TANZIA Mzee Muhidin Ndolanga afariki dunia, aliwahi kuhudumu kama rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Innallillahi Wainna Illaihi Raj Un. Mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi. Huyu ndio Senior chalii enzi zake.
 
Binadamu tukiwa duniani tunapita mapito mbalimbali katika harakati za maisha na wakati mwingine mnajikuta katika migongano ya hapa na pale,nilipoiona hii habari ghafla nimejikuta nakumbuka kifo cha mzee mwenzake Said El maamry ambaye naye amefariki wiki chache tu zilizopita,
Nakumbuka wawili hawa kipindi fulani Ndolanga akiwa bado mwenyekiti wa FAT waliwahi kurushiana maneno ya hapa na pale kupitia vyombo vya habari hadi kufikia Ndolanga kumtaka El maamry amuombe radhi vinginevyo angemshtaki lakini nafikiri baadaye waliyamaliza kiutu uzima kwani sikumbuki vyema walivyomalizana.
Leo hii wazee hawa wote wameiacha dunia tena kwa kufuatana maana wamepishana wiki chache tu, basi nawaombea kwa mwenyezi Mungu viumbe wake hao na awasamehe madhambi yao na awape mapumziko mema,Amiina.
Watoto wa mjini hao na wote walikuwa mawakili walikuwa wanajuana
 
Medani ya soka nchini imepata pigo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga kilichotokea leo jioni Dar es Salaam

Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameiambia Mwanaspoti kuwa kifo cha Mzee Ndolanga kimetokea katika Hospitali ya TMJ

"Ni kweli shirikisho na familia ya mpira wa miguu tumepata pigo la kuondokewa na Mzee wetu Alhaji Muhidin Ndolanga aliyewahi kuwa Rais wa TFF kilichotokea leo katika Hospitali ya TMJ.

Kwa sasa taratibu za kuuhifadhi mwili wa Mzee wetu ndio zinaendelea hivyo taarifa rasmi kuhusu utaratibu wa mazishi zitatolewa," alisema Ndimbo.

Ndolanga atakumbukwa kwa misimamo yake pindi alipokuwa Rais wa TFF na kabla ya hapo akiwa mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) kuazia 1992 hadi 2004

Hajawahi kuwa rais wa TFF
 
On 8 April 2003, the chairperson of the Tanzania Football Association (FAT), Muhidin Ndolanga, assaulted Emmanuel Muga, a reporter from the weekly newspaper “The Express”, for allegedly photographing him illegally.

Muga and 10 other reporters from “Mtanzania”, “Mwananchi”, “Daily News”, “The Express”, ITV and Radio Times FM went to Ndolanga’s office to seek comment on his decision to adjourn the association’s general assembly, which was scheduled for 5 April.

Ndolanga assaulted Muga when the reporter took a photograph in his office. Ndolanga also confronted the reporter, telling him that he “did not look like a newspaper man,” and had not been given permission to take photographs.

During the same incident, Ndolanga told the other 10 reporters to identify themselves. They were wearing press cards at the time and were not unknown to Ndolanga, who had met many of them at sporting events and press conferences.

“Where are you coming from and who has called you here?” Ndolanga rebuked the journalists. He expelled them from his office saying that he did not deal with soccer issues in his private office and that they had arrived there without a prior appointment.
 
Binadamu tukiwa duniani tunapita mapito mbalimbali katika harakati za maisha na wakati mwingine mnajikuta katika migongano ya hapa na pale,nilipoiona hii habari ghafla nimejikuta nakumbuka kifo cha mzee mwenzake Said El maamry ambaye naye amefariki wiki chache tu zilizopita,
Nakumbuka wawili hawa kipindi fulani Ndolanga akiwa bado mwenyekiti wa FAT waliwahi kurushiana maneno ya hapa na pale kupitia vyombo vya habari hadi kufikia Ndolanga kumtaka El maamry amuombe radhi vinginevyo angemshtaki lakini nafikiri baadaye waliyamaliza kiutu uzima kwani sikumbuki vyema walivyomalizana.
Leo hii wazee hawa wote wameiacha dunia tena kwa kufuatana maana wamepishana wiki chache tu, basi nawaombea kwa mwenyezi Mungu viumbe wake hao na awasamehe madhambi yao na awape mapumziko mema,Amiina.

Tatizo la hiki kirusi hata sisi twaweza kuwa ni matter of few weeks away
 
Enzi za FAT Mzee Ndolanga akiwa mwenyekiti alitaka Timu ya home ipande daraja Katavi Rangers ilipocheza na Tiger ya Tunduma hapo Sokoine walifungwa goli mbili ilibidi wachezaji wa katavi wajidondoshe kila mtu akiguswa anaanguka kajifanya kaumia wakabaki sita hiyo mechi haikuendelea na Mwenyekiti akaamuru mechi ichezwe shamba la bibi hapo huku Tiger ikiwa ya moto balaa Katavi walikufa hapo hapo Mzee ndolanga akiwaangalia walikuja kupanda msimu unaofuata kwa figisu na kushuka daraja aliwabeba sana nyumbani watu wenyewe hawabebeki...
RIP Mzee Ndolanga...
 
Back
Top Bottom