BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,109
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ametoa maneno mazito na ya hekima, ambayo kwa tamaduni nyingi za Kiafrika, hutolewa na wazee waliokula chumvi nyingi.
Mwinyi, ni mmoja wa viongozi adhimu wanaoweza kuwekwa katika daraja la juu miongoni mwa wanasiasa ambao hujipambanua kwa kutopenda makuu au hata kujikweza, tangu zama akiwa madarakani.
Watanzania walio wengi wanamkumbuka mzee huyo kwa maneno ya busara aliyoyatoa wakati alipokuwa akijilinganisha na mtangulizi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Huku akijua kwamba, yeye ndiye aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mwinyi aliwaeleza Watanzania kwamba, yeye alikuwa ni mtu ambaye asingeweza kulinganishwa na Nyerere na akasema kama kungekuwa na kipimo, basi yeye (Mwinyi) angekuwa ni kichuguu na Mwalimu ni Mlima Kilimanjaro.
Kwa hakika taifa linaweza likapata shida sana kupata aina ya kiongozi mkuu wa nchi, ambaye alipokuwa madarakani, alikuwa mtu mnyenyekevu, msikivu, mkarimu, mvumilivu na mcha Mungu wa aina ya mzee wetu Mwinyi.
Miaka takriban 12 tangu aondoke madarakani, Watanzania sasa wanaweza wakajithibitishia kwa kuyaangalia maisha yake na pengine hata kumuomba radhi kiongozi huyo aliyetudhihirishia kuwa alikuwa miongoni mwa viongozi wachache waadilifu wa kweli kweli waliopata kulitumikia taifa hili.
Tumelazimika kumtaja na kuelezea kwa sehemu tu wasifu wa kiongozi wetu huyo mstaafu, kutokana na ujumbe mzito wa maneno aliyotupa Watanzania siku mbili zilizopita.
Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa gazeti la Changamoto, aliwataka waandishi wa habari kutimiza wajibu wao kwa kuendelea kuwakosoa viongozi wao.
Kiongozi huyo alisema kuwa, waandishi wa habari wana dhima ya kuikosoa serikali na viongozi wake kwa sababu imejengeka tabia ya hatari miongoni mwa viongozi hao, ya kujisahau katika kutimiza wajibu wao.
Mwinyi maarufu kwa jina la Mzee Ruksa, alisema kuwa magazeti, ni moja ya njia madhubuti zinazoweza kutumika kukuza demokrasia nchini na sehemu nyingine duniani.
Alisema kuwa, watu wengi hupata habari za mambo yanayotokea kupitia magazeti, hivyo magazeti hayo na waandishi wake wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa, wanawapatia habari wananchi wenye kiu ya ufahamu.
Uzito wa maneno hayo ya rais wetu mstaafu, unaonekana hivi sasa, kutokana na ukweli kwamba, baadhi ya viongozi serikalini wamekuwa wepesi sana kuponda baadhi ya mambo yanayoandikwa magazetini dhidi yao.
Hulka hiyo mbaya ya baadhi ya viongozi, imefikia hatua ya kuwafanya baadhi ya waandishi wa habari wanaoonekana kuwa mstari wa mbele kukosoa waonekane kuwa ni wasaliti, wachimvi, wazushi na watu wasiolitakia mema taifa hili.
Hivi sasa ni dhahiri kwamba, wakati viongozi wa aina hiyo wakitamka kwa maneno tu kuwa tayari kukosolewa, baadhi ya maamuzi yao yamekuwa yakithibitisha kuwa, kile wanachokitamka sicho wanachokiamini kwa dhati na kukitekeleza.
Tunaamini kwamba, maneno mazito aliyotoa kiongozi huyo mstaafu, yanaweza yakawa ni somo zuri kwa baadhi ya viongozi wasio wavumilivu na wasiopenda kuguswa, ilhali wakijua kuwa madaraka makubwa waliyonayo ni dhamana nzito inayoweza kuathiri maisha ya Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kwa sababu hiyo basi, tunaamini pia kwamba, maneno hayo ya mzee wetu yanapaswa kuwa changamoto si kwa viongozi wetu tu, bali hata kwetu wanahabari, ya kuutambua, kuuheshimu na kuuendeleza wajibu wetu wa msingi wa kukosoa, inapopaswa katika misingi ya ukweli pasipo kumhofia yeyote.