#COVID19 Mzee Makamba: Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki. Lazima wajue uhuru wao unaishia Bungeni

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
51,961
41,438
Mzee Makamba anasema Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki ndani ya CCM kwakuwa wamekuwa wamekuwa wakipingana na Serikali hasa kwenye swala hili la chanjo.

Mzee Makamba anasema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakimdharau sana Rais samia hivyo ametaka washughulikiwe mara moja.

Mzee Makamba anasema yeye si msemaji wa CCM lakini anashangaa ukimya wa baadhi ya Wana CCM na viongozi wa CCM hasa katika hali ya Rais kuonekana ana dharauliwa na baadhi ya wana CCM.

Mzee Makamba ametaka wana CCM kuwachukulia hatua Gwajima na Pole pole.. kwani hawavumiliki.

=====

BAADHI ya viongozi waandamizi ndani ya chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, wanadaiwa kuwa na mkakati wa makusudi wa kumdharau Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho, zinasema hatua ya viongozi wake wakuu, kunyamazia matendo ya Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima na mwenzake, Humphrey Polepole, inatafsiriwa ni dalili tosha kuwa “wanamdharau na kumpuuza,” Rais Samia.

Polepole, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, pamoja na Askofu Gwajima, wamekuwa na kampeni ya wazi ya kupinga chanjo ya corona, kinyume na maelekezo ya chama chao.

Kutokana na hayo, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Mzee Yusuf Makamba, Naibu Katibu Mkuu Bara wa NCCR-Mageuzi, Anthony Komu na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Profesa Edward Hoseah wamezungunzia kadhia hiyo na hatari wanayoiona ndani ya serikali na CCM.

Undani wake, soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Ijumaa tarehe 20 Agosti 2021.
 
Wasilazimishe watu suala la chanjo..dharau inatoka wapi? Watu wana uhuru wa kutoa maoni. Wana haki ya kuchagua what's injected into their bodies. Pole Pole na Gwajima wametoa maoni and its constitutional. Hili suala linaweza kuiumiza sana ccm wasipokuwa makini.

Those of us who are not vaccinated are choosing to stay that way because we are allowed to make that choice for ourselves. My body, my choice, am tired with this bs on social media trolling us to get experimental vaccine that is not even approved.

What studies have been done showing the long term effects?? No one has even had the vaccine that long to conduct that type of study...
 
Mzee Makamba anasema Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki ndani ya CCM kwakuwa wamekuwa wamekuwa wakipingana na Serikali hasa kwenye swla hili la chanjo.

Mzee Makamba anasema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakimdharau sana Rais samia hivyo ametaka washughulikiwe mara moja.

Mzee Makamba anasema yeye si msemaji wa CCM lakini anashangaa ukimya wa baadhi ya Wana CCM na viongozi wa CCM hasa katika hali ya Rais kuonekana ana dharauliwa na baadhi ya wana CCM.

Mzee Makamba ametaka wana CCM kuwachukulia hatua Gwajima na Pole pole.. kwani hawavumiliki.

Chanzo: Magazeti
Wakati mwingine ni vizuri watoto wa hawa wazee wakajaribu kuwazuia baba zao kuji involve na mambo kama haya....huyu mzee zama zake zimepita.
Alimtukana sana Hayati JPM ona sasa hivi anakurupuka tu...akae kwa kutulia kwani hana mvuto wowote katika ulimwengu wa sasa.
 
Wewe makamba unatafuta kutukanwa. Si unyamaze, usubiri kufa. Ulifanya yako ukamaliza sasa unakenua meno ya nini? Watu wasiseme? Imperial president unamtetea nini? asisemwe? Rubbish!
Kufa hata wewe unasubiri kufa ntymbu wa makengeza. Tena unaweza ujafa wewe yeye akabaki.

Kama unatetea uhuru wa maoni wa Gwajima, unapinga vipi tena uburu wa maoni wa Makamba ?
 
Mzee Makamba anasema yeye si msemaji wa CCM lakini anashangaa ukimya wa baadhi ya Wana CCM na viongozi wa CCM hasa katika hali ya Rais kuonekana ana dharauliwa na baadhi ya wana CCM.

Mzee Makamba ametaka wana CCM kuwachukulia hatua Gwajima na Pole pole.. kwani hawavumiliki.
Alitakiwa aendelee kuiweka chini volume kama alivyofanya tulipokumbwa na tukio zito kama Taifa. Kwa sasa kuiweka volume juu ataleta rabsha zisizoza msingi. Asilazimishe watu waanze kumshuku isivyotakikana! Yangu ni hayo.
 
Mzee kusema anadharauliwa ni dharau pia,

Katibu Mkuu si alishasema wameshaanza mchakato wa kuwashughulikia ?

Au mnataka na "mama" aanze kuwabatiza kwa moto🔥
 
Mzee Makamba anasema Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki ndani ya CCM kwakuwa wamekuwa wamekuwa wakipingana na Serikali hasa kwenye swla hili la chanjo.

Mzee Makamba anasema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakimdharau sana Rais samia hivyo ametaka washughulikiwe mara moja.

Mzee Makamba anasema yeye si msemaji wa CCM lakini anashangaa ukimya wa baadhi ya Wana CCM na viongozi wa CCM hasa katika hali ya Rais kuonekana ana dharauliwa na baadhi ya wana CCM.

Mzee Makamba ametaka wana CCM kuwachukulia hatua Gwajima na Pole pole.. kwani hawavumiliki.

Chanzo: Magazeti
Uhuru wa kutoa maoni uko wapi?
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom