Mzee Kikwete ashangaa Walimu kukosa ajira

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,217
217,186
Sasa mimi namkumbusha tu Mzee wangu kwamba nini walimu bhana ! Kwa ujumla Tanzania haina ajira kwa vijana , kuanzia madaktari hadi wahasibu .

Nchi yeyote isiyotoa ajira kwa raia wake yenyewe wala nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wake ambao ni wachache kuliko wafanyakazi wa nchi yeyeto duniani ( chini ya laki 6 kwa uwiano wa wananchi mil 55 ) ni sawa na nchi mfu

=====
Kibaha. Wakati wimbi la wahitimu likiendelea kuongezeka nchini, Rais mstaafu Jakaya Kikwete ameeleza kusikitishwa na idadi kubwa ya walimu kuwepo mitaani kwa kukosa ajira licha ya upungufu wao kwenye shule nchini.

Kikwete ametoa kauli hiyo jana ikiwa zimepita siku 14 tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipolieleza Bunge mkakati wa Serikali wa kuajiri walimu 16,000 wa shule za msingi na sekondari.

Majaliwa alisema hayo Novemba 14, wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi ambaye alihoji mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wanapatikana watumishi wa kutosha kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo, Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 37 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) yaliyofanyika makao makuu ya chuo hicho Bungo, Kibaha mkoani Pwani alizungumzia mpango aliouanzisha wa kuzalisha walimu wakati wa uongozi wake.

Alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuboresha elimu nchini kwa nyakati tofauti huku akigusia utaratibu aliouanzisha kwenye utawala wake uliokuwa unawaruhusu wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuchukua mafunzo ya ualimu mpango ambao baadaye ulisitishwa.

Kikwete alisema wakati anamaliza kipindi chake cha urais aliacha idadi kubwa ya walimu nchini na baada ya hapo wameendelea kuwa wengi kiasi ambacho wapo wanaokosa nafasi za ajira.

“Tulianzisha mpango uliokuwa unawawezesha wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuchukua mafunzo ya ualimu nia ikiwa ni kuzalisha walimu wengi mpango uliokuwa unaitwa vodafasta,” alisema Kikwete aliyekuwa Rais kati ya mwaka 2005 hadi 2015.

Alisema jitihada zingine kwenye uongozi wake katika kuboresha elimu ilikuwa ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari za kata, ambapo walikumbana na changamoto ya uhaba wa walimu wakaja na mpango huo wa mafunzo ya vodafasta.
Akizungumzia kauli hiyo ya Kikwete, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo aliiambia Mwananchi jana kuwa mpango huo ulisitishwa kutokana na kukosa tija kutokana na kuwepo walimu wa kutosha.

Dk Akwilapo alisema mpango huo haukuwa na tofauti na ule wa `Elimu kwa Wote’ (UPE) mwaka 1974/75 ulitumika kuongeza walimu.

Kuhusu ukosefu wa ajira za walimu, Katibu mkuu huyo alisema suala hilo liko chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Naye Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara alipoulizwa kuhusu suala hilo la ajira kwa walimu alijibu, Serikali inakusudia kuajiri walimu 16,000.

“Hili alilisema Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) bungeni wakati akijibu swali la Mbunge (wa Mlalo- CCM, Rashid) Shangazi,” alifafanua Waitara.

Waitara alieleza serikali chini ya Rais mstaafu Kikwete ilianzisha mpango wa kuandaa walimu wa haraka kwa sababu wakati huo kulikuwa na upungufu.

“Kwa sasa tuna walimu wa kutosha wenye ubora wa kufundisha vyuo, sekondari, shule za msingi na awali, changamoto ni uwezo wa Serikali kuajiri walimu wa kutosha na Serikali itakuwa ikiajiri kulingana na uwezo wa fedha,” alisema Waitara

Pia katika mahafali hayo ya OUT, Kikwete alitahadharisha kutokana na tekInolojia inavyoendelea kwa kasi duniani, hali inaonyesha ifikapo mwaka 2050 nusu ya kazi zinazofanywa na binadamu kwa sasa zitakuwa zinafanywa na mashine.
Alisema kulingana na hali hiyo pia nafasi hizo zitakuwa zinawalenga wahitimu wa elimu ya juu huku wa elimu ya kawaida wakishindwa kupata nafasi.

Jumla ya wahitimu 3,900 wa shahada mbalimbali walitunukiwa na Mkuu wa Chuo hicho, Mizengo Pinda ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu.

Mmoja wa wahitimu kwenye mahafali hayo alikuwa ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa aliyetunukiwa shahada ya uzamivu (PhD), ambaye aliwataka watumishi wa umma nchini wenye lengo la kujiendeleza kufanya mawasiliano na waajiri wao kabla ya kujiunga na masomo ili kupewa maelekezo muhimu na njia za kufuata.

Alisema Serikali haina lengo la kuwazuia watumishi wake kujiendeleza kitaaluma bali inawaruhusu kufanya hivyo iwapo wanafuata utaratibu.

Dk Mary alisema aliamua kujiendeleza kielimu ili kuongeza weledi wake kwenye kutekeleza majukumu yake kwa umma.


CHANZO: Mwananchi
.
 
Wacha wanyooshwe si-ndio uwa wanasimamia uchaguzi na kuiweka ccm madarakani.

Sasa ivi hatutakiwi kuwa na huruma na watu wote ambao uwa wanashiriki maovu halafu yakiwakuta yakuwakuta wanataka huruma ya wananchi wapambane walimu ni kundi kubwa lakini hawajitambui.


Naunga mkono hoja yako..hawajitambui
 
Anashangaa nini? Unafiki tu, hamna jipya. Hakuna ajira kwa fani zote serekalini na kwenye sekta binafsi, kote hali ni mbaya, yeye anashangaa walimu! Yeye na mwenzake ndio chanzo cha mateso watu wanapitia sasa. Alikuwa ana uwezo kabisa wa kuzuia hii hali lakini aliachia. Kama hana la kusema ajikalie tu kimya, aendelee kuenjoy 80% ya mshahara wake wa zamani, angalau mwenzetu ana uhakika wa kula na kuvaa.
 
Kikwete aliingia na jina la magufuli mfukoni mpaka wenzake wakalalamika Sasa anashangaa nini, hata muhusika mwenyewe anasema alisukumizwa ndani
Sio kweli JK aliingia na jina la mdogo wake, mr niguse ninuke, mpasuko ukawa mkubwa kuokoa jahazi mr Ben akapendekeza jamaa aliepo, hii inaitwa tukose wote kati ya tim mamvi na timu niguse.
 
Erythrocyte,
Nchi hii kuna uhaba wa watumishi kuliko unavyojua.tuchukulie kwa walimu tu. Waziri wa elimu akiwa kahama siku ya walimu.aliseomewa taarifa kwamba Kahama ina upungufu wa walimu 700 kwa sekondari tuu.tufanye wastani kila halimashauri ina upungufu wa walimu 700 kwa msingi na sekondari. Tuna halmashauri 185 * 700=129500.minmum,hao n walimu wanaohitajika. Lakini mamlaka zinasema walimu wanatosha.
 
Sio walimu tu kila sekta haina ajira,tena kuna mashule kibao hayana walimu..lkn serikali bd kila siku inadanganya kuwa walimu wametosha

Ye anachoshangaa nini km si unfki, ndo wananch wanateseka ivyo ...

Akae kimya tu, tuone mchezo utaishia wp
 
Nchi hii kuna uhaba wa watumishi kuliko unavyojua.tuchukulie kwa walimu tu. Waziri wa elimu akiwa kahama siku ya walimu.aliseomewa taarifa kwamba Kahama ina upungufu wa walimu 700 kwa sekondari tuu.tufanye wastani kila halimashauri ina upungufu wa walimu 700 kwa msingi na sekondari. Tuna halmashauri 185 * 700=129500.minmum,hao n walimu wanaohitajika. Lakini mamlaka zinasema walimu wanatosha.
Unadhani viongozi hawajui hilo?Wanalijua sana.

Ndio maana watoto wao hawasomi hizo shule za serikali(zenye upungufu wa walimu) wanasoma zao huko shule za private.
 
Back
Top Bottom