Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend

Mbele yake Nyuma yetu.

JEMBE letu hatunalo tena.

Nawapa pole WAFIWA kwenye kipindi hiki kigumu walichonacho/wanachokipitia.

Ndio,

Ni SAFARI ya wote, tunachopishana ni wakti tu.

Mwenyezi Mungu amrahisishie Mzee wetu MAJUTO huko aendako.

Naam,

Pengo lake halitozibika, na SISI tuliobaki tunakumbushwa ya kuwa KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI
 
Kiukweli huyu mzee alikua mchekeshaji haswaa bonge la comedian

Mimi ni miongoni mwa watu waliopenda sana sanaa yake hususan movie zake za vichekesho

Hatokaa hatokee kwa sasa hayupo wala cjaona aliyemzidi au hata kumkaribia majuto kwa comedy

Ila kinachoniuma ni kimoja wasanii maarufu kama hawa wangekua europe wangekua mabilionea ila inasikitisha sana kuona wasanii kama mzee majuto na bibi kidude na wengineo wengi wanaish maskini wakati wamefanya kazi kubwa

Nina wasiwasi huenda kuna watu wanakula na kuwanyonya wasanii

Nimalizie kwa kusema jaman cc wabongo tuachen unafiki maana majuto aliugua sana akawa anaomba msaada huku na kule aende india ni wachache sana walichanga eti leo kafaa mnamwaga mirambi rambi na kumpost mara wengine wanatoa misaada ya msiba mxiiiiiiew kwanini mtyu akiwa hai tusimthamini lakini akishakufa tunaleta unafiki oooh rip ooooh nichangia
kwanini msijitoe akiwa hai?mpk afe tu ndo mjitolee mxxieewww

TUBADILIKE TUACHE UNAFIKI
 
Kufa kila mmoja wetu atakufa kwa wakati wake.

Cha msingi tujitenge na dhuluma.
 
Tatizo hawajitambui. Hawamjui adui yao. Yule anayewageuzaga karai za zege kila uchaguzi mkuu unapowadia.
 
Pole kwa family yake.. Japo naona wanasiasa wetu wanafuta kick mpka msibani.. Mtu msibani kaenda kavaa nguo za chama..analeta vyama mcbani ts boring
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom