Mzee Mkapa kasema "CCM inajiona bado iko kwenye monoparty system na sio multiparty system”

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,315
15,062
Wakuu

Ukitafakari hayo maneno, utagundua matendo ya CCM yanawachukiza baadhi ya wastaarabu.
Ukiangalia jinsi CCM inavofanya siasa zake kiukweli bado wako nyuma sana kwani bado wanaamini ukomonisti wa miaka ya kutafuta uhuru wa kisiasa.

Dunia sasa inapambana kutafuta uhuru wa kiuchumi, maana nchi nyingi walishamaliza kujenga shule za msingi, miundombinu mataifa mengi yalimaliza muda mrefu. Ukiangalia political popularity ambazo viongozi wanafanya ili watawale kisiasa utaona huruma.

Mzee kawakumbusha kua dunia imehama mnakofikiria, waacheni na wengine wafanye siasa kwani tofauti na hapo itakua mbaya sana baadae. Mtajikuta mmeiingiza nchi kwenye hata vita kwa kulazimisha watu wakubali chama chenu wakati kila mmoja anahaki ya kua chama chochote anachopenda na ni takwa la kikatiba.
 
Mkapa ana ustaarabu upi? Huyu alipaswa kupelekwa The Hugue kwenda kujibu kesi ya mauwaji ya Wazañzibar.

Na usisahau huyu ndiye aliyewaita Watanzania wenzake kwamba ni wapumbavu na malofa.

Hivi Watanzania ni wasahaulifu kiasi hiki?
 
Ukisikia ule msemo wa "Rungu kapewa kichaa......" utaona unavyo randana na CCM jinsi inavyotawala. Kila lililo mbele yao wao kazi yao ni kutembeza rungu tu. Hata ustarabu wa kawaida wameuweka kando na bado wanakenua tu mchana kweupe.
 
Matola,

Stori ya shimoni inasikitisha sana,walikufa wengi. Ila hawa wakubwa huwa wanakuja kuteseka sana wakishastaafu. Tony Blair ilimtesa akatoka na kuomba radhi kuhusu Iraq,Obama naye uvamizi wa Libya. Kuna kitu inaitwa GUILTY CONSCIOUS,acha kabisa,unaweza kutamani ufe lakini hufi.
 
Inabidi member wa ccm watahiri akili zao, naona kama kuna screw kichwani ziko loose. Hivi yawezekana vipi mtawale kwa miaka yote hiyo huku baadhi ya shule hazina waalimu wa kutosha? unapewa microphone unaanza kujimwagia masifa ya hovyo?. Nchi hii inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom