Mzee Juma Duni Haji, wanaotaka Mbowe asote gerezani ni Washirika wa Chama Chako

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,644
218,093
Mzee Juma Duni Haji kwanza Shikamoo , waendeleaje na hali yako mzee wangu ?

Nimekusikia Mzee ukizungumzia sakata la Freeman Mbowe , umesema ukipata nafasi ya kusaidia Mbowe kutoka gerezani utafanya hivyo bila kujali kama UTATUKANWA , na ukaenda mbali kwa kudai kwamba wanaotaka Mbowe aendelee kusota jela wao wako Ulaya wakitumbua maisha mazuri .

Tunakushukuru sana Mzee wetu kwa huruma yako uliyoionyesha kwa Mbowe , kwa kujitoa kwako kutaka "usaidie" atoke jela, Tunakuombea kwa Mungu akulipe kwa moyo wako huo , Amina.

Bali tunachokutaarifu ni kwamba Freeman Mbowe hatotoka jela kwa kujidhalilisha , hatotoka gerezani kwa kumpigia magoti yoyote kwa TUHUMA ZA UONGO ZA UGAIDI ALIZOBAMBIKWA NA WATAWALA WAOGA wanaoogopa Katiba mpya , wewe Mzee Duni unawafahamu waliombambikia kesi ya Uongo Mbowe, hao ndio wanaotaka Mbowe afie jela, hawa ndio waliokubambikia wewe mwenyewe na wenzako KESI YA UHAINI miaka ya nyuma, usisahau Baba yako mzazi alivyopigwa Kibao Mahakamani hadi akaanguka alipokuwa anakuja kukusalimia , na tangu siku hiyo hukumuona tena Baba yako hadi alipokufa na kuzikwa , Mzee hawa ndio ambao hawataki Mbowe atoke jela , usiwasingizie walio Ulaya .

Wasiotaka Mbowe awe Huru ni hao CCM ambao wewe na chama chako cha ACT mmeunda serikali ya Mseto Zanzibar , kwamba wewe na wenzako ni sehemu ya serikali inayomkandamiza Mbowe, na sasa mmekubaliana kudanganya Dunia kwamba Mtaunda TUME HURU BILA KATIBA MPYA , Yaani bila Katiba Mpya Mahera au Jecha watakuwa wanaongoza TUME HURU ZA UCHAGUZI ! Hiki ni kituko cha Karne ! yaani Katiba ile ile inayomruhusu Mwenyekiti wa ccm kuteua na kufukuza atakavyo eti leo tuiundie Tume Huru !

Japo nimeandika mengi lakini lengo langu ni kukumbusha kwamba WANAOTAKA MBOWE AFIE JELA NI HAO HAO WASHIRIKA WENU WA MADARAKA , WALA SI WALE UNAODAI WAKO ULAYA , Kwa Umri ulionao na madhira uliyopitia hatukutegemea upotoshaji wa namna hii kutoka kwako , BADO NAAMINI ULINUKULIWA VIBAYA .

Wabillah Tawfiq
 
Mama muachie Mbowe maisha yaende ulidanganywa, wachaga hatudanganyiki kwa kujikosea kwenye machief wasiotambulika kutafuta huruma ya wachaga. Hio mikoa mingine Hakuna machief hadi uje uchagani.
 
Mzee Juma Duni Haji kwanza Shikamoo , waendeleaje na hali yako mzee wangu ?

Nimekusikia Mzee ukizungumzia sakata la Freeman Mbowe , umesema ukipata nafasi ya kusaidia Mbowe kutoka gerezani utafanya hivyo bila kujali kama UTATUKANWA , na ukaenda mbali kwa kudai kwamba wanaotaka Mbowe aendelee kusota jela wao wako Ulaya wakitumbua maisha mazuri...
Acha ujinga wewe bibie mwenzenu anataabika huko nyie mko nje halafu manamwambia asitoke kwa huruma ? Shenzi kabisa mnajuwa ana miss ipi familia yake? Kafanya ugaidi halafu hamtaki ahurumiwe atoke? Yaani mnategemea kushinda kesi ili atoke kwa ushindi?

Sahauni huyo msipokuwa makini anafungwa nguo imewavuka chutameni mkilazimisha kutembea mnaonyesha matupu yenu watu wanawacheka tangu lini ukainshinda serikali ? Lisu kaolewa huko na lema kaolewa huko halafu wanapiga kelele asitoke wakati wao wanakata vitunguu kuwapikiwa waume zao
 
ACHA UJINGA WEWE BIBIE MWENZENU ANATAABIKA HUKO NYIE MKO NJE HALAFU MANAMWAMBIA ASITOKE KWA HURUMA ? SHENZI KABISA MNAJUWA ANA MISS IPI FAMILIA YAKE? KAFANYA UGAIDI HALAFU HAMTAKI AHURUMIWE ATOKE? YAANI MNATEGEMEA KUSHINDA KESI ILI ATOKE KWA USHINDI? SAHAUNI HUYO MSIPOKUWA MAKINI ANAFUNGWA NGUO IMEWAVUKA CHUTAMENI MKILAZIMISHA KUTEMBEA MNAONYESHA MATUPU YENU WATU WANAWACHEKA TANGU LINI UKAINSHINDA SERIKALI ? LISU KAOLEWA HUKO NA LEMA KAOLEWA HUKO HALAFU WANAPIGA KELELE ASITOKE WAKATI WAO WANAKATA VITUNGUU KUWAPIKIWA WAUME ZAO
Kafungwa Mbowe unalia wewe , kulikoni ?
 
Haya maharagwe umekula wapi mpaka uje kuharisha hapa?
 
Nakumbuka hao siyo mapapai hawaozi- babu Duni tatizo siasa chafu zile zile siyo political exiles. Same old shit a different day.
 
Kumbe babake Duni alipigwa kofi mahakamani hadi akaanguka, kama huyu mzee ameweza kumsaliti baba yake marehemu, ndio maana wanaendeleza usaliti wao kwa wapemba waliopigwa na kuumizwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Baba yake alikwenda mahakamani kufuatilia kesi ya mwanawe ambaye ni Juma Duni, kama nitakuwa sahihi askari alimwambia jambo lakini hakuweza kusikia kwa sababu mzee alikuwa na matatizo ya kusikia.

ndipo polisi akampiga baba yake Juma Duni.
 
ACHA UJINGA WEWE BIBIE MWENZENU ANATAABIKA HUKO NYIE MKO NJE HALAFU MANAMWAMBIA ASITOKE KWA HURUMA ? SHENZI KABISA MNAJUWA ANA MISS IPI FAMILIA YAKE? KAFANYA UGAIDI HALAFU HAMTAKI AHURUMIWE ATOKE? YAANI MNATEGEMEA KUSHINDA KESI ILI ATOKE KWA USHINDI? SAHAUNI HUYO MSIPOKUWA MAKINI ANAFUNGWA NGUO IMEWAVUKA CHUTAMENI MKILAZIMISHA KUTEMBEA MNAONYESHA MATUPU YENU WATU WANAWACHEKA TANGU LINI UKAINSHINDA SERIKALI ? LISU KAOLEWA HUKO NA LEMA KAOLEWA HUKO HALAFU WANAPIGA KELELE ASITOKE WAKATI WAO WANAKATA VITUNGUU KUWAPIKIWA WAUME ZAO
Umeandika upuuzi!Halafu jifunze kutumia herufi ndogo,uandishi wa namna hii ni sawa na uchafu mahala pasafi!
Mbowe ni mtuhumiwa tu,ila wewe umeshamuhukumu kwamba kafanya ugaidi!Ni kazi ya mahakama kutenda haki!Sasa unaposema kuwa kesi yake hawezi shinda kwasababu hawezi kuishinda serikali ni kama unakiri kuwa kesi ni ya mchongo!
Msisahau Mungu yupo!
 
Hii haiwezi kuwa sababu ya kuacha kumwambia ukweli huyo mzee, siku zote heshima lazima ilindwe, mtu akiichezea heshima yake maana yake anakuwa tayari kuipoteza.
 
Umeandika upuuzi!Halafu jifunze kutumia herufi ndogo,uandishi wa namna hii ni sawa na uchafu mahala pasafi!
Mbowe ni mtuhumiwa tu,ila wewe umeshamuhukumu kwamba kafanya ugaidi!Ni kazi ya mahakama kutenda haki!Sasa unaposema kuwa kesi yake hawezi shinda kwasababu hawezi kuishinda serikali ni kama unakiri kuwa kesi ni ya mchongo!
Msisahau Mungu yupo!
Kwani hawajui kama kuna Mungu? Kulikuwa na mtu kiburi na katili kumshinda Mwendakuzimu? Yuko wapi leo?
 
Back
Top Bottom