Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Naamini Mwalimu Nyerere alikuwa mmoja wa watanzania wenye uwezo mkubwa wa akili

Just imagine kijana kutoka mwitongo,butiama huko mara kaja dar kawapinga kawaperemba ma-alwatan wa mji ,na vibopa wa kariakoo mpaka wakaingia line wenyewe halafu akawapiga chenga ya kiakili

Leo hii tunashuhudia vizazo vya wale ma-alwatan na maswahiba wao wanalala Hadi kesho ilhali muhusika mkuu ashatangulia mbele za haki
 
Mazigazi,
Huu ni mjadala mzito hautoweza kujadiliwa kwa lugha kama hiyo yako.
 
Denvers,
Unakusudia kuwasimulia wajukuu stori haya yalikuwa ya zamani sana.
Miaka hii TV imehodhi kila kitu.
Mimi niko tofauti..natamani sana ningekuwa na babu wa kunisimulia stori za zamani. Nachoka kusoma .
 
Mimi niko tofauti..natamani sana ningekuwa na babu wa kunisimulia stori za zamani. Nachoka kusoma .
Denvers,
Mimi ni ''scholar,'' si babu wa kusimulia wajukuu hadithi na hata kama ningetaka sina hadithi za kusimulia nimeandika vitabu na ''academic papers.''
 
Hakuna uhuru unaopiganiwa na kuletwa na mtu 'mmoja'

Denvers,
Ahsante kwa fikra zako.

Kama unaona kuandika historia nilikofanya mimi kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni "mahaba" ya "udini,"mimi sina tatizo na hilo kwani yawezekana walioandika historia ya uhuru wakafuta mchango wa wazalendo wengi tu walifanya hivyo kwa kusukumwa na mahaba ya dini yao.

Muhimu na kubwa sana kwangu ni kueleza ule ukweli wa historia yenyewe kama ilivyokuwa.

Nashukuru sana kuwa azma hii nimeitimiza na historia ya uhuru wa Tanganyika sasa inafahamika na inasomeshwa vyuoni Ulaya na Marekani na kwengineko kwa usahihi wake.

Hayo mengine sina haja ya kuyasemea nawaachia wasomaji watumie akili zao kutafakari na kupata majibu.
 
Mwarabu alikuja mwanzo Afrika mashariki ,bila ya kutumia mtutu wa bunduki.

Mzungu alikuja baadae na alitumia mabavu na kumwaga damu za wenyeji kwa wingi, na baadae akaanzisha biashara ya Utumwa ambayo wote walishiriki, hatimae kutufanya koloni.

sasa vita vya kugombea uhuru vya Maji Maji, Waafrika na Waarabu walishirikiana kumuondoa Mjerumani.

Tumeoni kitu hapa?
 
Mzee wangu, mtume Muhammad (s.a.w.) asema hawatakua radhi mayahudi na manasara mpk mufate mira zao, sasa basi walipokataa kufata mira zao ndio ata kwenye history hawakuandikwa nashukuru allah leo hii umeleta history ya kwel baada ya ile ambayo tulipotoshwa nayo, hongera mzee wangu hongera sn na Allah akuifadhi, waacha wakuite unaudini na maneno kibao kwani walimwengu ndivyo walivyo
Denvers,
Ahsante kwa fikra zako.

Kama unaona kuandika historia nilikofanya mimi kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni "mahaba" ya "udini,"mimi sina tatizo na hilo kwani yawezekana walioandika historia ya uhuru wakafuta mchango wa wazalendo wengi tu walifanya hivyo kwa kusukumwa na mahaba ya dini yao.

Muhimu na kubwa sana kwangu ni kueleza ule ukweli wa historia yenyewe kama ilivyokuwa.

Nashukuru sana kuwa azma hii nimeitimiza na historia ya uhuru wa Tanganyika sasa inafahamika na inasomeshwa vyuoni Ulaya na Marekani na kwengineko kwa usahihi wake.

Hayo mengine sina haja ya kuyasemea nawaachia wasomaji watumie akili zao kutafakari na kupata majibu.
 
Hivi mbonai George Washington ambaye ndiye baba wa Taifa USA alikuwa anavuma sana,? mbona yeye alikuwa anavuma na General Nathanael Greene hajulikani kabisa?

Mkuu Marekani ina founding fathers na sio founding father. Gen Washington ni mmoja wao ila huwezi kueleza uhuru wa marekani ukamtoa mtu kama Ben Franklin au Hamiliton Secretary wa kwanza wa treasury na kwa heshima wote wapo kwenya Pesa yao.

Hata Rais wa tatu Thomas Jefferson ni Baba wa Taifa lao na kuna John Adam Makamu wa kwanza na Rais wa pili wa US. Tukubali tu kuwa Historia yetu imekuwa manipulated na imeamua kwa kila hali kumfanya Nyerere aonekane ndio kila kitu imewasahau figure keys wengi tu, mtu kama Kambona leo hatumsomi kabisa vitabuni.
 
Kabla ya hilo kundi kudai uhuru watu walikuwa wanafurahia kunyonywa..., Tangia muarabu aanze kuja kuuza ndugu zetu kama watumwa watu walikuwa wananungunika na kugombana kutoka katika hali ya Unyonyaji.., Mjerumani alivyokuja wapo kina Mkwakwa n.k.

Sasa kusema kwamba hilo kundi ndio lilikuwa na wazo la kudai uhuru na Nyerere alikuwa tu pugu anashika chaki.., basi hilo kundi lisingemfuata Nyerere bali lingemfuata jamaa yoyote pale mtaani...,
Kwani utumwa umekwisha duniani?
 
Acha utani mkuu yaani shule muache nyie kwenda afu useme kuna mkono wa mwalimu..
Kiimani tunaamini mungu ndo muweza wa kila jambo.

Kidunia kuna watu wanayo Power ya kubadilisha ukweli kuwa Uongo na Uongo kuwa ukweli.

Eg. Msanii mdogo anaweza kutoa nyimbo Kali ikafunikwa na nyimbo mbovu ya msanii Mkubwa (power)

I mean the reality of historical events are being controlled by power.
 
Kwa mantiki hiyo wamaaanisha nini?
 
Back
Top Bottom