Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,900
- 30,235
Maalim Faiza,Kama umeyasoma na ni yake tuwekee nukuu japo moja, mbili, tatu.
Kinakushinda nini kufanya hivyo?
Kinachonistaajabisha mimi ni hiki.
Hivi wanataka tuiondoe historia hii ibaki ile yao rasmi au wanataka nini?
Historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni iko toka mwaka wa 1981 na ikisomwa bila tatizo.
Hakutokea hata mtu mmoja kuipinga.
Sasa kwa hili siwezi kuwalaumu kwa kuwa walikuwa hawajaijua historia ya kweli.
Ajabu ni kuwa pale nilipoandika historia ya kweli na ikasomwa ingetegemewa ingepokelewa kwa furaha kuwa sasa historia ya kweli imepatikana.
Badala ya kushukuru kuwa historia imerekebishwa wao hawaitaki na wanaanza kuipiga mawe.
Hofu ya hawa ni sawa na hofu ile ya Kivukoni walioletewa ''notes,'' za Abdul Sykes za historia ya TANU wakaogopa kuzipokea wakidai ati historia ya TANU haina uhusiano na Abdul Sykes.
Kuna mtafiti wa historia ya TANU atakaeweza kuandika historia hiyo bila kumtaja Abdul Sykes?
Tofauti na hawa vyuo vikuu nje ya Tanzania walipoisoma historia hii kitu cha kwanza kilichogonga akili zao ni kuwa inawezekanaje kwa miaka yote hiyo historia hii haikufahamika?
Wakataka sasa kumjua mtafiti na mwandishi wa historia hii na wakataka kuonana na yeye uso kwa macho.
Hapa wanashughulishwa na kuishambulia.
Bahati kuna ushahidi wa nyaraka na picha sijui ingekuwaje endapo vitu hivi vingekuwa havipo?
Angalau Prof. Shivji na jopo lake wamekuja kunihoji na nimewapa picha na nyaraka na wamezithibitisha kuwa hakika ni za kweli kwani wamepata kuzionyesha katika Kavazi la Mwalimu Nyerere.