TANZIA Mzee Muhidin Ndolanga afariki dunia, aliwahi kuhudumu kama rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
16,775
2,000
Hivi hapa mtaalam ni nani?
Unataka kuniambia kupewa chanjo bure bila kujua aliyekupa aliigunduaje ndo utaalam?
Mbona mnadhalilisha taaluma?
Eti mtu anakwambia TUMEJIRIDHISHA. umejiridhisha nini?
ungekuwa na uwezo wa kujiridhisha si ungegundua ya kwako?
Jitafakalini mara mbili,msidhani kila mnayeongea naye ni mbumbumbu.
Hizo chanjo za ndui,surua,polio,ukoma nk ulizochoma tangu utotoni Wazazi wako walidhithibitisha?
 

kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
5,937
2,000
Hivi ni kweli Ndolanga ndiye aliyechomesha ile ishu ya umri wa wale wachezaji wa Serengeti boys ya kina Nizar Khalfani?
 

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,737
2,000
Apumzike kwa amani Muhidini Ndolanga.

Ila kwa mara nyingine tanzia zimekuwa nyingi wajameni.

Kwamba madaktari wa mikoa walipokutana majuzi walipendekeza chanjo ifanywe kuwa lazima?

Yawezekana hatuko vizuri kwani zile mortuary (wodi 26 au 10) hawa ndiyo haswa ziko mikononi mwao.

Eeh Mola wetu bora ungesema na yule Farao mwenyewe kabisa, vinginevyo mawazo yake hayatatoka kwenye urais, post 2025.
Kwani ukichanjwa ndio hupati virusi? au hutaugua? unajuaje kama hakuchanjwa ama alichanjwa? bwashee siku ikifika hata ufanyeje utaondoka tu.
 

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,825
2,000
Alimtandika ngumi mwanasiasa mmoja. Kiboko ya Mauldi Baraka wa Kitenge alimwambia hana shule.
 

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,570
2,000
Mwamba mwingine baada ya Hanspope umeondoka

Juma Othman Kapuya akiwa Waziri wa Michezo na Hayati Said Hamad El mamry walitaka kumpeleka peleka wakajisahau kuwa Huyu Mmakonde alikuwa na misimamo yake

Akiwa Mkurugenzi wa Misitu aliwahi kumtwanga Makonde Waziri wake Hayati Sebastain Kinyondo ( Mzee wa Kiko)

Pole sana Maulid Baraka wa Kitenge kuondokewa na aliekuwa kiboko yako ya Interview

Hakuwa anaogopa Interview na Mwandishi yeyote na Majibu Sahihi utayapata tu

I wish zile Interview korofi za wakati ule ziwekwe hadharan watoto wamjue Jabali hili
Kitenge: Kwanini Taifa Stars imeshindwa kuweka kambi kwa wakati?

Ndolanga: Unajua wewe Maulid mimi ni sawa na babayako mzazi, sasa kwanini unaniuliza maswali magumu hivyo?
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,698
2,000
Medani ya soka nchini imepata pigo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga kilichotokea leo jioni Dar es Salaam

Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameiambia Mwanaspoti kuwa kifo cha Mzee Ndolanga kimetokea katika Hospitali ya TMJ

"Ni kweli shirikisho na familia ya mpira wa miguu tumepata pigo la kuondokewa na Mzee wetu Alhaji Muhidin Ndolanga aliyewahi kuwa Rais wa TFF kilichotokea leo katika Hospitali ya TMJ.

Kwa sasa taratibu za kuuhifadhi mwili wa Mzee wetu ndio zinaendelea hivyo taarifa rasmi kuhusu utaratibu wa mazishi zitatolewa," alisema Ndimbo.

Ndolanga atakumbukwa kwa misimamo yake pindi alipokuwa Rais wa TFF na kabla ya hapo akiwa mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) kuazia 1992 hadi 2004

Alikuwa fisadi acha wapungue. Bado Singh na Rugemalira na akina Jakaya Kikwete
 

chuma cha mjerumani

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
9,113
2,000
nakumbuka maulid kitenge wa radio one kipindi cha michezo walikuwa wanasumbuana sana na huyuu mzee kwenye mahojiano hadi raha.

Anaekumbuka baadhi ya mahojiano atushushie hapa.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,739
2,000
Mwamba mwingine baada ya Hanspope umeondoka

Juma Othman Kapuya akiwa Waziri wa Michezo na Hayati Said Hamad El mamry walitaka kumpeleka peleka wakajisahau kuwa Huyu Mmakonde alikuwa na misimamo yake

Akiwa Mkurugenzi wa Misitu aliwahi kumtwanga Makonde Waziri wake Hayati Sebastain Kinyondo ( Mzee wa Kiko)

Pole sana Maulid Baraka wa Kitenge kuondokewa na aliekuwa kiboko yako ya Interview

Hakuwa anaogopa Interview na Mwandishi yeyote na Majibu Sahihi utayapata tu

I wish zile Interview korofi za wakati ule ziwekwe hadharan watoto wamjue Jabali hili
Alikuwa jeuri na aliyekuwa anampa ujeuri alikuwa anajulikana,mbona badaye alikuja kutulia

Ova
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,737
2,000
Jibu hoja kwa hoja.
Tofautisha wataalam,na wanaokariri kilichogunduliwa na wataalam.
Si ajabu hiyo amri unayotoa kwa wasiokuhusu ni mojawaopo ya madhara ya kuchanjwa.

Kwa hiyo wewe kijiweni uko vizuri zaidi ila madaktari wakuu wa mikoa ambao taarifa za wagonjwa na mortuary zote za mikoa yao ziko mikononi mwao wamekariri?

Bado hujihurumii tu na kuwa uko vizuri?!

"No wonder ACP Kingai hakuisha tukumbushane kuachana na ambayo hayakuwa kazi yake!"

Hiiiiii bagosha!
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,737
2,000
Kwani ukichanjwa ndio hupati virusi? au hutaugua? unajuaje kama hakuchanjwa ama alichanjwa? bwashee siku ikifika hata ufanyeje utaondoka tu.

Suala la chanjo si rahisi kama unavyodhani.

Ndiyo maana kila fani ina wataalamu wake.

Mwulize ACP Kingai kupata mrejesho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom