Mzee Mkapa awasilisha salamu za Rais Magufuli kumuaga Mzee Moi, asema alikuwa 'mentor' wake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,873
Rais mstaafu mzee Mkapa amesoma salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Magufuli katika msiba wa Mzee Moi.

Mzee Mkapa amesema yeye binafsi amefanya kazi na Mzee Moi kwa miaka 7, akiwa na Rais na mzee Kikwete aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Mkapa amesema Rais Magufuli amewatuma wao wawili kama ishara ya upendo na ushirikiano wa kindugu kati ya nchi zetu mbili.

=======

Akitoa salamu hizo, Mzee Mkapa amesema:

“Rais wangu Dkt. John Joseph Magufuli, kwa dhati kabisa ametuleta sisi wawili (na Mzee Kikwete) kuthibitisha ukaribu, undungu na umoja uliopo kati ya nchi zetu mbili”

“Nimekuwa Rais kwa miaka 10. Katika miaka hiyo 10, miaka 7 nilikuwa nafanya kazi na Rais Moi. Kwahivyo, kama alivyosema Dkt. Ruto, pamoja na kwamba ni mzee wetu, lakini kwangu mimi alikuwa ‘mentor’ katika utawala na uongozi. Ndiyo sababu nilisema lazima nije na ku-pay tribute kwa uhusiano huu niliokuwa nao, lakini vilevile kushirikiana nanyi katika kumuombea apumzike mahali pema peponi, kwa Mungu wetu ambaye alimpenda sana”

Mzee Mkapa pia ameambatana na Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ameeleza kumfahamu Mzee Moi tangu yeye (Kikwete) akiwa shule akisoma.

“Nimemfahamu Mzee Moi tangu nikiwa shule, nikisoma habari za Kenya, harakati za kudai uhuru wa Kenya. Baadaye na mimi nilipokuwa katika Serikali, nikiwa Waziri, niliwahi kuja. Nilitumwa na Rais wangu, Rais Ali Hassan Mwinyi nikiwa Waziri wa Nishati na Madini, kuja kuzungumza naye juu ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya katika mradi tuliokuwa tumefikiria kuuanza wa kujenga bomba la gesi kutoka Songosongo kuja Dar es Salaam”

Mkapa at Moi memorial service.PNG

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin W. Mkapa akiwasilisha salamu za rambirambi kwa Wakenya, kwa niaba ya Rais John Magufuli.

Kikwete.PNG

Rais wa Nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu zake kwa Wakenya kufuatia kifo cha Mzee Moi. Kikwete ameeleza mchango mkubwa wa Mzee Moi katika kuimarisha umoja wa wana Afrika Mashariki.

Source: Citizen TV
 
Rais mstaafu mzee Mkapa amesoma salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Magufuli katika msiba wa mzee Moi. Mzee Mkapa amesema yeye binafsi amefanya kazi na mzee Moi kwa miaka 7 akiwa Rais na mzee Kikwete akiwa Waziri wa mambo ya nje.

Mkapa amesema Rais Magufuli amewatuma wao wawili kama ishara ya upendo na ushirikiano wa kindugu kati ya nchi zetu mbili.
Kwa hiyo angeenda Magufuli mwenyewe ingekuwa ishara feki ya upendo na ushirikiano? Labda anajua Wakenya wanakumbuka alivyouza ng'ombe wao!
 
Magufuli sijui kwanini anaogopa sana kusafiri nje ya nchi. pia anaogopa misiba uwa namtafakari nashindwa kuelewa angalia Mugabe, Moi, hajaenda popote.
Tabia ya wafalme wwa zama za kati na za kale; kujifungia ngomeni kwa hofu ya kupinduliwa!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi naona wewe ndiyo unachukulia powa maana haujali hata usalama wa Rais wako. Unadhani mambo haya huwaga yanakwenda kirahisi rahisi tu. Msiwe mnachangia kama hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Yaani wangeenda wote wanne waliopo hai. Lakini kwa sababu hatujui umuhimu wa nguvu yetu hapa EA na duniani JPM anachukulia poa tu na kuwatuma wengine!!

So shameful!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongereni sana wastaafu kwa kuaminiwa na kutumwa kumwakilisha Rais.
Tumia akili, wao wameenda kama viongozi wa zamani, anaye weza kumtuma kwa mamlaka yake kama kiongozi wa Taifa ni makamu wake au Waziri mkuu, labda Mzee Mkapa kwa kutoa aibu ndiyo maana ameamua kukisemea kwamba wametumwa, vinginevyo labda angekuwa mgonjwa.
 
Back
Top Bottom