'Mzee mtoto' mbabe aliyetutesa sana lakini mwisho wake ulikuwa mbaya sana

jooohs

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
2,066
8,593
Kama ambavyo kumewahi tokea wababe katika sehemu tofauti tofauti kwa watoto wa mjini, kwenye migodi mikubwa, wazee wa connection, makundi ya wababe, ubabe wa kutumia pesa, makundi ya wauzaji wa madawa ya kulevya

Ubabe huo huo ndio Ulikuwa unafanyika sehemu nyingi za vijijini sema tu, kusambaa kwa information ndio ilikuwa tabu yaani mtu anakuwa maarufu kwenye kijiji kimoja tu au viwili,

Ubabe uliokuwa unafanyika kijijini ulikuwa balaa kwani matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi yalikuwa yameshamiri sana, . Familia ambayo ilikuwa na vijana wengi, au ukoo wao ni mkubwa ndio ilikuwa inaamua kila kitu, kipindi hiko ukitaka kupigana na mtu lazima kwanza uangalie back ground yake, kama hapaingiliki bora utimue mbio.

Hii ilikuja kuwa tofauti kwenye kijiji tulichokua tukikaa kwani kulitokea na mwamba mmoja ambaye alikuwa na miguvu ya ajabu,?(jina la utani alikuwa anaitwa 'mzee mtoto' kwenye familia yao alizaliwa peke yake, baada ya mama yake kukaa muda mwingi bila kupata mtoto inasemekana alienda kwa sangoma ndio jamaa akazaliwa baada ya hapo akupata mtoto mwingine.

Katika kijiji chetu kulikuwa na familia moja inawatoto wa kiume kibao kama 16 halafu wanaukoo mkubwa balaa walikuwa wanaishi pamoja yaani kila mmoja na kijumba chake cha majani mmoja wao akileta taarifa amechokozwa, wanatoka wote walikuwa wanatembeza kipigo cha mbwa koko, serikali ilikuwa inaendeshwa na mwenyekiti na sungu sungu nao walikuwa wanaagalia sura kwenye kutoa maamuzi.

Kuna siku iliyowaacha raia midomo wazi kwani kuna jamaa mmoja kwenye hiyo familia alimkuta mzee mtoto yuko ndani ya shamba lao amekata miwa kibao amekaa anakula akaenda kumuuliza alijibiwa na kipigo cha kufa mtu, jamaa ikabidi atoke nduki kwenda kuwaambia makaka zake, bila kupoteza muda wakatoka na zanaa kwenda kumfundisha adabu jamaa

Walizani watamkuta labda amekimbia lakini walimkuta pale pale shambani, wakaenda wote kumchangia asee jamaa walipigika balaa mtu kama 6 hivi, kisha akawaweka chini ya ulinzi kila mmoja akabebeshwa miwa ya kutosha hadi kwenye getto la huyo jama 'mzee mtoto'

Baada ya siku kadhaa kupita wazazi wote wawili wa mzee mtoto walifariki ndani ya siku moja habari zikaenea jamaa ndio atakuwa kahusika, kijiji kikamtenga mazishi akafanya peke yake nyumbani kwao.

Kuanzia hapo akatengeneza uadui mkubwa na raia, akikuta ngombe zinachungwa karibia na shamba lake zote anazikatakata miguu, wale vijana waliokuwa wanazunguka mtaani akikudaka kwenye anga zake anakupeleka shambani unamlimia hadi jioni ndio unaondoka

Jamaa alikuwa nyumbani kwao amebaki mwenyewe, masaa 24 unakuta kavua nguo zote anafanya kazi ya kunoa panga lake yaani siku nzima nikunoa panga na kulimwagia maji.

Kuna wale wamasai waliokuwa wanatoka vijiji jirani kuja kulisha mifugo yao, walikuwa na dharau balaa, kunasiku mzee mtoto alivizia akakata muguu ya ngombe kama 50 za wamasai na kutoa kipigo cha maana toka siku hiyo hadi leo mmasai hapitishi mifugo kwenye lile eneo

Jamaa alikuwa anasheria yake akienda buchani anaweza kupa hata sh 100 , nyama anayokula haishikwi na mtu, anajikatia mwenyewe kwa kutumia panga lake, muda mwingine alikuwa anaondoka na paja zima la ngombe na huwezi fanya lolote.

