MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,011
- 16,748
Ni ukweli usiopingika kuwa 60% ya wasomi wa miaka ya karibuni walifanikiwa kusoma kwa juhudi za Marehemu Mzee Mkono alipokuwa Mkuu wa Bodi ya Mikopo ambaye binafsi alihakikisha hakuna mtoto wa masikini hasomi na ndiyo maana kuna muda aliweza hata kutoa pesa zake mfukoni ili wanafunzi walipwe na wakasome.
Vile vile kwa wakazi wengi wa kawaida (hasa wa Mkoa wa Dar es Salaam) tutamkumbuka Marehemu Mzee Mkono ambaye alipenda sana kujichanganya na watu wa kawaida (masikini) huku yeye akijijua ni tajiri huku akihakikisha anawasaidia ama kwa kipato (pesa) au kuwatafutia fursa za kitaaluma (elimu) na ajira (kazi).
Moja ya wema wake Marehemu Mzee Mkono alioufanya na MINOCYCLINE kuushuhudia ni pale alipoamua kumjengea nyumba mbili mmoja wa Shamba Boi wake wa muda mrefu aliyewashuhudia hata akina Leah (watoto wa Marehemu wakizaliwa) aitwae Makavu ambaye nasikia kuwa sasa ni marehemu (alishafariki) na kumpa fedha za kuanzisha mradi baada ya kuwa Mzee.
Mkono alikuwa ni Tajiri asiye Mchoyo, Mjivuni na hakuwa na Dharau kama walivyo 90% ya Matajiri wa Kitanzania.
R.I.P Mzee Nimrod Elirehema Mkono.