Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Kama umeyasoma na ni yake tuwekee nukuu japo moja, mbili, tatu.
Kinakushinda nini kufanya hivyo?
Maalim Faiza,
Kinachonistaajabisha mimi ni hiki.

Hivi wanataka tuiondoe historia hii ibaki ile yao rasmi au wanataka nini?

Historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni iko toka mwaka wa 1981 na ikisomwa bila tatizo.

Hakutokea hata mtu mmoja kuipinga.

Sasa kwa hili siwezi kuwalaumu kwa kuwa walikuwa hawajaijua historia ya kweli.

Ajabu ni kuwa pale nilipoandika historia ya kweli na ikasomwa ingetegemewa ingepokelewa kwa furaha kuwa sasa historia ya kweli imepatikana.

Badala ya kushukuru kuwa historia imerekebishwa wao hawaitaki na wanaanza kuipiga mawe.

Hofu ya hawa ni sawa na hofu ile ya Kivukoni walioletewa ''notes,'' za Abdul Sykes za historia ya TANU wakaogopa kuzipokea wakidai ati historia ya TANU haina uhusiano na Abdul Sykes.

Kuna mtafiti wa historia ya TANU atakaeweza kuandika historia hiyo bila kumtaja Abdul Sykes?

Tofauti na hawa vyuo vikuu nje ya Tanzania walipoisoma historia hii kitu cha kwanza kilichogonga akili zao ni kuwa inawezekanaje kwa miaka yote hiyo historia hii haikufahamika?

Wakataka sasa kumjua mtafiti na mwandishi wa historia hii na wakataka kuonana na yeye uso kwa macho.

Hapa wanashughulishwa na kuishambulia.

Bahati kuna ushahidi wa nyaraka na picha sijui ingekuwaje endapo vitu hivi vingekuwa havipo?

Angalau Prof. Shivji na jopo lake wamekuja kunihoji na nimewapa picha na nyaraka na wamezithibitisha kuwa hakika ni za kweli kwani wamepata kuzionyesha katika Kavazi la Mwalimu Nyerere.
 
lukubuzo Samsis,

Mtu asiye na hoja hutanguliza matusi, jibu swali acha Viroja. Nyerere 1945 hata Edinbrugh hajaenda, hakuwepo Manchester conference walokuwepo wanafahamika. Ukweli ni Nyerere hakuwepo Manchester Pan Africanism Congress.
 
Mtu asiye na hoja hutanguliza matusi,jibu swali acha Viroja.Nyerere 1945 hata Edinbrugh hajaenda ,hakuwepo Manchester conference walokuwepo wanafahamika , kadirio la,tukana ,jinyonge etc ila ukweli ni Nyerere hakuwepo Manchester Pan Africanism Congress.

Kuwepo huko ndio nini nini kwa mfano mkuu???
 
Azarel,

Umejitungia habari zako na kujitoa ufahamu ukajitia kucheka. Kwa taarifa yako mimi ni muumini wa ukweli siyo mtu wa kutukuza uongo na habari za kuzusha.

Kwa hiyo unataka kusema kila jambo nchi kafanya Nyerere peke yake na kila akataaye uongo huo basi ni mtu wa Pwani na mfuasi?
 
Umejitungia habari zako na kujitoa ufahamu ukajitia kucheka. Kwa taarifa yako mimi ni muumini wa ukweli siyo mtu wa kutukuza uongo na habari za kuzusha.

Kwa hiyo unataka kusema kila jambo nchi kafanya Nyerere peke yake na kila akataaye uongo huo basi ni mtu wa Pwani na mfuasi?
Ni nani amesema Nyerere alifanya kila kitu?

Mbona unanilisha maneno? Au huelewi?

Nimekuuliza wakati Nyerere anadominate kwny political sphere ya Tanganyika mpaka Tanzania...hao Waislam wa pwani walikuwa wapi? walifanya nini mpaka leo mumlaumu?

Jibu kinagaubaga.
 
Ni nani amesema Nyerere alifanya kila kitu?

Mbona unanilisha maneno? Au huelewi?

Nimekuuliza wakati Nyerere anadominate kwny political sphere ya Tanganyika mpaka Tanzania...hao Waislam wa pwani walikuwa wapi? walifanya nini mpaka leo mumlaumu?

Jibu kinagaubaga.
Umeelezwa fitina alizozifanya Nyerere na serikali yake, umeambiwa na kwa ushahidi alivyouwa jumuiya ya waislamu na kuunda Bakwata kwa gilba, umeonyeshwa kilichowakuta kina Sukwa Said Sukwa na Bibi Titi,umeonyeshwa masaibu ya mufti Hemed bin Ameir na Kina sheikh Takadiri.

Uambiwe nini zaidi? Mimi sisemi haya kwa kuwa ni mtu wa Pwani na ni muislamu la hasha,mimi ni mtu wa bara na ni mkiristo. Mtu akiandika mchango wa waislam hazuii mwingine kuandika kuhusu Wakristu, Wabudha ,Wahindu na wale wa dini ya asili, andikeni.Tusifungwe na minyororo ya udikteta uchwara.
 
Umeelezwa fitina alizozifanya Nyerere na serikali yake, umeambiwa na kwa ushahidi alivyouwa jumuiya ya waislamu na kuunda Bakwata kwa gilba,umeonyeshwa kilichowakuta kina Sukwa Said Sukwa na Bibi Titi,umeonyeshwa masaibu ya mufti Hemed bin Ameir na Kina sheikh Takadiri.

Uambiwe nini zaidi? Mimi sisemi haya kwa kuwa ni mtu wa Pwani na ni muislamu la hasha, mimi ni mtu wa bara na ni mkiristo.Mtu akiandika mchango wa waislam slamu hazuii mwingine kuandika kuhusu Wakristu, Wabudha, Wahindu na wale wa dini ya asili, andikeni. Tusifungwe na minyororo ya udikteta uchwara.
Mtasema sana ila atabakia kutambulika JK the Almighty kelele za chura tu hizi
 
Katika mpira hasa wa miguu anyehangaika sana kuutafuta mpira, kupigwa kiatu na kuumizwa lengo lake likiwa ni kumpasia mwenzake ili afunge goli na kwa urahisi kabisa, mchezaji atakayefunga goli ndiye shujaa na ndiye atakayeshangiliwa na watazamaji, wachezaji wenzake hata na mtoa pasi ya mwisho.

Bila kuwabeza wale waliopata taabu na masumbuko mengi na hata wengine umauti ukawapata wakati wakiwa kwenye harakati za kutafuta uhuru lakini mwisho wa siku hakuna katika hao wote atakayemzidi Nyerere kwa umaarufu na umuhimu katika kuleta Uhuru wa Tanganyika.

Tulipigana Vita na Uganda tukashinda.
Aliyepata sifa kuliko wote ni Amiri Jeshi mkuu ambaye alikuwa ni Nyerere.
Hapa Nyerere hakwenda mstari wa mbele wala hakushika bunduki lakini ndiye aliyekuwa anaratibu mapigano akisaidiana na makamanda wa Jeshi.

Kosa kubwa wanalofanya ndugu zetu Waislamu ni kuchanganya matendo yanayotokana na utashi wa mtu na Maandiko matakatifu ya Koran. Wao kila jambo analofanya Muislamu hata kama ni la kijinga na ni ovu na linaleta maangamizi wao huliunga mkono.

Nimechunguza sana hili la kugundua kuwa wengi wanaounga mkono kila jambo linalofanywa na Mwislamu hata kama linapingana na Koran Tukufu, elimu yao ni ndogo sana na kwa hiyo wana upeo mdogo wa kutambua mema na mabaya.

Ndugu zangu Waislamu wenye elimu ndogo somesheni watoto wenu wa kike na kiume elimu ya juu ili wapate wigo mpana wa kuelewa mambo.

Mapadre wa Kikatoliki katika Syllabus yao kuna topic inayohusu elimu ya Koran Tukufu na yeyote ambaye hatafaulu somo hilo hatapata Upadre. Lengo kubwa si kuijua Koran Tukufu na kuanza kuikashifu, bali ni kupata elimu nzuri iliyoandkikwa mle na kuwapa uwezo mpana wa kueneza neno la Mungu kwa watu wote.

Ndani ya vitabu vitakatifu hapajaandikwa matusi, ubaguzi, chuki, uchochezi bali jambo kubwa ni moja tu - upendo.
 
Katika mpira hasa wa miguu anyehangaika sana kuutafuta mpira, kupigwa kiatu na kuumizwa lengo lake likiwa ni kumpasia mwenzake ili afunge goli na kwa urahisi kabisa, mchezaji atakayefunga goli ndiye shujaa na ndiye atakayeshangiliwa na watazamaji, wachezaji wenzake hata na mtoa pasi ya mwisho.
Bila kuwabeza wale waliopata taabu na masumbuko mengi na hata wengine umauti ukawapata wakati wakiwa kwenye harakati za kutafuta uhuru lakini mwisho wa siku hakuna katika hao wote atakayemzidi Nyerere kwa umaarufu na umuhimu katika kuleta Uhuru wa Tanganyika.
Tulipigana Vita na Uganda tukashinda.
Aliyepata sifa kuliko wote ni Amiri Jeshi mkuu ambaye alikuwa ni Nyerere.
Hapa Nyerere hakuenda mstari wa mbele wala hakushika bunduki lakini ndiye aliyekuwa anaratibu mapigano akisaidiana na makamanda wa Jeshi.
Kosa kubwa wanalofanya ndugu zetu Waislamu ni kuchanganya matendo yanayotokana na utashi wa mtu na Maandiko matakatifu ya Koran. Wao kila jambo analofanya Mwisilamu hata kama ni la kijinga na ni ovu na linaleta maangamizi wao huliunga mkono.
Nimechunguza sana hili la kugundua kuwa wengi wanaounga mkono kila jambo linalofanywa na Mwislamu hata kama linapingana na Koran tukufu, elimu yao ni ndogo sana na kwa hiyo wanaupeo mdogo wa kutambua mema na mabaya.
Ndugu zangu Waislamu wenye elimu ndogo somesheni watoto wenu wa kike na kiume elimu ya juu ili wapate wigo mpana wa kuelewa mambo.
Mapadre wa Kikatoliki katika Syllabus yao kuna topic inayohusu elimu ya Koran tukufu na yeyote ambaye hatafaulu somo hilo hatapata Upadre. Lengo kubwa si kuijua Koran tukufu na kuanza kuikashifu mbali ni kupata elimu nzuri iliyoandkikwa mle na kuwapa uwezo mpana wa kueneza neon la Mungu kwa watu wote.
Ndani ya vitabu vitakatifu hapajaandikwa matusi, ubaguzi, chuki, uchochezi bali jambo kubwa ni moja tu upendo.
Njolo,
Umeandika: ''Bila kuwabeza wale waliopata taabu na masumbuko mengi na hata wengine umauti ukawapata wakati wakiwa kwenye harakati za kutafuta uhuru lakini mwisho wa siku hakuna katika hao wote atakayemzidi Nyerere kwa umaarufu na umuhimu katika kuleta Uhuru wa Tanganyika.''

