TANZIA Mzee Muhidin Ndolanga afariki dunia, aliwahi kuhudumu kama rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

bumilo

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
332
250
Medani ya soka nchini imepata pigo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga kilichotokea leo jioni Dar es Salaam

Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameiambia Mwanaspoti kuwa kifo cha Mzee Ndolanga kimetokea katika Hospitali ya TMJ

"Ni kweli shirikisho na familia ya mpira wa miguu tumepata pigo la kuondokewa na Mzee wetu Alhaji Muhidin Ndolanga aliyewahi kuwa Rais wa TFF kilichotokea leo katika Hospitali ya TMJ.

Kwa sasa taratibu za kuuhifadhi mwili wa Mzee wetu ndio zinaendelea hivyo taarifa rasmi kuhusu utaratibu wa mazishi zitatolewa," alisema Ndimbo.

Ndolanga atakumbukwa kwa misimamo yake pindi alipokuwa Rais wa TFF na kabla ya hapo akiwa mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) kuazia 1992 hadi 2004

Maswali na majibu kati yake na Maulid Kitenge yalisisimua sana enzi hizo. Nanukuu: "Tulia bwana mdogo, hutuongei kama bata pa pa pa pa...." RIP mzee Ndolanga
 

uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Bado hujihurumii tu na kuwa uko vizuri?!
Mimi sijihurumii,kwa nini wewe unihurumie? Huvijui vituo vya watoto yatima ukaenda kuwahurumia,unahangaika na mimi mwenye uwezo wa kupata komputa kuingia jamii forume,are you serious?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,683
2,000
Mimi sijihurumii,kwa nini wewe unihurumie? Huvijui vituo vya watoto yatima ukaenda kuwahurumia,unahangaika na mimi mwenye uwezo wa kupata komputa kuingia jamii forume,are you serious?

Wapi umeona ninakuhurumia au hata nmekuhurumia?

Usiniwekee maneno mdomoni mwangu tafadhali!
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,328
2,000
Apumzike kwa amani Muhidini Ndolanga.

Ila kwa mara nyingine tanzia zimekuwa nyingi wajameni.

Kwamba madaktari wa mikoa walipokutana majuzi walipendekeza chanjo ifanywe kuwa lazima?

Yawezekana hatuko vizuri kwani zile mortuary (wodi 26 au 10) hawa ndiyo haswa ziko mikononi mwao.

Eeh Mola wetu bora ungesema na yule Farao mwenyewe kabisa, vinginevyo mawazo yake hayatatoka kwenye urais, post 2025.
Kwa hiyo Marehemu hakuchanja
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,683
2,000
Kwa hiyo Marehemu hakuchanja

Umekurupuka, comment #31 inahusika:

IMG_20210922_161037_457.jpg
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,328
2,000
Mambo mengine ya kitaalamu msiyokuwa na ujuzi nayo mngekuwa mnakaa kimya!

Yaonesha hata hujawasikia wanaokumbushwa na mheshimiwa jaji kukaa kimya kwa kuwa siyo kazi zao.

Madaktari wa hospitali za rufaa za mikoa wanapendekeza chanjo iwe lazima ila vi mburumundu fulani vinajua kuliko wao?!

Hata kujishangaa hamna?!

Ashindwe askofu Rashid na alegee.
Serikali imesema chanjo ni hiyari.
Na kusisitizia hilo wewe mwenyewe unasema/ au kuandika kwamba chanjo iwe lazima.

Sasa watu wakufute wewe au ?? Zaidi ya hapo tumekuuliza Marehemu hakuchanja.
Hutaki kujibu unakimbilia ujuzi ambao upo kichwani kwako sio kwamba kila mtu anao.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,683
2,000
Serikali imesema chanjo ni hiyari.
Na kusisitizia hilo wewe mwenyewe unasema/ au kuandika kwamba chanjo iwe lazima.

Sasa watu wakufute wewe au ?? Zaidi ya hapo tumekuuliza Marehemu hakuchanja.
Hutaki kujibu unakimbilia ujuzi ambao upo kichwani kwako sio kwamba kila mtu anao.

Wewe si tulishafika comment #86?

IMG_20210922_175221_910.jpg


Hii ikiwa tumepitia pia comments #37 na #59 ambapo unayouliza sasa yalishajibiwa.

Huku kujitoa kwako ufahamu, kwa hakika ni wa kipaji cha kuzaliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom