Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Wewe ungepewa ekalu kama zawadi ungerudisha?

Hapo ndipo ujue kuna viongozi waadilifu midomoni na wale ambao ni waadilifu mioyoni. JKN alipoambiwa kuhusu kujengewa ^kasri^ akajibu: ^Lijumba lote hilo kwani mi tembo!???^ Sidhani kama angepokea zawadi ya billions wakati wananchi wake wanakufa kwa kukosa dawa na huduma hata zile basic kabisa. This is ignorance of highest magnitude. Tunapaswa kutafakari sana hata haya majina tunayowaita watu waheshimiwa wakati ni full madudu, tena kwa makusudi. Viongozi wa matumbo yao wenyewe na familia zao --- huku wakitiririkwa maneno mithili ya asali kuwahadaa raia wema. Pathetic!!!
 
Prime minister wa uingerezaYuko Chini ya uchunguzi Kwa kukarabati flat wanakolala mawaziri wakuu lililo no 11 downing Street Kwa kuwa alitumia michango bila kutangazia umma nchi Tajiri kabisa inayojiweza walau.nchi yenye ufukara wa kutupwa wanajengeana ma kasiri na kuopeana hadharani kabisa mbele ya mafukara na ufukara wao. Matusi haya ya watawala wa kiafrika unahisi tuyakomeshe Kwa kuwaadhibu hasa CCM inayotuketea hawa wachumia tumbo.


Watu ni walewale -- poor thinking, visionless, selfish, wachumia-tumbo. Wako kwa ajili ya maslahi yao wenyewe. Huo ndio ukweli mchungu...
 
Yaani sheria za kinyonyaji walizojitungia wao wenyewe kujinufaisha, au ambazo hawakuzibadili wao wenyewe nazo tuziheshimu?.

Sheria hiyo mbovu ni hoja lakini hoja kubwa zaidi ni Unyonyaji uliowekwa kisheria!

Tunapinga unyonyaji na kujilimbikizia mali unaohalalishwa kisheria au unaofanyika gizani kwa mlango wa nyuma.

Huwezi kutunga sheria au kubariki sheria ya kuhalalisha embezzlement, kisha utoke hapo useme aaah siyo kosa langu mie kupewa mahekalu bali ni sheria!

sheria mliiweka wenyewe kwa hila ili kujinufaisha.

Oneni aibu kwa matendo yenu hayo
 
Naimani kwa kutumia katiba hii hii inayo walinda atatokea Rais bomu kama Jiwe na kuwanyanganya hayo makasiri walio pora pesa zetu
Mbona Jiwe liweza kupora kutumia katiba hii!!
 
hizi nyumba ni vipoozeo kwani Jiwe aliwagusa watu wao wengi. walikuwa na mishahara nje ya serikali!

acha awajengee maana kazi aliyofanya jiwe kwa washikaji wa waliomtangulia inastahili vifutia machozi kama hivi! hongera zao kwa mahekalu!

kwani pia mimi ningempa jiwe makusanyo ya mwezi mmoja TRA kama zawadi :)
 
Sijaona tatizo kwa kiongoz yeyote kulaumiwa kwenye hili. Tatizo ni sisi wananchi mazwazwa kuchagua viongoz mazwazwa kwenda kutuwakilisha kizwazwa pale bungeni. Sheria zote za nchi hii zinaanzia bungeni. Na sheria ni msumeno. Leo mwananchi unalalamika wakati mbunge wa jimbo lako kazi ni kukonga makifi wakati sheria hiz kandamizi zinapopitishwa unategemea nn?... my take. Watanzania amkeni wapimeni viongoz kabla la kuwachagua. Kwani ndio chanzo cha haya maswahibu yote yanalolikumba taifa.
 
Sijaona tatizo kwa kiongoz yeyote kulaumiwa kwenye hili. Tatizo ni sisi wananchi mazwazwa kuchagua viongoz mazwazwa kwenda kutuwakilisha kizwazwa pale bungeni. Sheria zote za nchi hii zinaanzia bungeni. Na sheria ni msumeno. Leo mwananchi unalalamika wakati mbunge wa jimbo lako kazi ni kukonga makifi wakati sheria hiz kandamizi zinapopitishwa unategemea nn?... my take. Watanzania amkeni wapimeni viongoz kabla la kuwachagua. Kwani ndio chanzo cha haya maswahibu yote yanalolikumba taifa.
Ndugu yangu, hata chaguzi zenyewe zinaibiwa ili waweke ndugu zao, rafiki zao au watu wa chama chao ili kulinda uharamia kama huu!

Tazama bungeni kuna wake, watoto, ndugu wa viongozi wastaafu kedekede, unafikiri ikipelekwa hoja ya kuzuia maslahi ya "kuvuka mipaka" ya wazee wao wataipitisha?

Wananchi huwa Tunazungumza vizuri kipindi cha Uchaguzi ila Hawa wanaojinufaisha kwa mali ya umma bila ya aibu wanaiba au kupora chaguzi.

Rejea wizi wa uchaguzi serikali za mitaa 2019, na wizi wa kura za ubunge 2020
 
Sheria ilikuwepo lakini marais wote waliona Haya kuitekeleza, akaja Jiwe mwenye PhD ya unafiki akawajengea wote Kwa mpigo. Lawama ni Kwa Jiwe sio JK
nahisi alikuwa anajijengea mazingira yeye mwenyewe pia, lakini mwisho wa siku hakupata alichokitegemea
 
Back
Top Bottom