Mzee Mwinyi amlaumu January Makamba kwa kutumia picha yake wakati huu

Mzee Mwinyi amesema hajafurahishwa na picha aliyoposti Makamba baada ya kutumbuliwa ikiwaonyesha wanafurahi pamoja. Kwa mujibu wa taaarifa ya habari Channel Ten.
Inaonesha kuna tatizo sehemu.
Picha yenyewe iko wapi mkuu ungeweka hapa tuione ingenoga zaidi.
 
*RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI ACHUKIZWA KUTUMIWA PICHA YAKE NA JANUARY MAKAMBA, AUITA WARAKA WA KINANA NA MAKAMBA NI UTOTO NA AMPONGEZA JPM KWA KASI KUBWA YA MAENDELEO.*

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi ameelezea kutofurahishwa kwake na kitendo kilichofanywa na aliyekuwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba kutumia picha yake katika mitandao ya kijamii muda mfupi baada uteuzi wake kutenguliwa na Rais Magufuli.

Mzee Mwinyi amesema picha iliyotumiwa na January Makamba katika mitandao ya kijamii ikimuonesha yeye ameketi na January Makamba wakicheka muda mfupi baada ya kufukuzwa Uwaziri imemkwaza kutokana kutumiwa katika mazingira na wakati usiostahili.

Mzee Mwinyi anasema picha hiyo ilipigwa zamani wakati January Makamba alimpomtembea kwa ajili ya kupata uzoefu wake kwa kuwa nae aliwahi kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira na pia alikwenda kumuomba aandike dibaji katika kitabu chake.

===================

Kuhusu waraka ulioandikwa na Makatibu Wakuu Wastaafu Ndg. Abdulrahman Kinana na Ndg. Yusuf Makamba kwenda kwa Baraza la Viongozi Wastaafu, Mzee Mwinyi amesema huo ni Utoto.

Mzee Mwinyi amepongeza majibu yalitolewa na Katibu wa Baraza hilo Mzee Pius Msekwa na kusema walioandika waraka huo wameshindwa kufuata katiba na taratibu za chama na kwamba viongozi wastaafu hawawezi kupoteza muda wao kwa masuala ya kitoto.

================

Mzee Mwinyi amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya kuleta maendeleo kwa muda mfupi.

Amebainisha kuwa ukiondoa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere viongozi wengine waliofuata akiwemo yeye wamefanya juhudi za kuipeleka nchi mbele lakini kasi ya Rais Magufuli ni kubwa zaidi.

Mzee Mwinyi amezungumza hayo nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam, leo Julai 22, 2019.
 
Yule kjana alikuwa sahihi kulipiga kibao hili lizee!
 
Kaenda kulishwa tu maneno mzee wa watu
 
Mzee Mwinyi yeye na picha yake ni mali ya umma, kwani yeye ni mtu wa umma, tena wa vyama vyote.

Picha za wastaafu zinawezatumika kwa heshima
 
Kwani January kuna pahala kwenye post ile amelaumu kutenguliwa kwake? Si kashukuru?

Naelewa kuwa Rais Magufuli atakuwa kampigia simu mzee Mwinyi kumuuliza juu ya hilo. Yan tuna Rais wa ajabu sana kwa kweli! Kufuatilia mambo yasiyo na msingi kwake ni kawaida!
 
Mzee Mwinyi ana miaka 94, kwahiyo ni wa kumvumilia tu vinginevyo, cjui ni kwa vipi akwazwe na ile picha!
Picha ilivyotolewa katika muktadha wa huu mvutano wa sasa ingeweza kuonesha taswira ambayo ingeleta uchonganishi.

Kwa hiyo Rais Mwinyi ana haki kusema aliyosema.

Ila namshangaa hakuongelea tafrani zima lililopelekea picha kutolewa.

Au anatumia busara za kizee kutosababisha mtafaruku zaidi?
 
Makamba ni snitch sana, sasa kwa nini akatumia picha ya mzee Wa watu kwenye majanga yake kama sio uchonganishi. Jamaa mnafki sana.
Ila kwenye picha wanaonekana kufurahia jambo kwenye moja ya pozi zake na wazee, lakini nahisi ametumia ujumbe ule ule wa kufurahi katika kutenguliwa kwake, yaani alitaka kuonyesha kua hana kinyongo na mabadiliko yaliyofanywa na rais, sasa picha hio watu wameitafsri kivingine, kila mtu anakuja na lake ni kutokana na alivyoiona, lakini picha ina ujumbe zaidi ya huo
Screenshot_2019-07-22-14-51-37.png
 
Back
Top Bottom