile wanachokitamka sicho wanachokiamini kwa dhati na kukitekeleza.

Tunaamini kwamba, maneno mazito aliyotoa kiongozi huyo mstaafu, yanaweza yakawa ni somo zuri kwa baadhi ya viongozi wasio wavumilivu na wasiopenda kuguswa, ilhali wakijua kuwa madaraka makubwa waliyonayo ni dhamana nzito inayoweza kuathiri maisha ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Kwa sababu hiyo basi, tunaamini pia kwamba, maneno hayo ya mzee wetu yanapaswa kuwa changamoto si kwa viongozi wetu tu, bali hata kwetu wanahabari, ya kuutambua, kuuheshimu na kuuendeleza wajibu wetu wa msingi wa kukosoa, inapopaswa katika misingi ya ukweli pasipo kumhofia yeyote.
 
Mwinyi recalls the days of a ’clean’ civil service

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

FORMER president Ali Hassan Mwinyi yesterday declared that he has never taken a bribe from anyone in his life.

’’Actually, corruption was something that was totally unheard of in the civil service in the 1960s,’’ said Mwinyi, who served two full, five-year terms at State House from 1985 to 1995.

The 82-year-old retired president was speaking in a live television interview broadcast yesterday by the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) as part of a special programme in commemoration of the eighth anniversary of the death of founder president and Father of the Nation, Mwalimu Julius Nyerere.

Recalling the early years of the Nyerere administration after independence in 1961, Mwinyi said corruption was then not such a big problem ’’because civil servants were satisfied with what they were being paid.’’

He said although his first salary as a civil servant was no more than 90/- (ninety shillings only), it was enough to enable him live comfortably and provide for his family.

’’Greed is the overriding cause of corruption today,’’ remarked Mwinyi, acknowledging that some civil servants have chosen to ignore ethical conduct and national interests for personal gain.

In a related development, veteran journalist Jenerali Ulimwengu yesterday asserted that Mwalimu Nyerere’s spirit continues to haunt a number of government leaders now embracing corruptive practices at the expense of the Tanzanian masses, reports SEBASTIAN MRINDOKO.

Speaking during a one-day symposium at the University of Dar es Salaam in memory of Mwalimu’s death on October 14, 1999, Ulimwengu said there were many Tanzanians who tend to hail Mwalimu’s actions in words but not in deeds.

He said when such people are entrusted with government and public leadership positions, they usually turn their offices into de facto private business centres rather than proper public service vehicles.

According to Ulimwengu, during his presidency Mwalimu could have ordered his then finance minister Edwin Mtei to take money from the central bank and put it in his (Mwalimu’s) personal bank accounts within the country or anywhere else in the world if he had wished to do so, but he didn’t.

But he lamented the existence of national leaders who have failed to follow the example set by Mwalimu in terms of leadership integrity.

He noted that most politicians seeking public leadership positions today tend to use huge amounts of money to bribe voters, and then once elected they set out to loot the country’s wealth and resources for all it’s worth.

’’Lack of openness by some government leaders embracing corruption only serves to encourage injustice and oppression in the society,’’ said Ulimwengu, warning that most civil wars in Africa have been caused by corruptive actions committed by leaders.
 
Tuhuma zisipuuzwe

na Tamali Vullu na Irene Mark
Tanzania Daima


MADAI dhidi ya kushamiri kwa ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, jana yalipata sura nyingine baada ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, kuibuka na kusema kuwa madai hayo hayapaswi kudharauliwa na viongozi.
Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka minane tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere jana, Mwinyi alisema kuwa watu wanaotoa madai hayo wana akili na wameamua kufanya hivyo kutokana na hali ya mambo wanayoishuhudia.

Wakati Mwinyi akitaka kutopuuzwa kwa tuhuma hizo, mwanaharakati mwingine, Jenerali Ulimwengu, naye ameonya kuwa watu wanaodaiwa kuwa mafisadi, wanahatarisha kuanzishwa kwa vita nchini.

Akizungumza katika kongamano hilo lililoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwinyi alisema akili za watu hivi sasa zimepanuka na ndiyo maana wanaweza kuikosoa serikali hadharani.

"Haya yote ni matunda ya miti aliyoipanda Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alikazania suala la elimu, ili watu waondokane na ujinga," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, hivi sasa watu wako huru kuikosoa serikali na akasema kufanya hivyo ni ‘ruksa'.

"Sasa watu wanaikosoa serikali left, right and centre (kushoto, kulia na katikati), lakini hakuna anayetishiwa wala kukamatwa… haya ni matunda ambayo tunavuna kutokana na juhudi za Mwalimu Nyerere, ambaye alitoa uhuru wa watu kuzungumza na kukosa.

"Kuna mambo mengine yanazungumzwa katika magazeti, yanakereketa, lakini (mimi) sikasiriki… na baadhi yanayokosoa yana maana na yakifanyiwa kazi yanaweza kuleta maendeleo katika nchi yetu," alisema Mwinyi.

Alisema siasa ya kujitegemea haina makosa na wala haitakuwa na makosa, na akashauri iendelee, kwani kinachotokea sasa ni kutofautiana katika njia za kutafuta maendeleo ya nchi.

Pia, alimsifia hayati Baba wa Taifa kwa kueleza kuwa hakuwa mbinafsi na kwamba mpaka anastaafu hakuwa na nyumba wala shamba.

Alisema Mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu iliyokuwa na mshahara na kuingia kuongoza chama kilichokuwa na posho pekee, kwa lengo la kutetea wanyonge na kwamba alikataa kujinufaisha binafsi.

"Nani kati yetu anaweza kufanya hivyo? Hii inaonyesha Nyerere alikuwa mtu wa aina gani. Hakuwa na tabia ya ubinafsi," alisema.

Alitumia nafasi hiyo kuieleza CCM Mkoa wa Dar es Salaam kuwa, wamechelewa kuanzisha kongamano la aina hiyo, kwani walipaswa kuanza mapema baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere.

Naye Waziri katika Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Jamii, Kingunge Ngombale-Mwiru, alitoa mada kuhusu tafakari ya falsafa ya Mwalimu Nyerere, alisema njia nzuri ya kumuenzi ni kusikiliza hotuba zake.

"Kwa kutumia hotuba za Mwalimu Nyerere tunaweza kujifunza zaidi na kuyafanyia kazi, hii ndiyo njia kubwa ya kumuenzi Mwalimu Nyerere," alisema.

Alisema hivi sasa watu wengine wanasahau adui dhuluma, lakini akasema hiyo inawezekana akawa ni adui mkubwa kuliko wengine wanaotajwa.

"Tumezoea kusema Mwalimu alitufundisha kupambana na adui ujinga, maradhi na umaskini na kusahau dhuluma. Hii inawezekana ndiyo ikawa inasababisha haya mengine kutokea.

"Watu wa CCM hili tulitafakari sana, kwani tuna viongozi wanaopenda kufanya dhuluma," alisema Kingunge.

Alisema kuwa rushwa ni aina ya dhuluma, kwani inamnyima mtu haki yake, lakini cha kushangaza wakati mwingine watu wanaishangilia. Alisema hivi sasa viongozi wengi wanaweka mbele masilahi binafsi na kusahau ya taifa.

Akizungumza katika kongamano kama hilo, lakini lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ulimwengu alisema watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanahatarisha amani ya nchi iwapo hawatakuwa tayari kutekeleza maagizo ya hayati Mwalimu Nyerere ya kujikosoa na kujirekebisha.

"Wachochezi wa vita ya baadaye ni mafisadi wa leo," alisema Ulimwengu, hali iliyosababisha makofi na nyimbo kutoka kwa wanazuoni na baadhi ya watu waliohudhuria wakiwemo viongozi wa serikali, wanasiasa, mabalozi, maprofesa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU), Dk. Salim Ahmed Salim.

Ulimwengu alibainisha kuwa sera na mipango mizuri inayotekelezwa ndiyo matokeo ya amani na utulivu ulioimarishwa na hayati Baba wa Taifa.

Kuhusu mwelekeo wa nchi, Ulimwengu alisema hivi sasa ukoloni unarudi kwa kasi kuliko ilivyokuwa kabla ya uhuru.

"Tanzania na Afrika nzima inazidi kuwa koloni la weupe kuliko ilivyokuwa wakati wa ukoloni, siku hizi viongozi hakuna, hawa ni watawala," alisema na kushangiliwa tena.

"Uongozi umegeuka kuwa ni bidhaa inayonunuliwa, mtu anakaa Marekani anapiga hesabu ya kununua jimbo hadi jimbo kwa dola zisizozidi bilioni tatu.

"Wananchi tupo sokoni tunauzwa, mtu anakupigia hesabu ya kuchukua Ikulu ili kutawala nchi kwa dola bilioni kadhaa… fedha inanunua nchi," alisema.

Ulimwengu aliwataka watawala kumuenzi Baba wa Taifa kwa kutekeleza aliyokuwa akipigania ili kudumisha haki, amani na ujamaa kwa kukataa kutawaliwa.

Aidha, aliwataka kufahamu kuwa wananchi si wajinga na kuwashauri wanazuoni hao kuanzisha chama cha ujamaa kwa lengo la kupambana na nguvu mpya ya ukoloni na ubeberu.

"Nyerere kabla ya kifo chake alikuwa mzee lakini alikuwa na mawazo ya ujana, nawashauri vijana wasomi, undeni chama cha ujamaa halafu mwende kwa Msajili wa Vyama vya Siasa muone kama mtasajiliwa," alisema.

Aliongeza kuwa woga wa watawala baada ya Mwalimu Nyerere unasababisha vurugu za mara kwa mara, huku akitolea mfano migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Kuhusu misaada tunayopata, Ulimwengu alibainisha kuwa enzi za uhai wa Baba wa Taifa wakati wa Azimio la Arusha mwaka 1967, aliwataka wananchi kufahamu kuwa misaada ya wahisani itaifikisha nchi mahali pa kushindwa kuwa na sera binafsi na kuzitekeleza.

"Nilitamani kukutana na (Waziri wa Fedha) Meghji, siku chache kabla ya kusomwa kwa bajeti ili nimuulize amekuja lini kutoka Washington… siku hizi bajeti inapangwa Ulaya kwa e-mail tu, hapa waziri ana-download kisha anaenda bungeni kuisoma," alisema Ulimwengu.
 
I couldn't agree with Butiku more, it is imperative for Mkapa must come forward and clear his name by refuting those allegations...otherwise we are going to believe what has been said. Also attorney general must look on this issue and if he finds out that Ex-President used is office inappropriately then he must press charges against him.
 
Du i wonder kama kweli mwalimu alitoa uhuru wa watu kuzungumza. Naweza kusema labda Ben na JK wametoa uhuru huo, hapa naweza kutofautiana na mzee. Na kuhusu corruption, labda hakupokea bribe lakini i am sure alihusika kwenye corruption scandals. Wakati mwingine ni afadhari mtu apokee mlungula kuliko kuwa kwenye mascandal machafu zaidi
 
Tanzania Daima

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amesema kukithiri kwa rushwa na ufisadi serikalini kunatokana na kuwa na viongozi waliosoma, lakini hawakuelimika.

Mwinyi alitoa kauli hiyo jana wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha nne na sita kwa wanafunzi wa Shule ya Kiislamu ya Markaz, iliyopo Chang'ombe, Dar es salaam.

"Kuna matatizo makubwa ya uongozi katika nchi yetu. Tumevamiwa na maovu mengi, ujambazi wa kutumia nguvu, uongo, ulaghai na ujanja. Karibu kila sekta ya maendeleo ya jamii inakabiliwa na tatizo la kukosa viongozi waadilifu. Kuna matatizo ya uongozi katika mpira, taasisi mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

"Na haya tunayoyasoma na kuyasikia kwenye vyombo vya habari kuhusu kukithiri kwa maovu serikalini, yanatokana na kuwa na viongozi ambao wamesoma lakini hawakuelimika. Wangeelimika wasingelitenda haya tunayoyashuhudia na kuyasikia leo," alisema.

Alisema viongozi waliosoma na kuelimika ni waadilifu kwa sababu elimu ni nguvu ya ajabu ambayo mtu yeyote anayeipata humwingia ndani ya moyo wake na kumbadilisha kitabia.

"Viongozi walioelimika ni waadilifu, wana msimamo, huruma, ubinadamu, wenye upendo kwa wanaowaongoza kama wanavyojipenda wao," alibainisha mzee Mwinyi.

Kutokana na hali hiyo, Mwinyi aliwasihi wahitimu hao kuongeza bidii katika masomo yao ya juu ili waweze kuelimika vizuri na kuziba pengo la uongozi lililopo sasa nchini kwa kulitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa.

Akizungumzia umuhimu na faida za elimu, Mwinyi alisema elimu humsaidia mtu aliyeipata kumudu mambo ambayo awali hakuyaweza na hivyo kuweza kuboresha maisha yake.

Alibainisha kuwa ujinga ni adui namba moja wa kila jamii, kwani maadui wengine kama umaskini na maradhi hutokana kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa elimu.

"Tuna maadui watatu nchini - ujinga, umaskini na maradhi. Hata hivyo, mimi naamini ujinga ndiyo adui mkubwa na naweza kusema kuwa ni mama wa adui wengine wote, lazima tupigane vita vya jihadi kumtokomeza adui ujinga," alisema.

Alisema elimu ni safari ndefu ambayo mtu huianza mara tu anapozaliwa na inakoma pale anapofariki dunia.

Mwinyi aliwashauri wahitimu kusoma kwa bidii elimu zote, elimu ya duniani na ile ya dini na kutoitelekeza elimu ya dunia kwa sababu elimu hiyo ni muhimu mno kwa maisha ya bora ya duniani.

Kauli ya Mwinyi kuhusu viongozi wa umma kukosa uadilifu, imekuja wakati viongozi wengi serikalini wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali za ulaji rushwa na ufisadi, wakati baadhi yao wamelazimika kujiuzulu uongozi.

My Take:
Kwanini Mzee Mwinyi naye asipate nafasi kama aliyopata Mwalimu Mei Mosi Mbeya ya kuhutubia Taifa? Hakuna kasherehe kakitaifa ambako Mzee wetu angeweza kuzungumzia masuala muhimu yanayolikabili Taifa hadi tumsikie anazungumzie pembezoni? Kama kuna mtu anahutuba yake hiyo ni vizuri tungeipata.

NB: Kuchomekea kizenji: NI kutuma ujumbe mzito kwa kucheza na lugha kama alivyo fanya mzee Mwinyi "kusoma na kuelemika". M.M. Original
 
Tanzania Daima

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amesema kukithiri kwa rushwa na ufisadi serikalini kunatokana na kuwa na viongozi waliosoma, lakini hawakuelimika.

Waache kutuzuga. Tutamwuliza Mh. Mrema kama wale jamaa aliowakamata na dhahabu uwanja wa ndege alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kama walikuwa HAWAJASOMA NA KUELIMIKA. Au kama suala la Chavda na Benki Kuu lilifanywa na ambao HAWAJASOMA NA KUELIMIKA.
 
Namshangaa sana mzee huyu! alikuwa Raisi kwa miaka kumi hakuyaona hayo?
Wakati wa utawala wake rushwa ilizagaaa kila mahali kuanzia Loliondo hadi kwenye makontena pale bandarini.Yote haya hakuyasikia wala kuyaona! hakutambua kuwa kusoma tu haitoshi bali pia inapaswa kuelimika? au alikuwa kiziwi na kipofu hapo hapo?.
Leo hii mzee Mwinyi ndiyo anaanza kuona huruma kwa Taifa na wananchi wa kawaida!..Kweli ishi uyaone!
Naona sasa kunaanza kamchezo fulani kwa viongozi wetu kuwa baada ya kutoka madarakani ndiyo wanajifanya wanamachungu na Taifa letu.Tumeshamsikia Sumaye na sasa Mwinyi na sitoshangaa siku moja Lowasa au Karamagi watakapokuja kutuasa kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo.
Jamani viongozi wa CCM oneeni huruma wananchi wa kawaida,wanateseka na kutaabika huku wengi wenu mkijinufaisha bila kujali vilio vyao.
 
Mzee apumzike tu kwa sasa , si vema jamani kum mis use huyu mzee hata graduu za sekondari jamani, umma uelewe huyu mzee ni chancellor MUHAS, hapo ndio jukwaa lake ktk taaluma na mahubiri yake yanaweza kufikia hadhira na kueleweka.

Mzee tumekusikia ila washauri wawe makini na aina za matukio wanayokualika.
 
This is funny, a politician with a not so clean record chastising fellow dirty doers. Hii ni kama vile Museveni kumpigia kelele Mugabe
 
labda yeye hakumbuki ufisadi uliofanyika chini ya utawala wake. Au anadhani sisi ndio hatukumbuki!

1.Huenda .magnitude na scope vinatofautiana ktk ufisadi uliokuwa unafanywa enzi hizo..na pia scope ya awareness kwa wananchi ilikuwa ndogo sana...ufisadi wa sasa ni sawa na kula mboga yote usibakize hata makombo..watoto walale na njaa!

2.Ni zamu yake nae awapashe kama mstaafu.Ikumbukwe pamoja na Mstaafu kupewa jina la mzee Ruksa..siyo sifa bali ni kejeli .
 
Amesahau kuwa mkewe alikuwa mjasiriamali wa kwanza kuitumia Ikulu? Huyu mama si ndiye yule aliyetuuzia walevi Stella Artois na kuingiza majenereta ya umeme nchini? Watanzania hatusahau bwana.
 
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amesema kukithiri kwa rushwa na ufisadi serikalini kunatokana na kuwa na viongozi waliosoma, lakini hawakuelimika.


Pengine hiki ni Kizenj ama Kizaramo kinachomaanisha, 'TUNA BOMU LA VIONGOZI WALIOSOMA KWELI KWELI LAKINI HAWANA MAADILI.'

Angalia shule za Mafisadi, ndiyo utajua ukweli wa hili, wapo DK, wenye Masters, BSc, BA, nk.
 
Hakuna mtu fisadi Tanzania kama huyo Ali Hassan Mwinyi ,inasemekana huyu ndie alieshauri uchaguzi wa Zanzibar uibiwe kwa hali yeyote hata ikibidi kuwaua Wazanzibari wote na ndie aliehakikisha hoja yake hiyo inapita,ila kila kwenye kundi la wabaya basi hutokea ndani yao akawepo mwenye huruma na ndie aliewatonya wananchi wa Zanzibar watulie tuli ,kwani jamaa wamedhamiria kuua mpaka sisismizi ikiwa wenye msimamo uliosawa na Oginga watasimama kudai na Zanzibar ni ndogo sana hakuna pa kukimbia wengi watauliwa wakiwa hawajafika wanakokimbilia ,hivyo wananchi wakatulia ,lakini huyu Mwinyi amepoteza upendo na Watu wa Zanzibar ni mnafiki nambari moja na ana maneno mazuri sana anapozungumza lakini ndani ya moyo wake amejaa uwovu ,huyu ni mtu ambae ameukana Uislamu hivyo hafai hata kuhudhuria mahafali ya Kiislamu ni wakati aliposema kuwa katika CCM tuna Katiba yetu na waislamu wana msahafu wao (wakati wa uprisingi za mambo ya kidini Zanzibar) .aliyatamka maneno hayo ambayo Muislamu hapaswi kusema hivyo ,Mwinyi kwa waislamu wenye siasa kali za dini anaonekana ni murtadi na haruhusiwi kurudi tena kwenye Uislamu anatakiwa abakie hukohuko na kitabu chake cha Katiba na kama ataamua kurudi basi adhabu yake ni kukatwa kichwa (hapo ndipo penye utamu wa Uislamu) au aweke maneno yake sawa kitu ambacho amewahi kushauriwa personal kwa msemo alioutumia ,Je Mwinyi amerekebisha maneno yake hayo aliyoyatoa kwenye Ofisi ya CCM kisiwa Ndui ?
 
Mwanakijiji,
Toka lini nyani akaliona kundule!..
Hata hivyo point yake bado imesimama palepale... nakubaliana naye 100% kwamba Viongozi wamesoma, lakini hawakuelimika!.... ndio wale mimi huwaita wenye ELIMU ya KUIGA!...
Na elimu zao hawaelewi kabisa wanayoyafanya kuwa ni makosa makubwa!.. Utetezi toka IKULU na hata Mwanasheria mkuu wote wanatetea UFISADI.. sasa kweli hapo tuna nchi wasomi kweli!
 
Waache kutuzuga. Tutamwuliza Mh. Mrema kama wale jamaa aliowakamata na dhahabu uwanja wa ndege alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kama walikuwa HAWAJASOMA NA KUELIMIKA. Au kama suala la Chavda na Benki Kuu lilifanywa na ambao HAWAJASOMA NA KUELIMIKA.

Na pia kumwachia Capt. Azizi mtoroshaji mwingine wa dhahabu ati kisa mamke Capt Aziz alimfuata na kumlilia Rais.

"Watanzania Si Mabwege Tena" Mh. Dk. Mwakyembe, MB (Kyela)
 
chimbuko la ufisadi lilianzia kwake baada ya kukubali kulizika azimio la arusha sasa anatutonesha vidonda. kwanini na yeye tusimweke kwenye list ya akina NKAPA??
 
nakubaliana naye 100% kwamba Viongozi wamesoma, lakini hawakuelimika!.... ndio wale mimi huwaita wenye ELIMU ya KUIGA!...
Na elimu zao hawaelewi kabisa wanayoyafanya kuwa ni makosa makubwa!.. Utetezi toka IKULU na hata Mwanasheria mkuu wote wanatetea UFISADI.. sasa kweli hapo tuna nchi wasomi kweli!
Hapa kweli mkuu umesema kweli tupuuuuuuuuuuuu!
Lakini????...............................................
 
Back
Top Bottom