Mzee Kikwete akanusha kuwepo kwa Mawaziri wanaotafuta fedha na mikopo nje ya nchi kumg'oa Samia Uchaguzi 2025

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
TAFAKURI YA KAULI YA RAIS MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIKWETE ALIYOITOA KWENYE MKUTANO MKUU WA 10 WA CHAMA CHA MAPINDUZI 8/12/2022 DODOMA

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amemtaka Mh. Rais Samia Suluhu Hassan asisikilize porojo zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa kuna mawaziri wanaokwenda nje ya nchi kukopa na kutafuta fedha za kumng’oa Rais Samia mwaka 2025, Mh. Kikwete amekanusha kwamba maneno hayo sio ya kweli na ni uongo na upuuzi mtupu.

1. Ninaona kama Mh Kikwete anajaribu kutaka kumfundisha kazi Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi namna ya kushughulikia matatizo ndani chama. Rais aliyeko madarakani anavyo vyombo vyote vya uchunguzi vyenye kuweza kubainisha ukweli au uongo wa kauli ya Mheshimiwa Albert Chalamila juu ya mawaziri kwenda nje ya nchi kukopa matrilioni ya fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2025 na kuchukua hatua stahiki.

2. Nchi yetu inavyo vyombo vya dola kama Usalama wa Taifa, TAKUKURU, Jeshi la Polisi, CAG nk. ambavyo vimepewa mamlaka kisheria kufanya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali na kubaini ukweli wake. Mh Kikwete yeye ni nani hadi atoe taarifa za kiuchunguzi mbele ya umma na kwa Mh Rais kuhusiana na mawaziri kwenda kukopa nje na kujiimarisha kuelekea 2025

3. JK ni mstaafu hana cheo chochote serikalini wala kwenye Chama anajuaje kama hadi sasa hatua hazijachukuliwa kwa Mh. Albert Chalamila juu ya kauli yake kuhusiana na mawaziri

4. Ni kwanini JK ameelekezea lawama nzito upande mmoja tu wa mtoa kauli Mh Albert Chalamila hadi kuagiza achukuliwe hatua na Chama na sio wale waliotajwa na RC Chalamila kuhusika na njama za kumhujumu Rais aliyeko madakarani

5. Je Mheshimiwa Mstaafu Jakaya Kikwete kwanini atumie nguvu kubwa kukanusha kuwepo kwa mawaziri wanao tafuta fedha na mikopo nje ya nchi kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka 2025 na kumbwaga Rais aliyeko madarakani Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Kwa vyovyote vile mawaziri waliotajwa na Chalamila, Mzee Kikwete atakuwa anawajua kwa majina na wizara wanazoziongoza ni washirika wake katika kupanga njama za kumtoa Rais Samia 2025 ndio maana povu jingi likamtoka kuwatetea hadharani bila aibu.

6. Rais Mstaafu Kikwete anamwambia Rais Samia kwamba kwenye utawala wake hakukubali upuuzi huo, Lakini watanzania wote tunakumbuka nchi alivyoitumbukiza kwenye matatizo mengi kama uendeshaji duni wa chama na Serikali mpaka ikafikia hatua hatua ya KUJIVUA GAMBA ili kuinusuru CCM, mikataba mibovu kama Richmond, IPTL, Bandari ya Bagamoyo na Escrow mbayo ilisababisha hasara kubwa kwa nchi yetu lakini pia tunakumbuka bandari ya Dar es Salaam JK alivyoikabidhi kwa GSM hadi kusababisha mfarakano mkubwa na wafanyabiashara hadi watu kumwagiwa tindikali. leo Mzee Kikwete anapata wapi kiburi cha kutamka hayo hadharani kwamba jkwenye utawala wake hakukubali upuuzi huo.

7. Kwanini Rais JK badala ya kumuombea mema Rais wetu yeye anamtabiria mabaya kwa kauli yake eti labda mambo yaharibike sana kuanzia sasa na wakati huo ndio anaweza kujitokeza mwana CCM mwingine kugombea urais. Rais wetu anaongoza nchi vizuri na analeta maendeleo kwa kasi, je hayo mambo anayotarajia yaharibike ni yapi na kwaninji hakuyataja?

8. Tunaomba Mh Jakaya Mrisho Kikwete amuache Mama yetu Samia Suluhu Hassan aendelee kuiongoza nchi nchi yetu kwa misingi ya haki bila ubaguzi wala udini.

9. Endapo JK analo jambo la kushauri alipeleke kwa utaratibu unaofahamika na Mama atalipokea kwa kuwa Mama yetu ni msikivu na mnyenyekevu tofauti na yeye JK ambaye wakati wa utawala wake aliwafukuza marais wastaafu Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ili afanye maamuzi atakavyo.


 


Kimepasuka Kimepasuka Kimepasuka Kimepasuka Kimepasuka Kimepasuka Kimepasuka Kimepasuka

 
"akukanusha" ndio neno gani? Katika kupitia kwako shule zote hizo, ulishawahi kufundishwa neno hilo? Nilivyoliona tu, sijajisumbua hata kusoma kilichomo.
 
Labda yeye mstaafu anavyo vyombo vya uchunguzi mahiri zaidi ?? Hapo Alichemsha kwa lugha ya mtaani halafu amesababisha yawepo maswali mengi yasiyo na majibu!! Ukichanganya na Maneno ya Mzee Makamba unapata wasiwasi kidogo ! Ndo maana wengine wakauliza je wanamtisha Mkuu ??!!!
 
Hivi JK yeye mwenyewe amejuaje kuwa ni uongo? Na wakati huo huo anasema eti Chalamila aitwe kwenye vikao vya nidhamu awataje.
Kama ni mkweli, angeshikilia hapo pa kuitwa awataje na siyo kukanusha na kusema kwamba ni uongo.
 
Ila kuna watu hamna kazi aisee, Haki ya Mungu tena! Sasa kale kaushauri kana uhusiano gani na kuingilia madaraka ya raisi, eti anampangia. Hivi ni leo tu kiongozi kama raisi anashauriwa?!!!! Mbona hili jambo lipo miaka na miaka.
Wakati wa ziara za maraisi mbona wakuu wa mikoa, wilaya n.k huwa wanasema mara nyingi tu, 'mh. Rais, hawa wapinzani niachie mimi....n.k.

Aina hiyo ya uongeaji nimepata kuisikia kutoka kwa viongozi mbalimbali wa serikali, dini, mashirika n.k wakitoa kwenda kwa raisi......na marais wote niliowawahi kipindi changu nimeshuhudia jambo kama hilo. Shida ipo wapi kwa Kikwete?!!!!!! Mbona mmemsakama hivi mzee wa watu?!!!! Sasa hapo amempangia nini Raisi zaidi ya ushauri tu wa kawaida wenye kumsihi asianze kupatwa na wasiwasi na wasaidizi wake?!!!
 
Chalamila hakutaja jina la Waziri ila kitendo cha JK kukanusha kwamba hawapo maana yake anawajua kwa majina waliolengwa na Chalamila
Na inaelekea Kweli wapo !! The guilties are always afraid Wanasemaga wataalam wa vitengo !! Ngoja tuone hii jigsaw puzzle !!
 
Labda yeye mstaafu anavyo vyombo vya uchunguzi mahiri zaidi ?? Hapo Alichemsha kwa lugha ya mtaani halafu amesababisha yawepo maswali mengi yasiyo na majibu!! Ukichanganya na Maneno ya Mzee Makamba unapata wasiwasi kidogo ! Ndo maana wengine wakauliza je wanamtisha Mkuu ??!!!
Nafikiri alitumia uzoefu kutokana na yaliyomkuta way back 2020, kama ulimsikia vema alisema vizuri tu kuwa kila unapokaribia uchaguzi basi maneno maneno huwa meeengi......mara hv mara vile. Akatoa mfano kabisa wa jinsi gani mtu fulani aliyejiita 'mwanaharakati huru' alivyozusha kila aina ya uongo kipindi hicho na jinsi gani kiongozi mkuu, kutokana na nguvu zako labda ndani ya chama na nchi labda, unavyoweza kusababisha mtafaruku ikiwa utayachukulia juu juu na kwa pupa maneno kama hayo. Leo, kwa kutumia experience hiyo, anamshauri aliyopo madarakani. Tatizo nini hapo waheshimiwa?!!!!!!!
 
Nafikiri alitumia uzoefu kutokana na yaliyomkuta way back 2020, kama ulimsikia vema alisema vizuri tu kuwa kila unapokaribia uchaguzi basi maneno maneno huwa meeengi......mara hv mara vile. Akatoa mfano kabisa wa jinsi gani mtu fulani aliyejiita 'mwanaharakati huru' alivyozusha kila aina ya uongo kipindi hicho na jinsi gani kiongozi mkuu, kutokana na nguvu zako labda ndani ya chama na nchi labda, unavyoweza kusababisha mtafaruku ikiwa utayachukulia juu juu na kwa pupa maneno kama hayo. Leo, kwa kutumia experience hiyo, anamshauri aliyopo madarakani. Tatizo nini hapo waheshimiwa?!!!!!!!
Ni kwanini JK ameelekezea lawama nzito upande mmoja tu wa mtoa kauli Mh Albert Chalamila hadi kuagiza achukuliwe hatua na Chama na sio wale waliotajwa na RC Chalamila kuhusika na njama za kumhujumu Rais aliyeko madakaran
 
Hao mawaziri ni Mwigulu, January Makamba,Nape Nauye,iko wazi kabisa,sema Chalamila kagusa watoto pendwa,sidhani kama ataendelea kuwa RC tena,

Hii nchi msemakweli ni adui mkubwa wa walamba asali,naona Samia kapewa maelekezo na boss wake kikwete lililobaki ni utekelezaji wa kutengua Chalamila
 
Ni kwanini JK ameelekezea lawama nzito upande mmoja tu wa mtoa kauli Mh Albert Chalamila hadi kuagiza achukuliwe hatua na Chama na sio wale waliotajwa na RC Chalamila kuhusika na njama za kumhujumu Rais aliyeko madakaran
Eh, kumbe ameagiza Chalamila achukuliwe hatua?!!!!! Hilo nilikuwa sijasikia, sijui alilisema pale au pembeni?
Hivi zaidi ya kutoa angalizo tu kidogo kuna jingine kalisema hadi unasema 'ameelekeza lawama nzito' kama vile alinena hayo kwa muda mreefu?!!!!
 
Back
Top Bottom