Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

"Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli," alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika. Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha, kuhubiri amani na kuiishi. Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape, Wasira, Kamani, Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu, busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu. Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA, you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!

 
Last edited by a moderator:
Heeeee, Heeee ni tuna masikitiko makubwa kwa kauli ya MATUSI aliyotoa Mh. Rais mstaafu Ben Mkapa jana katika uzinduzi wa kampeni kwa chama tawala (CCM). Alisema wapinzani ni WAPUMBAVU na akarudia ni WAPUMBAVU SANA.

Sasa kwa masharti yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya kutotoa kauli za kuudhi wala kashfa huyu naye mbona alikiuka?

Mzee Mkapa iga mfano kwa Rais mstaafu mwenzio Mzee Mwinyi alivyotoa hotuba ya busara.

Kwa wadhifa wako hukupaswa kutukana kabisa, kwa hapo Mh umekididimiza chama.

Sasa sisi wananchi ni jukumu letu tarehe 25 Octoba,2015 kuondokana na watu wa chama kile kile miaka yoooote toka uhuru ambao hawana lugha nzuri kwa kizazi kijacho.

Jamaaaaaaniii eeeee akili kumkichwa, Oct, 25
 
Heshima yenu wanabodi!

Nimesikitishwa sana na kitendo cha Rais wa tatu wa Tanzania Mh.Benjamin Mkapa kuporomosha matusi jukwaani badala ya kujenga hoja!

Mkapa amekuwa mtu wa kupanic sana tangu alipokuwa Rais,aliwatukana waandishi wa habari wa Tanzania hadharani na kuwaita wasiofaa huku akiwakumbatia waandishi wa nje.

Wakati wa kampeni za ubunge jimbo la arumeru mashariki Mkapa pia aliporomosha matusi kwa wapinzani badala ya kujenga hoja matokeo yake Chadema ilishinda asubuhi na yeye kukimbilia uwanja wa ndege na kuondoka mapema sana asubuhi!

Mkapa amerudia kuporomosha matusi jana kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM na kuwaita watu malofa na wapumbavu! Hivi mh.Mkapa pamoja na kukaa ikulu miaka kumi anashindwa kujenga hoja kweli na anaamua kutumia matusi kama sehemu ya kampeni kweli?

Wapinzani fanyeni kampeni ya kistaarabu acheni kujibu matusi ya Mkapa,waelezeni watanzania mtawafanyia nini mkipewa ridhaa,wananchi wanataka maendeleo sio matusi!

Kila la heri UKAWA kila la heri Lowassa na maalimu Seif.
 
Punda akikaribia kufa huwa anarusha mateke sana. Tumsamehe mzee mkapa hali ya chama chetu ccm si nzuri. Watanzania tuombeeni jamani wenzenu.
 
Duuu, haki ya Mungu siasa mchezo mchafu kweli.

Yani ufunguzi wa kampeni zote za jana jambo ambalo limebeba bango ni maneno ya Rais mstaafu Mkapa.

Sasa hivi nashika kusema Mkapa kusema vile ni moja ya mbinu za kisiasa kuwapumbaza watu wasione madhaifu mengine. Mimi nimeangalia karibuni tukio zima kulikuwa kuna mapungufu mengi tu lakini watu hata hawazungumzi.

Sasa hivi nimeona post ya Lowassa facebook na yeye habari ni hiyo tu tumetukanwa.

Siasa mchezo mchafu kweli
 
Wana JF Heshima kwenu.

Mithali 26:5
Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

Aidha neno upumbavu limeandikwa zaidi ya mara 46 katika Biblia. Mfano :-

Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.

Aidha Rais wa kwanza wa TZ; Mwl Nyerere amekuwa akitumia neno hili mara nyingi sana. Huko ndiko Mhe. MKAPA alipojifunzia. (Nimeshindwa kuweka video clip msaada plz)

Mhe. Sugu alipotumia neno mpumbavu pale mjengoni UKAWA walimtetea. Leo kwao limetumika imekuwa nongwa kwenye mitandao. Kweli nyani haoni naniii yake.

Mhe. Mkapa ni Mkristo mzuri mwenye kusoma Neno la Mungu kila wakati. Alichofanya ni kujibu hoja ambayo ameipima na kuiona ni ya kipumbavu ili walioitoa wasijione wana akili.

Nani asiyejua Mhe. Sumaye alibatizwa jina la utani la ZIRO!!! Kwanini mlimuita hivyo na Kipanya alichora katuni nyingi za ZIRO. Mhe. Mkapa anamjua sana Mhe. Sumaye. Hivyo amemjibu SAWASAWA na UPUMBAVU wake. Mbona wanawake tunapohubiriwa tusiwe wapumbavu hawasemi wametukanwa?

Hakuna shida hapo, message sent and delivered.

Queen Esther
 
Naomba ni Quote part ya speech ya Major C.A Bach iliyotolewa kwa maofficer wanafunzi katika kambi ya pili ya mafunzo Fort Sheridan wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia,kwaajili tu ya viongozi wa CCM.

"Moral force is the third element in gaining Moral Ascendency.To exert moral force you must live clean; you must have sufficient brain power to see the right and the will to do the right.Be an example to your men! An officer can be a power for good or a power for evil.Don't preach to them~ that will be worse than useless.Live the kind of life you would have them lead, and you will be suprised to see the number that will imitate you.

A loud~mouthed, profane captain who is careless of his personal appearance will have a loud~mouthed,profane ,dirty company .Remember what I tell you .Your company will be the reflection of yourself!"
 
Akina makonda wakajifunze wapi adabu kama wazeee wao wote ni wakosa adabu , nimeshangazwa sana na mtu huyu ambaye alishika dhamana ya juu kabisa ya nchi hii.
 
Duuu, haki ya Mungu siasa mchezo mchafu kweli.

Yani ufunguzi wa kampeni zote za jana jambo ambalo limebeba bango ni maneno ya Rais mstaafu Mkapa.
Sasa hivi nashika kusema Mkapa kusema vile ni moja ya mbinu za kisiasa kuwapumbaza watu wasione madhaifu mengine. Mimi nimeangalia karibuni tukio zima kulikuwa kuna mapungufu mengi tu lakini watu hata hawazungumzi. Sasa hivi nimeona post ya Lowassa facebook na yeye habari ni hiyo tu tumetukanwa.

Siasa mchezo mchafu kweli
Kwavile muanzisha uzi hajasema watu wasieleze mapungu mengine uliyoyaona, ni vema basi nawe ukayaorodhesha hayo mengine kinyaa
 
Last edited by a moderator:
CCM walikuwa wanazindua matusi na fiester wala si ilani kama tulivyotegemea maana mimi sijasikia cha muhimu kutoka kwenye ilani
 
Back
Top Bottom