Mzee JK NY: Vipi Mkutano Wa Rais New York?

Apr 27, 2006
12,622
1,235
Mkutano wa rais wetu Mzee JK, jana na wa-Tanzania pale New York nyumbani kwa balozi, nafikiri ilikuwa ni moja ya the finest moment ya urais wa rais JK, best perfomance by our president, best makaribisho kwa wananchi wote nyumbani kwa balozi, chakula safi baada ya hotuba na maswali,

lakini niseme one thing, jamani wazee wa NY vipi? Maswali kama watu waliolala usingizi? What a joke, eti rais vipi hospitali ya Musoma bado inajengwa au vipi? He! are you serious haya ndio maswali ya kumuuliza rais wako? Eti umeme wa Solar ufutiwe kodi na wakati sisi wabongo wote tunajua kuwa siku zote hauna kodi?

Wazeee wa NY mmenishangaza sana, bravo mzee Jasusi kwa swali lako dogo lakini makini kwa manufaa ya wakulima wadogo wadogo,

Je Wazeee wangu mnasemaje?, lakini mimi ninadhani kuwa ilikuwa one of the best perfomance by our president na ubalozi wetu pale chini ya mzee Mahiga!
 
bwana Es tafadhali tuelezeni zaidi yaliyomo maana hatukuwepo huko sasa mtu kama mimi nashindwa ku comment lolote .Kama watu walikuja ki shabiki pale na wakashindwa kuuliza maswali basi hakuna la kusema .Au kama kuna maelezo zaidi tuelezeni hapa ili tujenge hoja ya mjadala .
 
Sikusikia issue ya mapanki wala madini, ilikuwa very depressing hata kuyaongelea maswali ya kitoto, huku wananchi wakitaka kuvunjana miguu kugombea kuuliza ujinga!

Rais ameongelea mambo yote muhimu kuanzia barabara, maji, umeme, ujambazi, dual citizenship, wananchi walioko nje kupiga kura kwenye uchaguzi nyumbani wa siasa, yaani ali-cover kila kitu, sasa kilichotakiwa ni creativity ya maswali kutokana na aliyoyasema, hakugusa mambo mawaili rushwa, na madini, to my shock, jamaa anasema mbona maji hayatoki Temeke na zamani hayajawahi kukatika! are you kidding me! In the end Mzee wangu JK was a hero, huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu zote,

kumbe na huku majuu ni sawa tu na sisi wapiga kura wa bongo wa 80%?
 
Wewe Mzee ES ulikuwepo, mbona hukuuliza swali la nguvu? Watanzania wengi ni waoga sana. Tazama hapa kwenye forum, karibu kila mtu anaficha jina lake. Wanatoa vizingizio vingi, lakini sababu ya kweli ni woga.

Sasa hapo NY mbele ya wahusika wenyewe, JK, Mahiga etc, wote mlifyata mkia.

Augustine Moshi
 
Nadhani yeye alikuwa kwenye msafara.(Mzee Es nisahihishe kama nimekosea)
Na ingekuwa kioja mgeni kuuliza maswali angali wenyeji wapo.
 
Ni ukweli ulio wazi kwamba asilimia kubwa ya wananchi wa Watanzania walioko nje ni wazamiaji na shule zao ni ndogo sana . Idadi nyingine inafuatiwa na watoto wa kubwa ambao nao wanaona Tanzania ni moto sasa wako ama US ama UK au Canda wengi wao hivyo .Vihiyo ni wengi na kazi ni ushabiki .Hao ukitaka kuwaona ingia youngafrican.com nk .Hao ndiyo wana mwaga maparty kila ugenini hawaijui Tanzania na hawana tofauti na wananchi wa kijijini kwangu ambao wanaamini ni CCM tuuuuuu. Hao hawawezi kujenga hoja ni waoga sana na wanafiki .Sishangai maswali ya aina hiyo kuulizwa maana uwezo wa kufikiri pia una kikomo .Walikuwa pale kuoiga picha na kuweka historia kwamba wamemuona JK etc.Na yeye anajua mahala pa pakwenda JK akijua kuna watu makini hagusi .JK hawezi kutaja rushwa maana aliingia madarakani kwa rushwa na serikali yake imejaa wala rushwa hadi wapewa nafasi ya kucha kula na kuiba .Hawezi kutaja madini maana kesha ona moto wa kupitia mikataba kambi ya mtandao ni wachafu na labda yeye mwenyewe pia sasa hatakuwa na la kusema lazima aguse issues ambazo si contentious kiasi hicho .
 
Mzee Aljazeera,

Heshima yako mkuuu, huyo Moshi anajua hilo, na ninarudia kuwa ilikuwa ni aibu ya mchana kweupe!, Tana tuliambiwa kuwa kuna wananchi walitoka mikoa mbali mbali kuja kumuona JK, lakini maswali hakuna!
 
ES,

Naomba kukueleza kitu kimoja ndugu yangu, watu wengi wanaenda pale kujipalilia ulaji, "angalau rais anione", mimi ni profesa wa maji pale chuo cha OLAF, naomba kuuliza mbona maji hayatoki temeke?", swali kama hilo ni la kumuarifu rais kuwa u profesa wa maji ..nakufikirie..

Huo ni mfano tu, ila wadanganyika tu wavivu wa kufikiri.

FD
 
Mzee ES,
Summary yako muruwa. Lakini unajua kitu kimoja katika vikao vya hadhara kama ile hafla ni kwamba huwezi kujua nani atapewa microphone na anataka kuuliza nini. Nilipenda lile swali la yule mama wa Tarime ambaye baba yake atahamishwa shambani kwake ili mwekezaji achimbe dhahabu pale. Ningekuwa na nafasi ningependa sana kulifuatilia kwa sababu naona hapa serikali inafanya kosa kama lile lile la Bulyanhulu. Hawa watu wameishi pale maisha yao yote, kwa nini wasipewe royalty kwa yale madini yatakayochimbwa? Wanapohamishwa wanapewa fidia gani? Hili ni jambo ambalo nafikiri serikali inahitaji kuliangalia upya. Kuna school mate wangu mmoja kule Illinois ambaye waligundua natural gas katika shamba la baba yake. Kampuni ilimlipa fidia na royalty ya kuchimba ile gesi na mpaka sasa anakaa tu akisubiri hundi yake. These people deserve the same ama sivyo tutabaki kichekesho tu cha kusema Tanzania is one of the world's greatest gold producers yet her people are the poorest. Kama unaweza kumfikishia JK hiyo they need to look into it again.
 
Fikira duni
hata huyo ES mie sidhani kama anatofauti na hao waliokwenda kujionyesha na hata ukifutilia makala yake utaona ni kujitia ujuaji tu.
nakupa mfano kuna mada sensitive ya pesa za mengi tunataka data. yeye kaja kutuwekea namba za cm za Kingunge, mkapa, Migiro na msururu kibao wa mawaziri.
tuchukulie aliombwa namba hizo lakini waombaji si wanazo email adress zao? au private box?
kingine kaweka namba ya JK ambayo kila mtu anaijua tena alipoingia tu IKULU aliacha kuitumia namba hii ilikuwa maalum kwa ajili ya kampeni na alikaa nayo sana foreign.
sasa hata kama angekuwepo hapo mkutanoni na kupewa na nafasi ya swali angeuliza pumba. nadhani angeomba apewe namba ya Shein.
hizi ni forum za kuleta vitu vizito lakini kama kila mtu anaweka namba ya Michael Jackson. Beckham n.k tutakuwa tunapoteza muda.
pia wanaohitajia namba za viongozi hizo alizoweka Es ziko website ya Bunge. na wengine waliomba zifutwe kwa kero za akina sisi.
nina Doubt hata huyo aliyesema yumo kwenye msafara kwani huyu bwana yuko marekani muda aliingia vipi kwenye msafara? au ndio usaani
 
Mzee Es
Umesema JK alisema kiume sawa . Lakini kuondoka pale akiwa hero naomba ufafanue ni what way .Watu kwa mfano Jasusi amesema na mimi nilikuwepo kwamba Mama wa Tarime kalia na wazazi kuondolewa ili mgeni achukue ardhi .Unaonaje majibu ya JK ? Hakuonyesha hata kujali wala utu .Alisema kwa kifupi kwamba kama kuna madini basi tutawatafutia mahala pa kuishi ili madini yachimbwe . Ina maana JK hajuai habari zam Royalty na na Compensation? Tuache Mzaha Jk he is not serious .

Unakumbuka Mzee JK ametetea habari ya ndugu yake Msabaha na wamarekani wale ambao sasa wameingia kuchota na kutuumiza wakati walisha kataliwa huko nyuma? Kupiga picha na Bush na Clinton kutoa msaada wa umee jua tutaumia baadaye is not pure msaada mambo yake ni haya .Nasema pale JK hakutoka hero ila walio kuwepo nao walitaka kupiga picha naye tu na si watu serious ama wanakua kwa mrija .

What was the point of mtoto wa mwema kusimama na kuuliza juu ya usalama na ujambazi wakati Rais alisha ongelea hilo ? Kama si kumjengea baba yake jina na kujitambulisha kwa rais kwamba ni mtoto wa mwema ?

Watanzania tuamke tunaenda kubaya na JK hajali kabisa .Ameanza kusifiwa na wakubwa kama Bush basi ndani tutaumia na hatutasikilizwa kamwe.Hali ya umeme ni mbaya sana na hata Uchimi wa Nchi unayumba maana hakua umeme na mazingira yanachafuka na watu wanaugua hovyo Dar kila kona ni tukutukutuku jenerata .JK aliongelea swala lile kama mzaha na watu wakapiga makofi jamani kweli ??/
 
Unajua ni waste of time kukujibu, wewe ni wewe na mimi ni mimi kilio chako hakiwezi kubadili kitu bro, inaonekana una hasira ambazo siwezi kukusaidia kuzitatua, siwezi kukosa usingizi kwa ajili ya hela za Mengi ambaye sio kiongozi wa CCM wala upinzani, nitakosa usingizi kwa ajili ya IPTL ndio maana niko njiani kukusanya signatutres ili kulifikisha hili suala linapotakiwa, na kwa taarifa yako kuna wajumbe humu wanaoelewa hilo na kujihusiha nalo, so far tunazo sahii 20, zinatakiwa 250, ili suala hilo liende panapotakiwa je unataka kujiunga uletewe makaratasi badala ya kulia lia tu humu kwenye forum?

hayo makelel yako ya mlango hayazuiii wananchi ndani kulala, Mengi sio tatuizo la nchi yetu labda la kwako wewe binafsi, kwangu mimi Mengi ni great mwananchi wa bongo na a hero wa nchi yangu, FULL Stop, I dore him so much kwamba hata akiiba nitampa free pass maaana kazi aliyoifanya ya kutoa ajira na kuwalipa wananchi mshara ambao hata serikali yetu haiwezi sio ndogo!

Na hizo namba kuna wanozihitaji na hasa mzee Mwanakijiji kwa jli ya shughuli zake, hiyo namba ya JK bado inafanya kazi ila huwa anaifungulia masaa ya usiku sana, na nido maana nikasema kama ina tabu kuna right hand man wake ambaye anaweza kukuunganisha wakati wowote kutegemea na shida yako, otherwise wewe hata upige mpaka machozi ya damu yakutoke huwezi kuongea na rais wa jamhuri bila ya kuunganishwa, kijana kuna unayoyajua na kuna usiyoyajua, sasa unayoyajua wewe sio kwamba kila mtu anayajua na usiyoyajua kubali usijifanye unajua wakati hujui, kwenye hili la namba hujui lolote bro!!

Mengi is my hero!
 
Mugishagwe said:
Ni ukweli ulio wazi kwamba asilimia kubwa ya wananchi wa Watanzania walioko nje ni wazamiaji na shule zao ni ndogo sana . Idadi nyingine inafuatiwa na watoto wa kubwa ambao nao wanaona Tanzania ni moto sasa wako ama US ama UK au Canda wengi wao hivyo .Vihiyo ni wengi na kazi ni ushabiki .Hao ukitaka kuwaona ingia youngafrican.com nk .Hao ndiyo wana mwaga maparty kila ugenini hawaijui Tanzania na hawana tofauti na wananchi wa kijijini kwangu ambao wanaamini ni CCM tuuuuuu. Hao hawawezi kujenga hoja ni waoga sana na wanafiki .Sishangai maswali ya aina hiyo kuulizwa maana uwezo wa kufikiri pia una kikomo .Walikuwa pale kuoiga picha na kuweka historia kwamba wamemuona JK etc.Na yeye anajua mahala pa pakwenda JK akijua kuna watu makini hagusi .JK hawezi kutaja rushwa maana aliingia madarakani kwa rushwa na serikali yake imejaa wala rushwa hadi wapewa nafasi ya kucha kula na kuiba .Hawezi kutaja madini maana kesha ona moto wa kupitia mikataba kambi ya mtandao ni wachafu na labda yeye mwenyewe pia sasa hatakuwa na la kusema lazima aguse issues ambazo si contentious kiasi hicho .

Heshima yako Mzee.

Inawezekana ni kweli kwamba asilimia kubwa ya Watanzania walio nje ni wazamiaji na shule zao ni ndogo (japo sijui kama "nje" unayozungumzia ni South Afrika,Uganda au U.S of A,na pia sina hakika ya wapi ulipopata takwimu hizo).Mie ni mtoto wa mlalahoi (ndio asili ya jina nalotumia) na nimekuja UK kwa kushinda scholarship ya kusomea Master na jitihada zangu binafsi ziliniwezesha kushinda schlarship nyingine hapa nilipo ya kusomea PhD.Nawafahamu akina Watanzania wengine ambao ni wasomi halisi (eg Dr Mbogoni,Prof Lwakabamba,Prof Alwiya Omar,Dr Masangu Matondo,Dr Rose Lugano,Dr Leonce Lushubirwa,etc bila kumsahau Prof Tibaijuka) na baadhi yao wanaitwa "wazamiaji" kwa vile tu wameamua kuachana na ubabaishaji wa taasisi zetu za elimu nyumbani na kuja kujitafutia maisha huku ughaibuni.Huwezi kuwalaumu kwa vile mkono shurti uende kinywani.

Kwa uzoefu wangu,watoto wa vigogo huwa hawako serious na masomo kama sie tunaotoka familia za kilalahoi ambao kwetu nafasi ya kuja huku ni bahati ya mtende kuota jangwani.

Back to the point.Nadhani wakati mwingine kuna kijitabia cha kuwategemea watu flani wafanye vitu kwa niaba yetu.Sijui Mugishgwe uko wapi lakini naamini kama ulihudhuria mkutano huo ulipaswa kuuliza maswali yanayokukera kuliko kutegemea flani aulize them umlaumu.Nadhani kila mtu anafanya kitu kulingana na priorities zake mfanyaji.Mtoto wa kigogo akiuliza swali kwa rais sanasana atamtetea baba yake au kumpatia ujiko rais kwa kumteua baba yake.Mie mlalahoi ntauliza swali kulingana na mateso wanayopata wazazi wangu walalahoi kule nyumbani.Ni kichekesho kumtegemea mtoto wa kigogo aulizie mgao wa umeme wakati hajawahi kuona koroboi nyumbani kwao,au mtoto wa mwizi wa madini yetu ahoji suala la mikataba ya madini (swali la madini linategemewa kutoka kwa yle ambaye pengine kaka au mdogo wake ni miongoni mwa "boys of mererani")

Naafikiana na baadhi ya observations zako eg kuhusu youngafrican.com lakini kama nilivyochangia kwenye hoja kuhusu topic ya matatizo ya Taifa letu,kuna uhaba wa uzalendo miongoni mwa watanzania.Wachangiaji wakubwa katika misaada ya kuikomboa nchi yetu ni watu wenye uwezo kifedha na hawana uhusiano wowote na Tanzania lakini wanatuonea huruma.Laiti watoto wa vigogo wangekuwa wazalendo wangepaswa kuuliza maswali ya maslahi ya taifa na sio yao binafsi.Na kwa wale waliokaa kimya bila kuuliza maswali au hawakwenda kabisa kwenye mkutano kwa vile tu walitarajia flani na flani wangeuliza maswali yaliyokwenda shule,all I can same is shame on them bcoz they've let us down
 
