Mzee Kikwete leo Mbagala umenena vyema kuwa miradi mingi ya awamu hii uliiasisi wewe japo wa gesi ya Mtwara hujauongelea

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,187
2,000
REA, Shule za Sekondari, Barabara za Lami nk ni baadhi ya miradi uliyoiasisi au kuiendeleza ulipokuwa Rais wetu. Mungu akubariki kwa kuwa mkweli.

Tulifika mahala tukaaminishwa kwa nguvu za ajabu kuwa awamu zilizopita hazikufanya kitu!

Nilimsikia mgombea mmoja akisema kuanzia wakoloni hadi marais wa awamu zilizopita nao walijenga barabara, miradi kadhaa nk. Kuwa, kazi ya serikali inayokusanya kodi ni kuleta maendeleo ya vitu na watu.

Hivyo, kwa kijana anayekuwa, ni vyema ajue tulikotoka tuliko na tunakoenda kwa usahihi bila kujisifu.

Nimefurahi pia kusikia kuwa wewe ndio ulitoa wazo la elimu bure kwa shule za msingi na sekondari na kuweka kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Chetu. Lakini ukisikiliza miziki ya Diamond na wasanii wengine utafikiri kila kitu kimebuniwa na kuwekwa kilipo na awamu ya tano.

Hongera sana Mh. Dr. Kikwete kwa kuweka wazi mambo haya japo hukugusia Mradi Umeme wa Gesi ya Mtwara kuwa uliishia wapi.

Naamini iko siku utaweka wazi tujue kwani tulishaamini tungepata umeme wa nafuu kuliko ilivyo sasa.
 
Wacha

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
1,038
1,500
Kutekeleza mkuu. Kila mtu anaweza kuahidi maziwa na asali lakini kuileta ndio shida. JPM ataendelea kuwa N0. 1 kwa vitendo hatutaki ngonjera. Huyu watoto wake nao walikuwa marais, Watanzania mnakwama wapi? Mlikuwa mnamsimanga kuwa ni Vasco da Gama Wabongo kwa usahaulifu hamjambo!
 
Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
960
1,000
Sijui ni nini cha ajabu hapo
Kikwete alitekeleza Ilani ya CCM na Dr Magufuli anatekeleza Ilani ya CCM hivyo lazima kuna mambo yatafafa au itabidi mmoja wao ayakamilishe pale mwenzake apoishia ila tegemea mengine/miradi mingi mipya kwani ilani inatekelezwa kwa kwenda Mbele.
 
Antetokounmpo

JF-Expert Member
Feb 5, 2020
289
500
Sijui ni nini cha ajabu hapo
Kikwete alitekeleza Ilani ya CCM na Dr Magufuli anatekeleza Ilani ya CCM hivyo lazima kuna mambo yatafafa au itabidi mmoja wao ayakamilishe pale mwenzake apoishia ila tegemea mengine/miradi mingi mipya kwani ilani inatekelezwa kwa kwenda Mbele ....
Mkuu watu wana chuki binafsi na Magufuli...sio CCM bali ni Magufuli.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
34,649
2,000
Kutekeleza mkuu. Kila mtu anaweza kuahidi maziwa na asali lakini kuileta ndio shida. JPM ataendelea kuwa N0. 1 kwa vitendo hatutaki ngonjera. Huyu watoto wake nao walikuwa marais, Watanzania mnakwama wapi? Mlikuwa mnamsimanga kuwa ni Vasco da Gama Wabongo kwa usahaulifu hamjambo!

JK sio anasifiwa bali anapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa ili kumnanga jiwe. JPM ni namba moja kwako maana unafaidika na madaraka yake.
 
Wacha

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
1,038
1,500
JK sio anasifiwa bali anapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa ili kumnanga jiwe. JPM ni namba moja kwako maana unafaidika na madaraka yake.
Are you sure? Watanzania punguzeni unafiki, watu walikuwa wanakaa Ubungo kwenye foleni kwa masaa, Tazara et. achilia mbali kila mgonjwa mwenye connection alikuwa anakwenda kutibiwa nje kwa pesa za Serikali hasa viongozi wakati Watanzania wengi walipoteza maisha bila kuwa na tiba ya uhakika. Leo hii kila moja anapata matibabu ya uhakika hapa hapa.

Kila kona ya duka Dar ilikuwa na generator lake sijui ile polution tu iliua wangapi? JPM ni moto wa kuotea mbali mwacheni tu. Endeleeni na huyo mlevi wa Konyagi huko anakowapeleka anakufahamu mwenyewe peke yake.
 
Wacha

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
1,038
1,500
Teh... jiwe anaogopa kukanyaga Mtwara naona na JK naye anaogopa hata kupataja🙌🙌

Sijui nini kinaendelea
au yule bibi wa gesi ameshawatumia ujumbe😀😀
Mkuu humtendei haki JPM amekuwa Mtwara mwaka huu mara ngapi? Hata kabla ya kampeni alikuwa kule kama sikosei alilaumiwa kuhongwa jogoo akitokea ntwara.
 
Heron

JF-Expert Member
Oct 4, 2013
1,905
2,000
Sijui kwanini huyu jamaa watu bado wanamkumbuka na kumsifia. Wamesahau kaingizia nchi yetu hasara ya Matrillion kwa kuuza gesi yetu. Na Wamesahau pia anapata mgao wake wa IPTL wa shilingi million mia nne na ushehe KWA SIKU.

A smiling devil
KWANI KUNA RAISI WA CCM AMBAYE HAJATUTIA HASARA?
Sijui Mwinyi na JK Nyerere

BENJAMIN--- Kauza viwanda Vyetu vyote na nyumba za serkal.

MRISHO_________________________

JEIPIIEM_________________________
 
havanna

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
1,623
2,000
Sijui kwanini huyu jamaa watu bado wanamkumbuka na kumsifia. Wamesahau kaingizia nchi yetu hasara ya Matrillion kwa kuuza gesi yetu. Na Wamesahau pia anapata mgao wake wa IPTL wa shilingi million mia nne na ushehe KWA SIKU.

A smiling devil
Hufaham au unaweza kuwa unajisahaulisha, ukiwa na mali nyingi kwenye nchi yako na ukashindwa kuwapa nchi mabepari basi jua vita au migogoro kwenye nchi yako itakuwa kawaida, hawashindwi kukutengenezea zengwe, usipende kulalamika utakuta jamaa walimbana kwenye gas na akakubali, kwani kipindi hiki hawachukui Mali zetu, sema propaganda eti mabeberu
 
havanna

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
1,623
2,000
Sijui ni nini cha ajabu hapo
Kikwete alitekeleza Ilani ya CCM na Dr Magufuli anatekeleza Ilani ya CCM hivyo lazima kuna mambo yatafafa au itabidi mmoja wao ayakamilishe pale mwenzake apoishia ila tegemea mengine/miradi mingi mipya kwani ilani inatekelezwa kwa kwenda Mbele.
Kujenga uwanja chato ilikuwa ni ilani ya chama? Au kutokuongeza mishahara, bidhaa kupanda bei au Kodi kwa wafanyabiasha ilikuwa ni ilani yenu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom