Mzee Kikwete aweka rekodi sawa, Uchumi wa Kati waliopanga na Mkapa ni wastani wa dola 3,000 kila Mtanzania

Mada inalenga kukebehi Serikali ya sasa kwa kumkariri Kikwete kana kwamba amekanusha yanayosemwa na Serikali. Mada inapotosha aliyoyasema Kikwete kuhusu mafanikio ya Serikali ya sasa ambayo wewe unayaita 'propaganda', kwa kumsingizia kwamba amekanusha yanayosemwa na Serikali. Ukweli wa mambo ni kama ifuatavyo.

Pato la wastani wa chini ya USD 1,000 huhesabiwa kuwa Low Income. Kuanzia USD 1,000 hadi USD 3,000 ni Middle Income; na juu ya hapo ni High Income. Ukiisha vuka USD 1,000 unaingia Lower Middle Income na ukikaribia kiwango cha juu cha USD 3,000 unahesabiwa kuwa kwenye Upper Middle Income. Malengo ya Serikali, tangu wakati wa Kikwete, yalikuwa kwamba ifikapo mwaka 2025 mosi, Tanzania iingie uchumi wa kati, yaani kuwe na pato la wastani wa zaidi ya USD 1,000; na pili, kipato cha wastani kiwe takriban USD 3,000.

Serikali ya Magufuli imefikia lengo la kwanza mwaka huu, ikiwa ni miaka mitano kabla ya tarehe iliyopangwa. Hatua hii ilitangazwa na World Bank yenyewe. Ni dhahiri kwamba mada yako inapotosha ukweli kwa kusema Kikwete amekanusha 'propaganda' za Serikali. Hakuna lo lote alilokanusha Kikwete. Yeye ameishia kutaja lengo la tangu Serikali yake ya kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. Serikali ya Magufuli imefanikisha hilo miaka mitano mbele na hilo likatangazwa na World Bank yenyewe. Hakuna cha propaganda hapo. Serikali iliendelea kusema kwamba kipato cha wastani, kufuatana na World Bank, ni USD 1,038. Wewe unamkariri Kikwete kwamba amesema Serikali inadanganya kwa kusema kiwango cha wastani ni USD 3,000. Serikali haijtamka hivyo. Mtu ambaye hakusikiliza hotuba ya Kikwete ataamini kwamba uyasemayo ni ukweli, ambapo si kweli. Tusubiri tuone kama lengo la pili la wastani wa mapato litafikiwa hapo mwaka 2025. Kwa kuangalia kasi iliyofikiwa katika miaka mitano tunayoimalizia, bila shaka lengo hilo litafikiwa pia. Mungu ibariki Tanzania na utulinde na habari potofu zinazoweza kuwaghafirisha wananchi.
Wewe ni utopolo
 
Wewe ni utopolo
Onyesha 'utopolo' wangu uko wapi. Nimekutajia vigezo vilivyopo, nani aliyeviweka na nani alivitaja mintarafu Tanzania. Bado unaniita 'utopolo', neno ambalo wala sijui maana yake ingawa nahisi linaashiria uduni, ujinga, upumbavu, n.k. Kwa kushindwa kwako kujadili hoja zangu na badala yake unakimbilia kutukana, hudhani kama dhihaka hizo zinakufaa wewe mwenyewe kuliko mimi?
 
Kushuka kwa uchumi kama ulivyosema ni kweli kunawezekana kutokea kwa kuwa uwekezaji wa miundombinu imara ni ghali sana,uchumi utaimalika kwa kasi pindi miundimbinu itakapo kamilika kujengwa.
Sio lazima kila wakati kupanda,kuna wakati unashuka alafu unapanda zaidi (wave) kwa kasi ya kufikia malengo.
Ndio maana yapo malengo ya muda mfupi na mrefu.
Shabaha kubwa ni kufikia malengo hata kama tutakwama katikati/mahala kikubwa ni kusimamia kile tunachoamini kuwa tunaweza kufanya kwa vyovyote vile.
Uchumi upi utakaoimarika kwa kuwekeza reli ambayo inaelekea kusiko na mzigo wowote wa maana? ratio iliyopo ni 30% kwa central corridor vs 70% kwa njia ya Tanzam,kwa hesabu hizo unaona kuna uchumi gani utakua hapo?
Pili unawekeza kwenye umeme kwa matilioni afu umeme utakuwa iddle hautumiki,so far tuna umeme excess na uko cheapest kuliko Kenya na nchi nyingine za EAC lakini je wapi kuna wawekezaji wengi? tatizo sio uhaba wa umeme wala gharama bali masuala mengine ya kiurasimu ikiwemo sera zisizotabilika na kukandamizana kwenye makodi hovyo..Tungeweza kujenga bwawa 1 tu la let say mg 400 zingedumu miaka zaidi ya 15 ili mapesa mengine yakafanye mambo mengine badala ya kuwekeza mationi kwenye umeme wa mgwt 2000 lakini tunatumia nusu tu ya huo na mwingine utakuwa iddle kwa miaka mingi huku maintanance cost zikiwa palapale
Tatu miradi yote hiyo pamoja na kuwa haina tija sasa wala baadae inagharamiwa kwa zaidi ya 60% kwa mikopo ya kibiashara sasa huoni kila awamu watanzania watakuwa wanaumia kwa kukosa focus nzuri ya kuwekeza pesa? maana awamu hii imekopa pesa nyingi haijawahi tokea kiasi kwamba awamu ijayo itakua kulipa madeni tu,kumbuka mkapa alipata nafuu ya msamaha wa madeni ndio uchumi ukaanza kufufuka sasa huyu anaturudisha kulekule kwa kukosa strategic thinking na proper allocation of resources
 
Kikwete naona kaweka sawa kuhusu hizi propaganda kuwa Magufuli kafikia uchumi wa Kati kabla ya muda uliopangwa.

Kikwete kaweka sawa kuwa Uchumi wa Kati uliopangwa ni dola 3,000 na sio hii 1080. Na kampa Magufuli challenge kuwa 2025 inatakiwa awe amefikia kipato hicho kwa kila mtanzania.

Pia kaweka rekodi nyingine sawa kuwa Uchumi kukua kwa asilimia 7 Ni Mkapa ndio aliweka na baada ya Mkapa haijawahi kushuka hiyo Kasi.

Pia soma > Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Hii ni tofauti na propaganda za Sasa hivi kuwa Magufuli ndio kapandisha Kasi ya ukuaji Uchumi.



Hayo maneno ya Mh. Kikwete ni propoganda. Sasa hiyo programu anayosema ambayo haikuandikwa popote wala kutangazwa popote na wala haiko kwenye ilani yoyote ya CCM ila tu iko kichwani mwa mtu itaaminiwa vipi?. Na bahati mbaya anasema alipanga na mtu ambaye hawezi kuhakikisha kwa sababu ni marehemu. Kikwete hapo amebujiiii
 
Hayo maneno ya Mh. Kikwete ni propoganda. Sasa hiyo programu anayosema ambayo haikuandikwa popote wala kutangazwa popote na wala haiko kwenye ilani yoyote ya CCM ila tu iko kichwani mwa mtu itaaminiwa vipi?. Na bahati mbaya anasema alipanga na mtu ambaye hawezi kuhakikisha kwa sababu ni marehemu. Kikwete hapo amebujiiii

Au nae ni msaliti!?
 
72 Reactions
Reply
Back
Top Bottom