Mzee Mwinyi augua, ashindwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dodoma

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,360
8,093
Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameshindwa kuhudhuria mkutano wa 10 wa CCM baada ya kuugua mafua makali akiwa tayari yuko jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu leo Desemba 6, 2022 wakati akisoma salamu zake katika mkutano mkuu wa 10 unaoendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Amesema Mwinyi ameshukuru kwa kumuwezesha kwenda safari ya matibabu na kurudi salama.

“Lakini naomba radhi kwa kutoweza kushiriki katika mkutano wa CCM leo kutokana na kushikwa na mafua makali, japokuwa niko tayari hapa Dodoma,” Rais Samia amemnukuu Mzee Mwinyi. Pia, Rais Samia alisema salamu za Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akieleza kusikitika kukosa mkutano huo.

Amesema Kikwete amesema hakuweza kushiriki kwa kuwa yuko nchini Ufaransa na kwamba atahakikisha kesho atakuwa kwenye mkutano huo.

MWANANCHI
 
Pole sana kwa mzee wetu.
Wamwache apumzike sasa sio kila sehemu kumbeba.
 
Mzee wangemuacha tu apumzike mchanho wake kwa taifa unatosha na umri umesonga sana.

Maana kwa sasa hakumbuki hata majina ya watoto wake.
 
Vasco Da Gama kaanza tena ziara zake za kutifua kodi zetu. Huyu mama Mungu angeingilia kati tupate rais. Hadija kopa na urais wapi na wapi.
 
Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameshindwa kuhudhuria mkutano wa 10 wa CCM baada ya kuugua mafua makali akiwa tayari yuko jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu leo Desemba 6, 2022 wakati akisoma salamu zake katika mkutano mkuu wa 10 unaoendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Amesema Mwinyi ameshukuru kwa kumuwezesha kwenda safari ya matibabu na kurudi salama.

“Lakini naomba radhi kwa kutoweza kushiriki katika mkutano wa CCM leo kutokana na kushikwa na mafua makali, japokuwa niko tayari hapa Dodoma,” Rais Samia amemnukuu Mzee Mwinyi. Pia, Rais Samia alisema salamu za Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akieleza kusikitika kukosa mkutano huo.

Amesema Kikwete amesema hakuweza kushiriki kwa kuwa yuko nchini Ufaransa na kwamba atahakikisha kesho atakuwa kwenye mkutano huo.

MWANANCHI
Ana ngoja nini kufa mimi namtumia salamu popote alipo namwambia "happy dedi dei"
 
Back
Top Bottom