Biashara yake jamaa alikuwa anauza mafuta kwenye yale madumu ya lita 5 wengine wanapenda kuwekea maziwa, sasa alikuwa anachukua mafuta kidogo sana hata robo lita ,halafu anachukua hata madumu hayo 10 anajaza maji anaacha sehemu ndogo sana pale juu kisha ile sehemu anaweka mafuta kidogo mengine anapaka kwenye mfuniko ili unukie a aenda kuuza mnadani sasa ole wako akufate ukatae kununua ,kipigo chake utakoma inabidi ununue hivyo hivyo

Ila kunakipindi alimuuzia mtu wa kutoka mbali jamaa alipigwa juujuu tumbo likajaa maji likikuwa kubwa kuzidi mama mwenye ujauzito wa miezi 9 , sijui alitafuta dawa gani siku hiyo yuko buchani anajikatia nyama ,alianguka chini maji kama nusu pipa yalitoka tumboni kupitia kitovuni ndio akarudi sawa

Jamaa alikuwa hana mkee ila akitaka mkee wa mtu anaenda hadi anapokaa anakwambia baba fulani leo mkee wako mwabie usiku namtaka nyumbani kwangu itabidi usiku wewe ndio umsindikize mkeo na asubuh umfate bila hivyo utakiona cha mtema kuni

Baada ya manyanyaso ya huyu 'mzee mtoto ' kuzidi ikabidi mwenyekiti aandae kikao cha kijiji watu watoe malalamiko na vijana nijinsi gani watajiunga kumidhibiti huyu jamaa, kwani nguvu alizokuwa nazo zilikuwa zaajabu maana watu walikuwa wanadai amezaliwa na mfupa mmoja.

Kumbe siku ya kikao kuna snichi alienda akatoa siri kwa mzee mtoto kuwa kunakikao kinaedelea kukuhusu wewe. Jamaa akabidi atoe panga yake akamchukua yule snichi mpaka kwenye mishamba ya mipera wakaenda wakakata fimbo za kutosha ,wakati bado mwenyekiti hajamaliza kuutubia tukashangaa mzee mtoto na yule snichi wamefika kwenye kikao lundo la fimbo

Daa raia wakaanza kupagawa jamaa akasema mtu hata mmoja asinyanyuke alipokaa kama anataka usalama wake ,akamwabia mwenyekiti naanza na wewe lala chini mwenyeki bila hata kijitetea na wajumbe waliokuwa pale ikabidi wainame, tembezewa bakola za kufa mtu alvyomaliza akawaambia pigeni magoti hapo.

Kisha akageukia raia akaanza tembeza fimbo tano tano za moto wakati bado zoezi la utandikaji linaendelea akaona mwanamke mkali alikuwa amekuja na bwana ake, akamwabia naomba wewe dada nikukute nyumbani kwangu chumbani ukiwa hauna nguo hata moja yule dada ikabidi atimke kuelekea kwa mshikaji

Baada ya zoezi kuisha ikabidi amwabie mwenyekiti waandike wote majina kesho asubuhi wote uwapangie kazi kwenye mashamba yangu

Ila jamaa alikuja kugeukwa na wezi wenzake baada ya kuwa anashirikiana na majambazi wa mifugo kutoka sehemu za mbali anawachorea ramani, walikuja kugeukana akapigwa akaoza ndani kwa ndani alikaa ndani hana rafiki hakuna wakumuona raia kwenda kuchunguza wanakuta mwili umesha ozeana na kuoza kabisa.

Kama wewe pia mdau umeshakutana na wababe wa namna hii usiache kutoa comments hapo chini
 
Mzee mtoto alikula sana maisha, kazi yake ilikua ni kupoint tu demu anaemuona ni mkali halafu usiku anamkuta gheto akiwa tayari yupo kitandani ameshavua barakoa.
 
Dah ni nouma ilikuwa mkoa gani hii Kaka?. Na miaka gani?
 
Yani icho kijiji ni mapoyoyo wameshindwa kumuwinda na mikuki au kuchanga hela kwenda kumtafuta mtaalam mbali huko am fix
 
Chai ya tangawizi nyingi na limao inafaa sana kipindi hiki cha corona
 
Back
Top Bottom