Mzee Mwinyi amlaumu January Makamba kwa kutumia picha yake wakati huu

Kuna uwezekano January alishauriwa na huyo Mwinyi ila Mwinyi kaambiwa ole wako
 
  • Mzee Mwinyi ni mwenyekiti wa baraza la Wazee wa CCM, Kitendo cha Janaury kuweka picha ile katika post yake ya kwanza kuelezea kutolewa kwenye nafasi yake ni kujaribu kuimply kwamba Mwenyekiti huyo wa baraza la wazee yuko naye
  • Kiukweli January alichemsha
  • Mzee Mwinyi ni raisi mstaafu kutumia picha yake kupokea maamuzi ya raisi aliyeko madarakani tena wa chama kilekile ni kujaribu "kumteta" au "kumsimanga" raisi wa sasa kwa raisi wa zamani
Sahihi kabisa, January aliofanya utoto sana
 
Yaani sisi tumuunge mkono mtekaji na muuaji thubutu we Mzee sigida ya bure unamtania mwenyezi Mungu muunge mkono wewe na familia yako .Maendeleo yapi aliyoyaleta Jiwe ya utekaji au?
 
Mzee acha uoga wewe na wazee wenzio wastaafu wa ccm ,wewe unaona kabisa na wenzio nchi inaenda kudumbukizwa shimoni halafu unasifia we Mzee kabisa ? Nchi imevurugwa ,watu wana hali mbaya ya uchumi we Mzee na sigida yako unamsifia shetani ,hebu tumieni akili nyie wazee wote wa ccm ,bora mfe mmesimamama kuliko kufa mmekaa .
 
Mimi nilitafsiri Kwamba kwakuwa Mwinyi aliwahi kuondoka kwenye uwaziri na Baadae Akaja kuwa raisi wa JMT na yeye Makamba Jr anajifananisha nae akiamini kuondoka kwenye uwaziri Nikufa kwa mbegu Ili iote tena.
 
Acha nikwambie, ukipatwa na matatizo kama hayo, kuna mtu anaweza akafuta namba yako kwenye simu yake ili ionekane hamkuwa na ukaribu wowote, ataku-unfriend kwenye social network na hata mkikutana njiani anajifanya yuko busy na simu yake, hao ndio watu.
Ukimpigia simu anaweza asipokee au akapokea na kukujibu kimkatomkato, yaaan halo ndio haya ok.
Kama hujawahi kukutwa na changamoto za namna hiyo unaweza usielewe lakini leo simbachawene kuna watu wanajiuliza watamuanzaje, walimuheshimu kwakuwa alikuwa waziri, alivyokaa benchi wakampotezea, leo karudi, aibu zimewashika. Maisha lazima yaendelee, lisilokuua linakuimarisha.
 
  • Mzee Mwinyi ni mwenyekiti wa baraza la Wazee wa CCM, Kitendo cha Janaury kuweka picha ile katika post yake ya kwanza kuelezea kutolewa kwenye nafasi yake ni kujaribu kuimply kwamba Mwenyekiti huyo wa baraza la wazee yuko naye
  • Kiukweli January alichemsha
  • Mzee Mwinyi ni raisi mstaafu kutumia picha yake kupokea maamuzi ya raisi aliyeko madarakani tena wa chama kilekile ni kujaribu "kumteta" au "kumsimanga" raisi wa sasa kwa raisi wa zamani
Ni kweli lkn kwanin asitumie ya baba ake ...na picha ile ya nguruwe alimaanisha nin
tapatalk_1563806152767.jpeg
 
Mzee Mwinyi yuko sawa. Kwa nini picha ile itumike wakati huu ? Jibu ni moja tu kuonesha kuwa Mzee Mwinyi yuko upande wa J. Makamba.
Mzee kahoji kwa nini picha ya zamani itumike wakati huu mtu akiwa na majanga yake ?
Mzee wa watu hapendi makuu.
Cyo tu apendi apendi kurupushani za jpm ndio maan kaenda kujisalimishaa mapema
 
Ubatizo wa moto si mchezo. Ikifika hapo, hakuna cha JK wala BWM; wote hao wanakuruka.

Januari aache ujinga. Asijidai anaijua CCM au ana hisa huko. Yeye na baba yake na Kinana wameshadhihirisha kuwa hawaijui CCM kabisa. Ukishatemwa huko wewe ingia chini ya rada tu. Kijana anataka kumzamisha mzee Mwinyi kirahisirahisi vile. Mzee makini yule; anaijua CCM kikamilifu.
 
Huyu mzee hafiki hiyo miaka hata kwa kupigwa bakora. Inazidishwa tu hiyo.miaka.sijui kwa nini. Nakup mfano rahisi tu. Tokea Mwinyi aondoke madarakani ni miaka 24 sasa. Jee unataka kuniambia Mwinyi kaacha uraisi wa JMT akiwa na miaka 70? Jee unataka kuniambia Mwinyi kachukuwa uraisi wa Zanzibar akiwa na miaka 59?
Wamuongezee umri kwa faida ya nani?! Ikiwa Bibi Sitti Mwinyi umri wake ni zaidi ya miaka 80, kinachokushangaza Mwinyi kuwa 95 ni kipi?! Tafuta historia ya elimu ya Mwinyi, unaambiwa kaanza darasa la kwanza mwaka 1933; sasa unaona haiwezekani mtu aliyeanza darasa la kwanza mwaka 1933 leo kuwa na miaka 95?! Au hata historia yake ya elimu na yenyewe imedanganywa?!! Kaanza kushika nafasi ya uwaziri mwanzoni kabisa mwa miaka ya 70, na hapo alikuwa kishapita sehemu nyingi sana kabla hajafika hapo!!
 
Ubatizo wa moto si mchezo. Ikifika hapo, hakuna cha JK wala BWM; wote hao wanakuruka.

Januari aache ujinga. Asijidai anaijua CCM au ana hisa huko. Yeye na baba yake na Kinana wameshadhihirisha kuwa hawaijui CCM kabisa. Ukishatemwa huko wewe ingia chini ya rada tu. Kijana anataka kumzamisha mzee Mwinyi kirahisirahisi vile. Mzee makini yule; anaijua CCM kikamilifu.
Mzee kaona jamaa anatafuta wa kuzama naoo Yani kamkataa balaa sijui kama hajafuta pichaa ilee
 
Back
Top Bottom