Mzee Lowassa alivyowazuga CHADEMA Monduli

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Ngoyai Lowassa kila aliposimama au kuzungumza na wazee wa mila wa kabila la wamaasai pamoja na viongozi wa dini wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Monduli aliwasisitiza

"Msiwasikilize watu wanaotaka kunichonganisha na Rais Magufuli,mimi niko vizuri na Rais Magufuli."

Wakati akisema haya viongozi wa chama chake wakawa wakimshambulia Rais Magufuli na chama chake kwenye majukwaa. Wazungumzaji wa CCM walikuwa na kazi moja tu kuwakumbusha wananchi kuwa msigombanishwe na Rais kwani hata Lowassa amesema hana tofauti na Rais Magufuli hivyo mchagueni mgombea wa CCM.

Matokeo yamethibitisha kweli Lowassa hakutaka kugombanishwa na Rais Magufuli.
 
Nani anapenda anyang'anywe mali yake?
Magufuli amejawa na kiburi visasi,wewe ulitaka Baba wa watu asemeje?
Magufuli anapenda kusifiwa na kujikweza,bila kuongea hivo ange ulizwa vyeti vya kuzaliwa.
Akili kichwani.
 
Huyu MZEE yupo ili kuuvuruga upinzani......toka kitambo nilishasema, huyu mzee ni wa kuachana naye
 
Mbona mnaweweseka sana, uchaguzi umekwisha mumejitangazia ushindi at gun point basi wacheni maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom