Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,130
Dunia hivi sasa inaomboleza kifo cha Nelson Madiba Mandela, Rais wa kwanza mwafrika, kutawala nchi ya Afrika ya kusini, mtu ambaye ndiye anayeaminika kuwa, ndiyo binadamu maarufu kuliko yeyote katika watu wote walioishi karne hizi za 20 na 21.
Sifa kubwa anazopewa mzee wetu huyu aliyetutoka siku chache zilizopita, ni namna alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kusamehe watu, hata wale walomfanyia makosa makubwa sana, ambayo katika hali ya ubinadamu wa kawaida ingekuwa vigumu mno kusamehe.
Vile vile mzee wetu huyo alikuwa na sifa kubwa ya kupenda upatanishi, mahali popote ambapo aliona kulikuwa na mafarakano, aidha kati ya mtu na mtu au hata kati ya kundi fulani la jamii na kundi jingine.Vile vile hakupenda kabisa,tabia ya ulipizaji wa visasi.
Hebu jaribu ku-imagine, mzee Mandela alikuwa na moyo wa aina gani, hata baada ya "kubambikiwa" kesi ya uhaini, kwa madai ya kuwa, alipanga njama za kuipindua serikali ya makaburu wa Afrika kusini, wakati katika hali halisi, yeye alichokuwa anakipigania ni kitu kimoja tu, kuwepo hali ya usawa, kati ya raia weupe na weusi ndani ya Afrika kusini.Jambo ambalo lilisababisha mahakama za enzi hizo za kikaburu, kumpata na hatia ya uhaini, na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Watu wengi sana, hasa wazungu makaburu wa Afrika kusini, walikuwa na hofu kubwa sana, baada ya mzee Mandela kutoka jela mwaka 1990, wakidhani kuwa mzee Mandela ataweza kuwalipizia kisasi, hasa atakapochaguliwa na kuwa mwafrika wa kwanza, kuliongoza Taifa hilo, lenye raia waliochanganyika rangi, kati ya weusi walio wengi na weupe walio wachache.
Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti sana na kinyume cha makaburu walivyofikiria, baada ya Mandela kushinda uchaguzi wa vyama vingi, mwaka 1994, na kuliongoza Taifa hilo, lenye nguvu kubwa kiuchumi, kuliko Taifa lolote barani Afrika. Kwani badala ya kulipiza kisasi, hasa ikijulikana yeye wakati huo ndiye aliyekuwa Amiri jeshi mkuu, ambapo vyombo vyote vya ulinzi na usalama, vilikuwa chini yake,lakini mzee huyo hakuwalipizizia kisasi hata chembe "wabaya" wake makaburu, badala yake, wakati wote alikuwa akihubiri maridhiano, na kusameheana kwa yote yaliyopita, na badala yake, akafungua ukurasa mpya, kwa wananchi wa Taifa hilo, ambalo wananchi wake weupe na weusi, walikuwa wanaishi kwa uhasama wa hali ya juu, sasa wakaanza kuishi kwa kuelewana, na kuonyeshana upendo wa hali ya juu!!
Bara hili la Afrika, halijawahi kupata kiongozi, mwenye kujua kusamehe na kuwapenda adui zake, kama ambavyo aliweza kufanya mzee wetu huyo, ambaye dunia nzima, hivi sasa inazizima, kwa kuomboleza kifo chake.
Pamoja na sifa hiyo ya kipekee ya mzee Mandela, kuwasamehe wabaya wake, hata wale waliomfunga jela,kwa miaka 27, kwenye gereza la kutumikishwa kazi ngumu, za kuponda kokoto, gereza la Robben Island, na hata hao waliomfunga kwa "kumbambikia" makosa hayo ya uhaini/ugaidi, bado aliweza kuwasamehe!!
Hata hivyo, lipo eneo moja tu, ambalo mzee Mandela alishindwa kusamehe, na eneo hilo si lingine bali ni lile, alipopata ushahidi wa kutosha kuwa, wakati anatumikia kifungo jela, na hata baada ya kutoka jela, mkewe Winnie, alikuwa "akichapwa" na mwanasheria wao wa familia, jambo ambalo hatimaye, lilimlazimisha mzee wetu huyo, anayeheshimika sana duniani kwa uvumilivu wake, wa mambo makubwa yaliyomkumba maishani mwake, kutoweza kulivumilia hilo, hadi kusababisaha, kumpa talaka mkewe Winnie na kumwoa, mjane wa Samora Matchel, bi Graca Matchel!
Sasa hapo ndipo ninajiuliza, hivi mzee Mandela, hakuwa anaiamini falsafa ya mwanumuziki Richi Maboko, kuwa kuchapiwa ni siri ya ndani, ambapo wana ndoa, wanapaswa kuyamaliza wenyewe ndani, badala ya kuyatoa nje, na kuwapa faida walimwengu, ambao hayawahusu mambo hayo?!!
Naomba wadau, tulitafakari kwa makini suala hili,na kuchangia mawazo chanya.