Umesema kweli.

Mchango wa Mwalimu Nyerere katika historia ya TANU na kupigania uhuru hauna mfanowe kabisa.

Mimi sikuandika kitabu cha historia ya TANU kupinga mchango wa Mwalimu Nyerere.

Kitabu nimeandika ili kuikamilisha historia hiyo kwa kueleza mengi ambayo hayakuwa yanajulikana kuhusu wengi waliokuwa katika harakati hizo kabla na wengine pamoja na Mwalimu.

Historia hii ndiyo iliyokuwa imepotezwa.
Hii mosi.

Pili tatizo si kuwa Waislam hawapeleki watoto wao shule.

Tatizo ni kuwa kuna mfumo uliojengwa kwa miaka mingi ya kuwazuia Waislam wasielemike.
 
Uhuru wa nchi hii umepiganiwa na waislam, iko wazi, kuanzia Mkwawa, Isike mwana Kiyungi, Vita vya Maji Maji, Abushiri na Bwana Kheri ndiyo waliokuwa wakazi wa mjini. Kipindi hicho mzungu bado anahangaika kubatiza watu kwa peremende, masweta na chupi za mtumba.
 
Elimu kwenu ni anasa ndio maana mlitolewa kwenye reli
Ile taasisi ya Waislam (EAMWS) ilijenga shule, na ilikua mbioni kujenga university (pale jirani Uwanja wa Taifa) lakini nyerere akaivuruga na kuivunja, angeiacha usingekua unazungumza huo upuuzi wa elimu ni anasa; ndiyo maana Waislam wanamuona Nyerere kama wakala wa Kanisa. Sheikh Takadir aliona dalili mapema akawaonya waislam, wakampuuza, akawaambia mtatawaliwa nyinyi na vizazi vyenu miaka mia, Waislam kuwa nyuma kielimu Tanzania unaweza hisi kuna mkono wa Mwalimu.
 
ile taasisi ya waislam(EAMWS) ilijenga shule,na ilikua mbioni kujenga university(pale jirani uwanja wa taifa),lakini nyerere akaivuruga na kuivunja,angeiacha usingekua unazungumza huo upuuzi wa elimu ni anasa,ndiyo maana waislam wanamuona nyerere kama wakala wa kanisa,sheikh takadir aliona dalili mapema akawaonya waislam,wakampuuza,akawaambia mtatawaliwa nyinyi na vizazi vyenu miaka mia,waislam kuwa nyuma kielimu Tanzania unaweza hisi kuna mkono wa mwalimu
Acha utani mkuu yaani shule muache nyie kwenda afu useme kuna mkono wa mwalimu..
 
Acha utani mkuu yaani shule muache nyie kwenda afu useme kuna mkono wa mwalimu..
Mwaka 1997-98, mkoa wa Dar, watoto shule ya msingi (darasa la 7), Waislam walikua 75%,wengine 25%, waliofaulu wengine 75%,waislam 25%, lilisemwa na Kitwana Kondo bungeni. Kipindi hicho Waziri wa Elimu Prof. Kapuya,1998 mitihani ya form 4 ilivuja kwa kiwango ambacho hakikuwahi tokea, 2000 Kapuya akapoteza Wizara ya Elimu, Kitwana Kondo akapoteza jimbo la Kigamboni, likaenda CUF.
 
Mwaka 1997-98,mkoa wa dar,watoto shule ya msingi(darasa la 7),waislam walikua 75%,wengine 25%,waliofaulu wengine 75%,waislam 25%,lilisemwa na kitwana kondo bungeni,kipindi hicho waziri wa elimu prof kapuya,1998 mitihani ya form 4 ilivuja kwa kiwango ambacho hakikuwahi tokea,2000 kapuya akapoteza wizara ya elimu,kitwana kondo akapoteza jimbola kigamboni,likaenda CUF
Kwanini huko visiwani kunaongoza kwa kufeli.?
 
Back
Top Bottom