Mzee Makassy - 'Mungu Kaniita Nimtumikie nifike Kwake Mbinguni' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Makassy - 'Mungu Kaniita Nimtumikie nifike Kwake Mbinguni'

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Apr 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Mzee Makassy - 'Mungu Kaniita Nimtumikie nifike Kwake Mbinguni'

  Kwa wale Vijana ambao walikuwa wamechipukia katika miaka 1963 watakuwa wanamkumbuka vizuri zaidi Kitenzogu Makassy, na Bendi yake ya OCHERSTRA MAKASSY, hata kama ulibahatika kusikia miziki yake miaka ya 1980 unaweza kujua ni nani tunayemuongelea hapa.

  Mwanamuziki Mkongwe ambaye jina lake haliwezi kusahaulika daima, Kitenzogu Makassy alizaliwa mwaka wa 1942 huko Kilumakivu Manyema nchini Kongo zamani Zaire.

  Alianza shughuli za muziki mwaka 1963 hapa nchini muziki wake ulikuwa kwa haraka na kupendwa na watu wengi kutokana na staili yake ya uimbaji ambayo iliwavutia wengi.

  Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa hajishughulishi tena na muziki tayari ameweza kuwa na kitu cha kujivunia katika uhai wake kwani mpaka sasa shughuli zake za muziki amemrithisha mtoto wake aitwaye Junior Makassy ambaye kwa sasa kijana huyo amekuwa maarufu sana hapa jijini Dar es Salaam kwa shughuli za ueMC katika maharusi na sherehe mbalimbli.

  Mzee Makassy hivi sasa hajishughulishi na muziki na aliamua kuokoka hata hivyo mwandishi wa Nifahamishe alipoomba kujua ni dhehebu gani analo anaabudu hakuwa tayari kujibu ila alijibu kuwa waliookoka hawana dhehebu.

  Mzee Makassy alipoulizwa ni albamu gani ambayo mpaka sasa anaikumbuka sana ,Makassy alisema kuwa ana nyimbo nyingi alizozitunga na kuziimba hivyo si rahisi kuzikumbuka zote kwa sasa zote ila kiduchu tu.

  Mnamo mika ya 1982, Mzee Makassy alivuma na albamu ambayo iliwashika vibaya mayanki wa enzi hizo na kufanya awe mmoja wa wakali wa muziki wakati huo na alijiwekea jina kubwa lililoendelea kuheshimika hadi leo.

  Nyimbo zake kama vile, "Mambo Bado", ”Nakolela Cherie" , "Nifa","Siku Yangu" na "Mungu Kaniita" zilivuma sana miaka hiyo na zimeendelea kupigwa maredioni hadi leo.

  Katika kumiliki bendi ya Ochestra Makassy, Mzee Makassy alishirikiana vizuri na wakali wengine akiwemo DK Remmy Ongara ambaye mpaka sasa yupo hai na alistafu shughuli za muziki kutokana na kuugua ugonjwa wa kupooza ambao ulimfanya aamue kuokoka.

  Wengine walioimba na Makasy ni Sega Mtindo ,Tshimanga Assossa, Mose Se Senga ,Maliki na Mbombo wote hao waliufanya muziki upendwe kutoka na kujituma sana jukwaani.

  Pia Mzee Makassy alitabainisha kuwa muziki wa sasa hauna utamu wala ladha kutokana na vijana wa sasa hivi kutojituma.

  Utashangaa mwanamuziki anapanda jukwaani tayari ameishalewa sifa pia upande mwingine hata maadili ya muziki nayo yamemepungua.

  Wakati nikifanya mahojiano na msanii huyo mkongwe pale katika Jengo la BIMA karibu na ofisi za Habari na Maelezo wazee wengi waliomuona Mzee Makasy walikuwa na shauku ya kutaka kujua alipo hivi sasa kwani ni miaka mingi iliyopita hawajawahi kuonekana.

  Mzee Makasy alihitimisha safari yake katika anga ya muziki tangu mwaka 1993 na kuanza shughuli za kumtumikia mungu.
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Na hii nayo ni siasa?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  #2 (permalink) Today, 08:02 PM
  Zakumi
  Zakumi has no status.
  JF Senior Expert Member Join Date: Wed Sep 2008
  Location: Mtoni
  Posts: 902
  Thanks: 482
  Thanked 440 Times in 302 Posts
  Rep Power: 22

  Credits: 1,817,410

  Re: Mzee Makassy - 'Mungu Kaniita Nimtumikie nifike Kwake Mbinguni'

  --------------------------------------------------------------------------------

  Na hii nayo ni siasa?

  hapana ni """"""""""""""""HISABATI"""""""""""""""""""""""""""
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tumika mzee Makasi, lakini Kumbuka Mungu hututaka tumtumikie siku za ujana wetu tukingali bado tuna nguvu!
   
Loading...