Mzee Jasusi,

Nimekusikia, na ninarudia tena bravo kwa maswali yenye uhakika, kuhusu hilo la wanachi kuhamishwa ninajua kuwa ki-sheria serikali yetu ina haki ya kuwahamisha wananchi, au kuchukua ardhi yoyote ile ambayo inaonekana kuwa itakuwa na faida kwa serikali, na kwamba ardhi yoyote ndani ya nchi yetu, kimsingi ni mali ya serikali,

na pia kuna Clause kwenye hiyo sheria inayoruhusu wananchi binafsi kufaidika na ardhi yao ikibidi, ikiwa na maana ya huyo jamaa yako unayemsema, ama sivyo poa litafika ila ninahitaji utafiti kidogo, ili kuwa na FACTS kwanza!

Otherwise bravo Mzee!

Mzee Shughuli,

Heshima yako mkuu, kwa kweli ninasikitika kuwa Mzee Boaz hakuwepo pale, maana yule ndiye mwenye maswali ya kweli siku zote, ni lazima ukubali kuwa kwenye ule mkutano kulikuwa na wananchi wengi wasioelewa what is going on, ninakumbuka jinsi walivyokuwa wakimshangilia JK kwa maneno ambayo yalihitaji uafaanuzi, kwa mfano suala la umeme, ndugu zangu nyinyi miloko nje siadhani kama mnaelewa kinachoendelea huko nyumbani na suala hili, makelele ya generator, moshi kwa wingi yaani yalioko nyumbani ni mateso, lakini hakukuwa na swali la kimsingi kwa hilo! Na nikaona akishangiliwa kwa kutaja hesabu ambazo sijui kama wananchi wanazielewa?

Elimu vipi hakukuwa na swali kabisaaaa!, vipi rushwa especially pale aliposema kuwa Mkapa amefanya kazi ya kuwatoa mbu na mbung'o ndani ya nyumba, si lingetokea swali la nyongeza kuwa je vipi awamu ya sasa na suala hilo?

Kuhusu Mwema, kwa kweli sikumuelewa na sikujua kuwa ni mtoto wa Mwema ila ninakumbuka akisema hilo jina, sina uhakika kuwa aliuliza swali au alikuwa ana-comment au ndio kama unavyosema alikuwa anampalilia baba yake,

kuna kijana aliyeuliza mwisho ambaye JK alisema tumuite na kumuingiza ndani aonane naye personal, huyo ninampa credit kidogo lakini angalau angeyasema aliyoyasema kule ndani pale nje,

Mzee wangu ninakubali kuwa kuna tatizo la seriousness, lakini hilo lilipaswa kusimamiwa na wananchi pale kwenye mkutano kama wakakti ule Mkapa alipoendeshwa mchaka mchaka na wananchi, na hasa yule kijana wa JM ambaye mpaka leo Ikulu kuna historia yake alivyomrusha juu mzee BM, mpaka akagoma hata kula kwa hasira na kupanda gari lake na kuondoka,

Siku nyingine wananchi wanahitaji kujitayarisha kikamilifu, na wananchi wasiokuwa na point wajifunze kuwaachia wenye points! Ushujaa wa JK pale ulitokana na wananchi kutokuwa na mwamko wa kisiasa, kwa maoni yangu! Na in the furture wananchi wanapaswa kuwa waangalifu na kuyakusanya maswali yao kwa pamoja na kuwapatia wale wenye uwezo wa kuyauliza hayo maswali kama Mzee Boaz na Mzee William, yatayarishwe maswali mazito wapewe na kuna watu kama Abbasi, Mzee Temba ambaye swali lake la professionals, kidogo lilimtoa jasho rais, ama sivyo hiyo mikutano itakuwa ni social gathering tu, na siku zote ninawasifu wananchi wabongo walioko Mozambique, maana mara ya mwisho nilikuwa pale kwenye mkutano wa Mkapa, na wakamjia juu ju ya balozi akiwepo pale pale!, uso kwa uso, sitakaa nisahau!
 
Nungwi,

Punguza mashambulizi binafsi, Usiwe unapiga chini ya mkanda, hairuhusiwi kwenye rules za boxing.

Tuendelee na mjadala.

FD
 
Nimezungumza na mtu mmoja toka DC.. na yeye amewashangaa Watanzania kweli, kwani wamepewa nafasi ya kuuliza maswali lakini wanauliza maswali pumba...!! Huu msiba ukipita we really need to talk wazee nina mengi kweli kichwani!!!
 
Mzee Mwanakijiji,
Naona "TATIZO LETU KAMA TAIFA" ni kubwa mno! Hao walioshindwa kuuliza maswali ya maana, hawana elimu? upeo? uzalendo? (kama wanauliza maswali ili wajulikane kama wao ni "Prof au Dr au Mr so..so..au kama wanawapigia chapuo ndugu zao (hivi huyo mtoto wa Mwema, si ilisemwa kuwa baba yake (IGP) ni shemeji yake JK? Kwa hiyo anamuuliza mjomba!) au hawajui nini kinaendelea nyumbani?
 
Wazee!

Unajua waTz tuna nidhamu ya woga kwa sana. Tukikutana kwenye kona tunasema yote pamoja na kutukana. Tukipewa mic kusema mbele ya mkulu, tunaanza kubwabwaja. Sijui ni residual ya mfuma wa ujamaa na single party wakati wa JKN, not sure. Vile vile elimu yetu bado haijatufanya tuwe na independentent thinking as well as confidence. May its also due to the fact that our seniors don't take criticism positively, rather we personalise issues as it is evident even in this forum. Its time to change if we really want to develop our country.
 
mTz,
Not only seniors. Wengi tu kwenye ubosile hawachukulii criticism positively. Hata viongozi vijana.
 
Naomba nitofautiane na wachangiaji wenzangu.Naona kila mtu anawalaumu watu,lakini hakuna anayejilaumu yeye mwenyewe.Hivi kwenye hii bodi si kuna wenzetu ambao wako USA?Mwanakijiji,Administrator,Mzee ES,na wengineo?Mbona hawatuambii wao waliuliza nini badala ya kukimbilia kulaumu hao waliouliza maswali ya kizembe?Leo Tony Blair alipokuwa anahutumia conference ya chama chake cha Labour kwa mara ya mwisho kabla ya kustaafu alisema kauli moja alomfanya ashangiliwe sana.Namnukuu "Waingereza wanaweza kusahamehe na kusahau kiongozi akifanya kitu vibaya,lakini hawawezi kumsamehe au kumsahau kiongozi ambaye hakufanya kitu kabisa..."Kwa mantiki hiyo,at least hao waliouliza waliuliza,what about wale ambao hawakuuliza chochote?

Kwanini kila mara tunategemea tufanyiwe vitu badala ya vitu hivyo kufanywa na sisi wenyewe?Nadhani wenye haki ya kulaumu ni sie ambao hatuko USA (na sio wale ambao hawako New York bcoz if they were real wazalendo wangesafiri kwenda kujua hatma ya nchi yao).

Mwanakijiji,radio yako ilikuwa wapi?Hukutuma hata mwandishi wako mmoja kuuliza maswali?Au ulitaka upate exclusive interview?Sio siri,wanabodi mliopo USA mmetuangusha na nadiriki kusema kuwa lawama mnazotoa hapa ni za kuficha makosa yenu.Mtuambie mmeuliza nini na sio kusema flani aliuliza swali lisilo na mantiki...

Nadhani tatizo sio elimu wala upeo finyu,bali ni UOGA wa wale wenye uwezo wa kuuliza maswali yaliyokwenda shule.Tuachane na haka kamtindo ka kusema "flani alifanya kitu flani vibaya,badala yake iwe mimi nilifanya kitu flani (na hata kama ni kibaya bado kutakuwa na pongezi kuwa at least you did something)"

Final suggestion.Mwanakijiji,do us a little favour.Tafuta fursa ya kumhoji Jakaya.Kuendelea kuwahoji watu wanaokosoa utendaji wake ni kitu kizuri lakini kumhoji yeye mtendaji ni kitu kizuri zaidi.Mahojiano hayo sio tu yataweka historia kwa radio yako na kutuwakilisha vema wanabodi wenzio bali pia utakuwa umefanya great service to all Tanzanians especially sie wazalendo na walalahoi.

I stand to be criticized
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom