Mzee Kikwete leo Mbagala umenena vyema kuwa miradi mingi ya awamu hii uliiasisi wewe japo wa gesi ya Mtwara hujauongelea

Village fooler

JF-Expert Member
Mar 16, 2020
308
1,000
Hamkuwahi kuyaona mema ya kiongozi yoyote ikiwa anatokea CCM, kwahiyo hatutegemei nyinyi kumsifia Magufuli.
Kama unajua hvo we endelea kusifia na kuabudu hayo unayoyaona Ni mema nasisi pia tutaendelea kuyasemea Yale ambayo si mema tunayoyaona na hiyo ndio siasa kwa bahati mbaya upande wenu wengi hamlijui hilo mnabaki mnasema eti upinzani unapinga kila kitu kwahyo mlitaka wapinzani nao waanze kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu???
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
5,282
2,000
Nimemsikiliza JK leo Mbagala, He was at pains kumwongelea Magufuli, unamwona kabisa nafsi inamsuta, body language betraying him...sidhani kama atasimama tena kwenye Jukwaa la Kampeni.
Ulichotaka kukiona wewe ndio akili yako imekuaminisha lakini ukweli ni kwamba jk na jpm wako chama kimoja na wana dira moja
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
1,417
2,000
Kama unajua hvo we endelea kusifia na kuabudu hayo unayoyaona Ni mema nasisi pia tutaendelea kuyasemea Yale ambayo si mema tunayoyaona na hiyo ndio siasa kwa bahati mbaya upande wenu wengi hamlijui hilo mnabaki mnasema eti upinzani unapinga kila kitu kwahyo mlitaka wapinzani nao waanze kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu???
Bahati mbaya ni kwamba, hata nyinyi hamjawahi kuelewa kuwa mnaishi katika ndoto ambazo hazina uwezekano wa kutoea.
Kusifia kwako au kutosifia kwako hakutabaadilisha uhalisia wa mambo.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
1,417
2,000
What’s your point?Manake I don’t see a logic katika maandishi yako
Na hauwezi kuiona logic kwasababu umekurupuka kuquote comment isiyokuhusu, bila kujua majibizano Kati yangu na huyo niliemwandikia yameanzia wapi.Subiri hoja mserereko unazoweza kizimudu userereke nazo Kama jinsi ilivyo nyumbu.
 

All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,508
2,000
REA, Shule za Sekondari, Barabara za Lami nk ni baadhi ya miradi uliyoiasisi au kuiendeleza ulipokuwa Raisi wetu. Mungu akubariki kwa kuwa mkweli.

Tulifika mahala tukaaminishwa kwa nguvu za ajabu kuwa awamu zilizopita hazikufanya kitu!

Nilimsikia mgombea mmoja akisema kuanzia wakoloni hadi maraisi wa awamu zilizopita nao walijenga barabara, miradi kadhaa nk. Kuwa, kazi ya serikali inayokusanya kodi ni kuleta maendeleo ya vitu na watu.

Hivyo, kwa kijana anayekuwa, ni vyema ajue tulikotoka tuliko na tunakoenda kwa usahihi bila kujisifu.

Nimefurahi pia kusikia kuwa wewe ndo ulitoa wazo la elimu bure kwa shule za msingi na sekondari na kuweka kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Chetu. Lakini ukisikiliza miziki ya Diamond na wasanii wengine utafikiri kila kitu kimebuniwa na kuwekwa kilipo na awamu ya tano.

Hongera sana Mh. Dr. Kikwete kwa kuweka wazi mambo haya japo hukugusia Mradi Umeme wa Gesi ya Mtwara kuwa uliishia wapi.

Naamini iko siku utaweka wazi tujue kwani tulishaamini tungepata umeme wa nafuu kuliko ilivyo sasa.
Wote hao si wanasisiemu
 

permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
4,613
2,000
Huyu si ndie JPM humnanga kila siku majukwaani kuwa serikali yake ilijaa wapiga dili?
Nimemsikiliza JK leo Mbagala, He was at pains kumwongelea Magufuli, unamwona kabisa nafsi inamsuta, body language betraying him...sidhani kama atasimama tena kwenye Jukwaa la Kampeni.
 

permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
4,613
2,000
Are you sure? Watanzania punguzeni unafiki, watu walikuwa wanakaa Ubungo kwenye foleni kwa masaa, Tazara et. achilia mbali kila mgonjwa mwenye connection alikuwa anakwenda kutibiwa nje kwa pesa za Serikali hasa viongozi wakati Watanzania wengi walipoteza maisha bila kuwa na tiba ya uhakika. Leo hii kila moja anapata matibabu ya uhakika hapa hapa.

Kila kona ya duka Dar ilikuwa na generator lake sijui ile polution tu iliua wangapi? JPM ni moto wa kuotea mbali mwacheni tu. Endeleeni na huyo mlevi wa Konyagi huko anakowapeleka anakufahamu mwenyewe peke yake.
Kadanganye watato, mgao wa Umeme uliisha baada ya JK kumteua prof Sospeter kuwa waziri wa Nishati. Kuhusu hospital, JK alifanya maboresho makubwa ya Hospital za kikanda pamoja na kujenga Kituo cha magonjwa ya moyo pale Muhimbili + ujenzi wa hospital ya Mloganzira etc. Labda useme JPM kajenga zahati tena kwa kushirikiana na wananchi.
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,157
2,000
Wivu ni ugonjwa mbaya sana. JK na JPM wote ni watekelezaji wa ilani ya CCM.

Akiondoka Ngosha atakayekuja ataendeleza alipoishia na wenye nongwa watakuwepo pia.
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,488
2,000
Sijui kwanini huyu jamaa watu bado wanamkumbuka na kumsifia. Wamesahau kaingizia nchi yetu hasara ya Matrillion kwa kuuza gesi yetu. Na Wamesahau pia anapata mgao wake wa IPTL wa shilingi million mia nne na ushehe KWA SIKU.

A smiling devil
Pia aliingiza nchi hasara ya mabillion ya pesa kwa mchakato wa katiba mpya ambao haukuzaa matunda kwa kuvuruga mapendekezo ya tume ya Warioba.
 

John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
593
1,000
Na hauwezi kuiona logic kwasababu umekurupuka kuquote comment isiyokuhusu, bila kujua majibizano Kati yangu na huyo niliemwandikia yameanzia wapi.Subiri hoja mserereko unazoweza kizimudu userereke nazo Kama jinsi ilivyo nyumbu.
Hoja iko kwenye public platform ,alafu comment unataka iwe ni private wakati haiko specified-Are you Ok upstairs?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom