Mzee Mwinyi asimulia alivyopotea Ulaya alipokuwa mwanafunzi; mzungu akataa kugusa hela yale isipokuwa kwa ncha ya penseli

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,794
18,514
Katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', Mwinyi anasema siku hiyo alikuwa anarejea Newcastle kutoka London alikokwenda kwa ajili ya likizo ya chuo.

Anabainisha kuwa kipindi hicho alikuwa anaishi kwenye nyumba iliyokuwa inamilikiwa na Kanisa la Methodist, ikipokea wageni kutoka sehemu mbalimbali wakiwamo wanafunzi kutoka makoloni ya Uingereza.

Mwinyi anasema balaa lilianzia kituo cha treni alikokuwa kwenye foleni ndefu ya kukata tiketi pasi na kujua kwamba hakuwa na nauli kamili.

"Ilipofika zamu yangu nikatoa kiasi kilekile cha fedha kama nilizokatia tiketi wakati wa kuja London kutoka Newcastle, muuza tiketi akaniambia ‘wewe husomi magazeti? Imetangazwa katika redio na kuandikwa magazetini kuwa nauli za treni zimepanda.

“Kusikia vile nikashtuka, nikatoa mfukoni mwangu pesa zote nilizokuwa nazo noti na sarafu nikamkabidhi, yule mzungu akaziangalia fedha zangu kwa dharau akachukua penseli aliyokuwa ameipachika kwenye sikio lake na kutumia ncha yake kuhesabia fedha nilizoweka mbele yake," anasimulia.

Anasema baada ya kuambiwa kuwa nauli yake haitoshi, aliamua kukata tiketi ya kuishia katika Mji wa Darlington badala ya Newcastle, ili baadaye maili 31 (Km 50) atatembea kwa miguu baada ya juhudi zake za kumshawishi mkatisha tiketi kumsamehe shilingi moja iliyokuwa imepelea kwenye nauli yake kugonga mwamba.

Hata hivyo, Mwinyi anasema alijitokeza mzungu aliyejitolea kumwongezea shilingi moja na hivyo kufanikiwa kusafiri hadi Newcastle kama alivyotarajia lakini anasema haukuwa mwisho wa matatizo yake kwa kuwa baada ya kufika huko Newcastle alipotea alipoamua kupita njia ya mkato badala ya kufuata barabara kubwa.

"Baada ya kuhangaika kwa muda, nikakutana na bwana mmoja nikamuuliza njia ya kunifikisha Methodisdt International House. Akaniambia tuongozane maana ya yeye anakwenda huko," anasimulia.

Mwinyi anasema raia huyo mwema alimsindikiza hadi karibu na nyumba hiyo na kuhakikisha kuwa ameiona na yeye kurejea alipotoka jambo ambalo anasema aliliona ni la kiungwana na akabaini mzungu huyo hakuwa mkazi wa eneo hilo bali aliamua kumpeleka tu.

Chanzo: Nipashe
 
"Baada ya kuhangaika kwa muda, nikakutana na bwana mmoja nikamuuliza njia ya kunifikisha Methodisdt International House. Akaniambia tuongozane maana ya yeye anakwenda huko," anasimulia.
Huu ndiyo uzuri wa mabeberu aka ngozi nyeupe, angekuwa ngozi nyeusi pale lazima ulambwe viatu, simu na vibao juu kwa nini unatembea mjini bila hela.
 
Sasa hii stori sie walala hoi inatusaidia nini,asubiri kipigo kwa kuikandamiza Zanzibar kiaina, siku hizi dua za waislamu waliojaa imani ni za kuangamiza tu, hakuna mswalie mtume na anaejipitisha kukandamiza na kulalia haki za Waislamu bila ya kuwasahau Mashee wa Taasisi ya Uamsho, malipo ni hapa hapa, mtu atatoka funza kitandani na harufu eneo zima.
 
Huyu mzee kwa umri wake inaonekana ameshaaza kupoteza kumbukumbu, ushahidi wa hili ni kule Chato siku ya kumuaga magufuli pale alipotaka kurudia kuaga mwili mara mbili na akakili kwamba alisahau.

SWALI: Wakati Kitabu Hiki Kinaandaliwa Ilitumika Njia Gani huyu mzee kuweza kukumbuka matukio yaliyotokea zaidi ya miaka 15 nyuma ikiwa tu hata watoto wake ameshaaza kuwasahau?

Nb: nimeuliza ili nipate kujua sina maana zaidi ya hiyo.
 
Sasa hii stori sie walala hoi inatusaidia nini,asubiri kipigo kwa kuikandamiza Zanzibar kiaina,siku hizi dua za waislamu waliojaa imani ni za kuangamiza tu,hakuna mswalie mtume na anaejipitisha kukandamiza na kulalia haki za Waislamu bila ya kuwasahau Mashee wa Taasisi ya Uamsho,malipo ni hapa hapa ,mtu atatoka funza kitandani na harufu eneo zima.
Jamani hajaandika kitabu kukusaidia wewe au mtu yoyote yule,bali kuelezea mausha yake ya uongozi wa nchi
 
Jamani hajaandika kitabu kukusaidia wewe au mtu yoyote yule,bali kuelezea mausha yake ya uongozi wa nchi
sasa akakiweke bookshop hapa au humu haswa jukwa hili la siasa kina mchango gani,hayo maswaibu mbona yanawakuta wengi tu,wacheni kushobokea mambo yasio na tija kwa taifa,eti kakutana mzungu blah blah blah.
 
Natamani sana nisome kitabu chote.....hazina kwa vizazi vijavyo
hazina gani iliyomo humo na huyo mtoto wako atafaidika na lipi kubwa la kumsaidia kwenye maisha yake ,kuna cha Nkapa bado cha vasco ,iwe sasa kazi kusoma vitabu vya maraisi wastaafu ,kwa kubwa lipi ? walilolifanya hata leo ikawa ya pili vitabu vyao vina maana saana ,bora hata kitabu cha Mbutolwe mwana wa Umma.
 
Yule mkata tiketi asingeamini kama angeambiwa baadae kuwa "yule uliyemkatalia kisa hana nauli itoshayo ndiye Rais wa JMT".

Ama kweli USIONE UKADHANI
Rais mstaafu wa DRC, Joseph Kabila, naye alishushwa kwenye basi huko Mbeya kwa kuwa hakuwa na nauli ya kutosha. Huo ulikuwa wakati wa hayati Mobutu na wakina Kabila walikuwa wakimbizi hapa Tanzania. Baadaye Kabila akaja kuwa Rais wa DRC.
 
Ila ngozi nyeupe huwa zatuzingua ngozi nyeusi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna ngozi nyeupe wabaguzi sanaa.

Nilishawahi kwenda mji mmoja unaitwa luga.

Nilivyoingia supermaket nikaambiwa jana kuna mtu mweusi alikula shaba hapo nje akafa.

Sikurudi tena mle ndani na sikutoka nje tena kuzurura na izingatiwe nilifuata mwanamke.

Na kimbeme demu akanitambulisha kwa baba yake nje baba yake yupo tungi mbaya nikasema leo ndio mwisho wangu leo nimejileta kibla.
 
huu ndiyo uzuri wa mabeberu aka ngozi nyeupe, angekuwa ngozi nyeusi pale lazima ulambwe viatu, simu na vibao juu kwa nini unatembea mjini bila hela.
Hata south africa ukitolewa mbio na blacks wenzako Ili wakuue we kimbilia kwa mabeberu watakupa msaada ukikimbilia kwa blacks umekwisha,hapo ni SAwa na kukimbizwa na simba ukajiputupa mtoni kwa mamba.
 
Back
Top Bottom