Mzee Lowassa: Kwa sasa nchi imeshika adabu na mambo yanakwenda vizuri. Bado tuna tatizo la ajira nchini...

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuondolewa kazini kwa watendaji wazembe na wasiotimiza wajibu wao umefanya nchi kushika adabu.

Lowassa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 20, 2019 katika mahafali ya Shule ya Msingi Meyers mjini Arusha.

"Rais Magufuli (John) anastahili pongezi anafanya kazi nzuri sana, tunaona mawaziri wanafanya kazi nzuri ,Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo kule wengine huku nchi imewaka moto kila sehemu,” amesema.

Asema kazi nzuri za Rais zinapaswa kupakwa ‘poda’ kwa kuhusisha na kuboresha elimu ambayo itawapa ujuzi wahitimu kujiajiri.

"Kuna vijana wengi wanamaliza masomo kutokana na mpango wa elimu bure sasa tujitahidi elimu hii iwasaidie vijana kupata ujuzi na ubunifu ili kuweza kujiajiri" amesema Lowassa.

Mkuu wa shule hiyo, Sista Anjali Thomas amempongeza Lowassa kwa mchango alioutoa mpaka kikapatikana kiwanja cha ujenzi wa shule hiyo.

View attachment 1212361

To paraphrase; "Amelegea kuliko mlenda".
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Bora kuwa mnafiki ili uishi salama bila misukosuko
 
Nampongeza sana kwa kuamua kuwa mkweliView attachment 1212423
Screenshot_2019-09-20-20-15-26.jpeg
 
Haya mahafari ya darasa la saba wageni rasmi si wanakuwaga wenyeviti wa vijiji, kweli rumenyooka kutoka kuwa mgombea urais hadi kuwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya std 7
 
Huu ndo unafiki wenyewe sasa! Yaani unatambua kuwa alipatia kumkataa Lowassa na wakati huohuo unamuona kuwa ni mpumbavu kwa kutengua kujiuzulu. Ndo kusema hukupenda Lipumba arejee uwenyekiti wake bali angeendelea kuwa mwanachama wa kawaida. Labda nikuulize; kwanini ulitamani Lipumba asiwe mwenyekiti tena wa CUF?
Mkuu lipumba ataingia kwenye rekodi kwa kuamua kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu.je alishikiwa panga au silaha ajiuzulu? Yaani baada ya kuona chama kimekusanya ruzuku za kutosha ndo anadai kurejea kwenye uwenyekiti?
 
Bila shaka umeshindwa kutambua kwanini hupendi kuona Lipumba anaendelea kuwa mwenyekiti wa cuf. Yaani kuingia kwake kwenye rekodi ndo tatizo unaloliona kuhusu Lipumba! Nikisema unafuata mkumbo mawazo ya watu nitakosea?

Ni kweli alipoamua kujiuzulu hakuna aliyemshikia panga bali alifanya hivyo kwa hiyari yake mwwnyewe. Mbona alipotengua kujiuzulu vile vile hakuna aliyemshikia panga; tatizo liko wapi hapo? Au katiba ya cuf inasema kiongozi akijiuzulu haruhusiwi kutengua maamuzi yake? Acha kushikiwa akili na wanaozuga aibu kutokana na maauzi ya kijinga ya kubadili gia angani.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Edward Lowassa akiwa Monduli mkoani Arusha amesema kwamba ''Kwa sasa nchi imeshika adabu na mambo yanakwenda vizuri”

Napenda kuipongeza sana Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya elimu kuwa bure.

Nimekuwa na nitaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusisitiza umuhimu wa Elimu bora na kwa wote, Elimu inayowaandaa vijana kuingia soko la ajira la dunia na pia kuwawezesha kujitegemea baada ya masomo.

Bado tuna tatizo la ajira nchini kwetu, niziombe mamlaka za elimu zitilie mkazo swala la elimu ya ujuzi (skills) ili vijana wamalizapo waweze kujitegemea.

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuondolewa kazini kwa watendaji wazembe na wasiotimiza wajibu wao umefanya nchi kushika adabu.

Lowassa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 20, 2019 katika mahafali ya Shule ya Msingi Meyers mjini Arusha.

"Rais Magufuli (John) anastahili pongezi anafanya kazi nzuri sana, tunaona mawaziri wanafanya kazi nzuri ,Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo kule wengine huku nchi imewaka moto kila sehemu,” amesema.

Asema kazi nzuri za Rais zinapaswa kupakwa ‘poda’ kwa kuhusisha na kuboresha elimu ambayo itawapa ujuzi wahitimu kujiajiri.

"Kuna vijana wengi wanamaliza masomo kutokana na mpango wa elimu bure sasa tujitahidi elimu hii iwasaidie vijana kupata ujuzi na ubunifu ili kuweza kujiajiri" amesema Lowassa.

Mkuu wa shule hiyo, Sista Anjali Thomas amempongeza Lowassa kwa mchango alioutoa mpaka kikapatikana kiwanja cha ujenzi wa shule hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Sasa ulitegemea aongee nini zaidi ya hayo?

Kwani Mama Regina yeye anasemaje??
 
Back
Top Bottom