Mzee Makamba alimpigia debe Manji kuwa mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Makamba alimpigia debe Manji kuwa mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jibaba Bonge, Nov 27, 2008.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wana JF; hili mnalionaje - Mzee Makamba alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salam, Manji alitoa shs 200 milion (I stand to be corrected) kuchangia ujenzi wa barabara kigamboni. Mhe. Makamba aliwaambia wanakigamboni - wanataka nini zaidi, kama Manji angechukua fomu za kugombea ubunge ndiye anayefaa kuwa mbunge kwa kujitolea fedha zake kwa maendeleo ya wananchi pamoja na kwamba haishi Kigamboni.
   
 2. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  lini wapi na saa ngapi??????
   
 3. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  siku chache kabla ya uchukuaji wa fomu za ccm za kura za maoni kugombea ubunge 2005
   
 4. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2008
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zilipendwa kampango pekee heheh
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,857
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyoiweje?
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Ochu ni kweli Manji alitoa Mil 200 na Makamba alimnadi kwenye kura za maoni na Manji alishinda ila busara za CCM na Mkapa kama mweneykiti zilitumika kumuengua na kumpatia nafasi hiyo Mbunge wa sasa Mwichumu Msomi.

  Huyu Makamba nadhani ni mtu hatari, provided mtu anapesa yeye yuko tayari kumuunga mkononi hata kama pesa zanyewe ni chafu kama hizo za Manji na Rajab Maranda zilizotumika kununua Tawi la Chadema Kigoma.
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Pesa ya EPA[Rajab Maranda] ndiyo iliyotumika kumnunua Kaborou kutoka Chadema kuja CCM; pesa hiyo hiyo Makamba akaitumia kuhakikisha Kaborou anachaguliwa kuwa mbunge wa Afrika Mashariki. Mzee Makamba ukiwa na michuzi basi kwake imetoka.
   
 8. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nyumba ya Makamba ya serikali alinunuliwa na Manji. That is why
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Ni kweli Manji 2005 alitoa millioni 200 kujenga barabara ya Zakiem mpaka Mbagala kuu katika jimbo la kigamboni. na alishinda kwenye kura za maoni, halafu akaenguliwa. Makamba nauwezo mdogo sana wa kung'amua mambo sensitive...porojho nyingi na kusema bila kufikiri ndio kunako mfanya ajulikane. Japo si jambo la kupinga, yule mzee ni mchapa kazi sana lakini kizingiti ni uwezo wa kufikiri na kuwa sensitive.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Very interesting kuona kuwa baadhi ya wanaJF wanambeza jibaba kwa aliloibua. Ni haki, given kuwa tuna uhuru wa kupingana kwa hoja. Lakini ni common sense kuwa mtu aki-invest anategemea returns, na swali linakuja hizo returns zinarudi vipi. Manji lengo lake la mbali si kuwanufaisha wapiga kura, kama lengo lake lingekuwa ndio hilo angeweza kuishia hapo tu bila kugombea. Ni sawa leo Makamba aibuke na kusema RA amechangia matrilioni kadhaa kwenye uchumi wa Tanzania, kwa hiyo anafaa kuwa rais that will be a joke. Ni kweli mzee wetu ni mchapa kazi, lakini uwezo wake wa kufikiri na kufanya judgement una utata.
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Luteni Makamba ni mzee anayetia kichefuchefu sana!
  Kwamba mtu huyu ameweza kupenya kuingia kwenye nafasi kubwa za uongozi - that is not such a big deal. Inapokuja kwamba anaendelea kuwepo kwenye nafasi ya juu kwenye uongozi wa chama kwa muda mrefu kiasi hiki, ...nakosa majibu kwamba inawezekanaje hili kutokea!

  CCM imeharibika beyond repair! Would you doubt that?
  .
   
 12. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hivi kweli hapa hatuchanganyi INAYAT Manji na YUSUPH Manji?
   
 13. D

  Dondoa Member

  #13
  Nov 28, 2008
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Makamba need to go.. amechoka kimwili na kifikra
   
 14. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Makamba atishia kuwaburuza watu kortini
  By Mike Williams | Published 08/14/2005 | Habari za Kitaifa | Unrated  Makamba atishia kuwaburuza watu kortini

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Luteni (mstaafu) Yusuf Makamba ametishia kuwaburuza mahakamani watu wanaodai alimpigia debe mshindi wa kura za maoni kwa tiketi ya CCM, Bw. Yusuf Manji, katika Jimbo la Kigamboni.

  Aidha tayari ameliandikia barua gazeti moja lililoripoti habari hizo, na kuelezea nia yake ya kuliburuza mahakamani iwapo halitamuomba radhi katika kipindi cha siku saba.

  Akihojiwa na Nipashe jijini jana, Bw. Makamba alisema madai hayo yamemdhalilisha machoni pa watu anaowaongoza na mbele ya chama chake (CCM).

  Alisema yeye kama Makamba, hana kiwanda, wala kampuni yo yote, na kwamba jina lake ndilo raslimali kubwa anayoitegemea, hivyo hatua yo yote ya kudhalilisha jina lake, hataivumilia.

  Akifafanua kilichotafsiriwa kwamba alimpigia debe Bw. Manji, mkuu huyo wa mkoa, alisema kilichomponza ni kauli yake kwamba watu wanaojihusisha na maendeleo, hususan kutoa misaada, ndio wanafaa kuwa viongozi.

  "Na mimi sijutii kauli yangu hiyo, huwezi kuwa kiongozi, kama wewe mwenyewe haupo mstari wa mbele katika maendeleo,' alisema.

  Vilevile alisema huenda hatua yake ya kukubali kuwa mgeni rasmi, katika hafla moja ya kuchangia maendeleo, ambayo pia ilihudhuriwa na Bw. Manji, huenda ndio imemponza.

  Hata hivyo, alisema katika hafla hiyo, Bw. Manji alichangia mikokoteni 20 kwa ajili ya vijana na yeye (Makamba) akachangia 10.

  Alisema katika hafla nyingine Bw. Manji alichangia Sh. milioni 1 kwa ajili ya visima, na yeye akachangia Sh. laki 5 na ofisi yake ikachangia Sh. milioni 1.

  "Jamani, ungetegemea mimi kiongozi wa watu, nipuuze hafla ya kuchangia maendeleo? Kwa taarifa waliochanga ni wengi, nikiwemo mimi mwenyewe, japo sigombei.

  Nasema hafla hiyo hata ingeandaliwa na Chadema au TLP, mimi ningekwenda, maana kuchangia maendeleo sio siasa,' alisema Luteni Makamba.

  Pia alisema ataliburuza mahakamni gazeti moja litolewalo kila wiki, kwa kuandika kwamba'Manji ni mhindi wa Makamba'.

  Luteni Makamba alikiri kwamba wana CCM wote waliojiingiza kwenye kinyang'anyiro cha ubunge walienda kumuona naye akawatakia kila la heri.

  Alisema kwenye mkoa wake wameshinda watu wengi kwenye kura hizo, ambao pia walikwenda kwake kumuona'Sasa nashangaa kusikia kauli za mhindi wa Makamba, mbona waliokuja kuniona ni wengi na wameshinda, kwa nini hawasemi Mpogoro wa Makamba au Mjaluo wa Makamba? Kauli hizi ni mbovu sana,' alisema.

  Bw. Makamba alisisitiza kwamba wakati wote wa kinyang'anyiro hicho, hakukanyaga kwenye mkutano wa mgombea ye yote na kwamba hata kwenye ofisi za CCM hakutia mguu.

  Source:
  Makamba atishia kuwaburuza watu kortini
   
 15. D

  Dondoa Member

  #15
  Nov 28, 2008
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gazeti hili la mwaka gani?
   
 16. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Makamba atishia kuwaburuza watu kortini
  By Mike Williams | Published 08/14/2005 | Habari za Kitaifa | Unrated  Makamba atishia kuwaburuza watu kortini

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Luteni (mstaafu) Yusuf Makamba ametishia kuwaburuza mahakamani watu wanaodai alimpigia debe mshindi wa kura za maoni kwa tiketi ya CCM, Bw. Yusuf Manji, katika Jimbo la Kigamboni.

  Aidha tayari ameliandikia barua gazeti moja lililoripoti habari hizo, na kuelezea nia yake ya kuliburuza mahakamani iwapo halitamuomba radhi katika kipindi cha siku saba.

  Akihojiwa na Nipashe jijini jana, Bw. Makamba alisema madai hayo yamemdhalilisha machoni pa watu anaowaongoza na mbele ya chama chake (CCM).

  Alisema yeye kama Makamba, hana kiwanda, wala kampuni yo yote, na kwamba jina lake ndilo raslimali kubwa anayoitegemea, hivyo hatua yo yote ya kudhalilisha jina lake, hataivumilia.

  Akifafanua kilichotafsiriwa kwamba alimpigia debe Bw. Manji, mkuu huyo wa mkoa, alisema kilichomponza ni kauli yake kwamba watu wanaojihusisha na maendeleo, hususan kutoa misaada, ndio wanafaa kuwa viongozi.

  ”Na mimi sijutii kauli yangu hiyo, huwezi kuwa kiongozi, kama wewe mwenyewe haupo mstari wa mbele katika maendeleo,’ alisema.

  Vilevile alisema huenda hatua yake ya kukubali kuwa mgeni rasmi, katika hafla moja ya kuchangia maendeleo, ambayo pia ilihudhuriwa na Bw. Manji, huenda ndio imemponza.

  Hata hivyo, alisema katika hafla hiyo, Bw. Manji alichangia mikokoteni 20 kwa ajili ya vijana na yeye (Makamba) akachangia 10.

  Alisema katika hafla nyingine Bw. Manji alichangia Sh. milioni 1 kwa ajili ya visima, na yeye akachangia Sh. laki 5 na ofisi yake ikachangia Sh. milioni 1.

  ”Jamani, ungetegemea mimi kiongozi wa watu, nipuuze hafla ya kuchangia maendeleo? Kwa taarifa waliochanga ni wengi, nikiwemo mimi mwenyewe, japo sigombei.

  Nasema hafla hiyo hata ingeandaliwa na Chadema au TLP, mimi ningekwenda, maana kuchangia maendeleo sio siasa,’ alisema Luteni Makamba.

  Pia alisema ataliburuza mahakamni gazeti moja litolewalo kila wiki, kwa kuandika kwamba’Manji ni mhindi wa Makamba’.

  Luteni Makamba alikiri kwamba wana CCM wote waliojiingiza kwenye kinyang’anyiro cha ubunge walienda kumuona naye akawatakia kila la heri.

  Alisema kwenye mkoa wake wameshinda watu wengi kwenye kura hizo, ambao pia walikwenda kwake kumuona’Sasa nashangaa kusikia kauli za mhindi wa Makamba, mbona waliokuja kuniona ni wengi na wameshinda, kwa nini hawasemi Mpogoro wa Makamba au Mjaluo wa Makamba? Kauli hizi ni mbovu sana,’ alisema.

  Bw. Makamba alisisitiza kwamba wakati wote wa kinyang’anyiro hicho, hakukanyaga kwenye mkutano wa mgombea ye yote na kwamba hata kwenye ofisi za CCM hakutia mguu.

  Source:
  Makamba atishia kuwaburuza watu kortini
   
 17. M

  Mkira JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2008
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Juzi juzi hapa nimetembelea kigamboni!!!!

  Nikaonyeshwa eneo Kubwa saaaaaaaana zaidi ya heka 100! kuwa manjia amenuanua hilo eneo. Loye hilo liko baada ya mji mwema. Eneo hilo ni beach ninadhani yeye kanunia kwa hela kiduchuu!!!!!!!!!! Lakini atakamua hela hapo siku za baadaye!!!!!


  Kwa hiyo hata milioni 200 hizo si kitu!!!

  Tanzanaia ya leo ili kuepusha vita baadaye ni vizuri JK yuko katika nafasi nzuri ufanyike unyanganyi wa mali Zote ziligawiwa buree!! kwa the so called viongozi na matajiri wahindi hapa na waafrica hapa TZ!!

  Asipofanya hivyo tutafanyua hivyo baadaye kwa gharama kubwa. Those of us who are concisious of our problem can not and will not torelate to see the richer get richer and richer while the pooerer becomes poorer and poorer!!
   
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kwanini unanini unahisi hivyo? maana katika thread hii sijaona hilo jina Inayat hapa anayeongelewa ni fisadi Yusuph Manji. Kama kuna ya huyo Inayat yawekwe hapa pia.
   
 19. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
   
 20. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Na mlioko Kigamboni mkichunguza vizuri basi na Mzee huyu mpenda pesa atakuwa kanunuliwa kiwanja pembeni ya kiwanja cha Manji
   
Loading...