Mzee Lowassa kuwasamehe Bure wanaccm na wanachadema waliomnyanyapaa na kumtuhumu ufisadi ili kunusuru siasa za nchi yetu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,791
2,000
Nimeelezwa na mzee mmoja ninayemheshimu sana ambaye amezaliwa upya katika Kristo ya kwamba mzee Lowassa amewasamehe bure wale wote waliomuita fisadi.

Inaelezwa kuwa mzee Lowassa ametafakari sana na kugundua siasa zetu zimefikia hapa tulipo kwa sababu ya kuzushiana mambo mabaya yasiyo na chembe za ukweli.
Hivyo Lowassa ameona njia pekee ya kulinusuru taifa na siasa UCHWARA ni wanasiasa kusameheana, hivyo ametangaza msamaha kwa wale waliomkata na kumzushia kila aina ya uongo kule CCM.

Kadhalika amewasamehe wanachadema wote waliomzushia kuwa yeye ni fisadi pale Mwembeyanga japokuwa kuna wengine wengi walishamfuata na kutubu.

Ni hayo machache
Maendeleo hayana vyama!
 

shungurui

JF-Expert Member
Sep 1, 2008
3,676
2,000
Huyu naye hajifunzi tu, alikwata panga na ccm aka gambas si kwa sababu ya ufisadi, maana tiss wanajua nani muhusika halisi wa Richmond na wizi mwingine, sasa hajiulizi kama wahusika halisi wanajulikana kwanini yeye alikwatwa panga ili kupisha wengine, mambo mengine huitaji kuwa na rocket science kuufahamu ukweli, hebu mliokaribu naye msaidieni huyo mzee kuamka,.sababu naona anafanya makosa yale yale kila mara, maana kama mpaka vichaa wanapata nafasi why yeye, kuna tatizo gani, hapa ndipo alipatikiwa kujiuliza.
 

TUTABAMS

Member
Sep 10, 2019
55
125
Jambo jema,Ila aanze kujisamehe kwa kutotaka kuongea ukweli ilihali aliujua. Naomba unisaidie kumwulia, Vipi wale M6 waliompigania ambao wengi wao walitiwa ulemavu wa maisha,waliofungwa jela,walioporwa biashara na mali zao,badae akaja kuwasalitia akaenda kuunga mkono juhudi Ameshawaomba msamaha kwa kuwakosea au anahisi yy tu ndio aliyekosewa??
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,669
2,000
Hilo neno "MAENDELEO HAYANA VYAMA" hebu lifute, unatuchefua roho. Maana juzi mzee wenu aliombwa awavutiwe maji kijijini na mama mtu mzima na akamjibu "NENDA KAMUOMBE MUME WAKO" au "DIWANI WAKO ULIEMCHAGUA (Upinzani)" au "MBUNGE WAKO ULIEMCHAGUA (Upinzani) .... Alikua ana maana gani?
 

Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
10,383
2,000
Pamoja na yote tuwe wa kweli Lowasa ni fisadi hata sasa japo hakosi mazuri yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom